Umesema vema, lakini kumbuka kuwa huwezi kumkamua mbuzi ambae hajazaa, watu wenye kipato/ajira wanakopesheka kwenye vyombo vya fedha, hivyo kumudu kuwekeza kwenye biashara na kilimo Kama unavyosema. Mtu ambae hana ajira/posho atapata wapi mtaji, ada na sadaka ya kutosha?
Kumbuka kwenye makanisa hata wakoloni walikuwa wanasali humo, mawaziri, wakurugenzi, maofisa na watu wengine wenye mishahara na posho za vikao na semina wengi hivyo kutoa hela nyingi ya kujenga nyumba ya ibada au shule Ni Jambo dogo. Siku ya Ijumaa ukitembelea misikiti ya Ijumaa angalia viatu vya waumini walivyoviacha nje wakati wanaingia misikitini, utangundua kuwa Hali sio nzuri kwa waliyimo ndani humo