Raia wa Malawi aliyetibiwa Magonjwa ya Moyo, asimulia JKCI ilivyorejesha furaha yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,991
7.jpg
Jane Chimuyaka, raia wa Nchini Malawi aliyekuwa akisumbuliwa na Magonjwa ya Moyo ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kuanzisha matibabu ya moyo nchini kusaidia wagonjwa wa moyo waliopo Tanzania na nchi za jirani.

Jane aligundulika kuwa na matatizo ya moyo kupitia kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanywa na Wataalam wa Afya wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Nchini Malawi, Mei 2023 katika Hospitali ya Queen Elizabeth.

Jane alisema kupitia kambi hiyo tatizo la moyo alilokuwa nalo liliweza kuonekana na kupewa rufaa kufika JKCI kwaajili ya matibabu zaidi, hivyo kufika kwake katika Taasisi hiyo kumemsaidia kupata matibabu kwa haraka, karibu na nchi yake na kupunguza gharama kama angekweenda kutibiwa nje ya Afrika.

“Nilipofanyiwa uchunguzi pale Hospitali ya Queen Elizabeth niligundulika kuwa na mapigo ya moyo ya chini ya asilimia 30, hivyo kupewa rufaa kufika JKCI kwa ajili ya matibabu ya kuwekewa kifaa kisaidizi cha moyo (Pacemaker) na kufanya mapigo yangu ya moyo kufikia asilimia 90,” amesema Jane.

Jane amesema baada ya kupatiwa matibabu sasa anaweza kutembea kwa haraka, kupanda na kushuka ngazi, pamoja na kukimbia vitu ambavyo alikuwa hawezi kuvifanya kabla ya kupatiwa matibabu hayo.

Amesema “JKCI ni hospitali nzuri sana, Serikali ya Malawi haina haja ya kupeleka wagonjwa nchi za mbali baadala yake wawalete hapa Tanzania katika Taasisi hii kwani gharama za matibabu ni za kawaida ambazo zilipelekea hata mimi kuja hapa.”

Akizungumzia kuhusu matibabu hayo daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa JKCI, Alex Joseph alisema katika Taasisi hiyo wamekuwa wakitoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa kuwahudumia wagonjwa wa ndani na wa kutoka nchi za nje hasa za Afrika.

Dkt. Alex alisema JKCI hupokea wagonjwa wengi kutoka nje ya Tanzania hiyo imetokana na uboreshwaji wa sekta ya afya Tanzania hasa katika huduma za kibingwa zikiwemo zamatibabu ya moyo, vifaa tiba vya kisasa na wataalamu wabobezi hivyo kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Dkt. Alex amesema “Katika siku chache za hivi karibuni tumepokea mgonjwa kutoka nchini Malawi ambaye mapigo yake ya moyo yalikuwa chini sana na baada ya matibabu mapigo yake ya moyo yameimarika na kuondoa hali zote za kuumwa alizokuwa akipata kabla ya kupatiwa matibabu.”

Aidha, Dkt. Alex ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya afya na kuokoa maisha ya watanzania ambao hawana uwezo wa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu na kuiomba Serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika vifaa tiba vya kisasa na kusaidia wagonjwa waliopo nchi za jirani.
 
Back
Top Bottom