kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,304
- 12,600
Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote wateuliwe na kuajiriwa kwa uwiano, hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.
Inahuzunisha sana kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu.
Ukifika kwenye ofisi za umma utakuta Mtumishi kaweka kwa sauti music wa dini fulani na watu hawahoji kwakuwa ni wa upande huo.
Hii sio bahati mbaya Wala coincidence. Ikumbukwe kuwa mishahara ya ajira na posho za vikao na mikutano ndizo zinazokwenda kuwekezwa kwenye elimu za watoto na maendeleo ya familia za watu waliopewa fursa ya ajira na kuhudhuria mikutano na kupata hela. Hivyo, wale wanaoikosa fursa hata familia na maendeleo yao yatakuwa duni.
Hii inasababisha maisha na familia za jamii inayopatiwa fursa hizi kuwa mbele kimaisha na kielimu. Hivyo familia za wanufaika kuendelea kutoa watumishi bora na wenye elimu shindani na wale wanaonyimwa fursa kuendelea kutoa watu wasiokuwa bora na elimu shindani kwenye ajira, "vicious cycle"
Rais anayekuja lazima azimulike ofisi zote za umma na taasisi, washa, mikutano, workshops na teuzi zote ili kujiridhisha na uwiano wa kidini pia baada ya vigezo vingine kukamilika.
Taasisi zetu za dini hazijui kazi zao au zinaogopa kutimiza kazi zao? Au ni hayo hayo matokeo ya kukosa fursa za elimu kwa njia hii?
Rais ajae pamoja na Mambo mengine ya jumla lakini autazame pia huu ufa kwenye taifa.