Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Kumbe tuwaachie muwe mnazikana wenyewe tuh maana mmetuona viherehere. Watanzania wote Arusha na monduli kwa ujumla jiepushane na msiba wa Lowassa msije mkapigwa ngumi za uso au risasi.

Waachieni kina Nape na Makonda hao ndio waliompenda.

Mwananchi
.kama kweli tuko makini huyu jamaa lazima achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu kulikuwa hakuna sababu yoyote ya yule mlinzi kumshambulia yule muombolezaji mimi niko tayari hata kuchangia gharama za kesi.
 
Hawa vijana wetu tunaochukua wa Div 4 ya mwisho wanatupa shida sana. Imagine Taasisi nzima inaonekana hamnazo kisa mtu mmoja kama huyu. Pole sana kwa mwathirika waa tukio hili.
Kila kitu chochote kikichukua muda mwingi athari sio ya kiuchumi hata kijamii inatatizika. Waislam akifa anazikwa chap chap kuepusha hayo
 
Kulikuwa kuna Ulazma wa Kumpiga Ngumi?
Hapana.

Je alikuwa anaonyesha Tishio au Ni yuko ana silaha au mabomu au anatishia Usalama wa Msafara?Hapana.

Shida ni nini sasa? Posho aliyolipwa kwa ajili ya Safari ya Msiba ni Ndogo? Stress za ugumu wa Maisha?.. Hasira?.. Kuonyesha kuwa anaweza kufanya Lolote na Asichukuliwe Hatua?


Kuishi Tanzania Na Ukiwa Maskini Ni bora Usizaliwe kabisa maana Utafanywa kila aina na dhihaka na dharau..
Mkuu umeongea Kwa uchungu sana
 
Kwahiyo huyo mlinzi alikuwa anahofia huyo jamaa anaweza kumdhuru kwa kumjeruhi au hata kumuua maiti! Hayo majamaa yanakuaga majinga sana hata jana pale Karimjee nilimuona askari mmoja na bunduki tena akitembea kwa madaha akilinda gari iliyobeba maiti wakati ikiondoka.
Hata mimi nilimuona pale azania front jashk linamtoka
 
Mlinzi wa msafara amtwanga bonge ya ngumi raia mwema aliyekuwa akijumuika barabarani kwenye maombolezo ya msiba wa Lowassa

Sio kwa ngumi hii aisee halafu huyu aliyepigwa inaonekana kama amekata Moto kabisa.

Mlinzi badala ya kulinda, yeye anashambulia? Kanuni za ulinzi jukumu la kwanza kabisa ni ku protect, lakini huyo ame attack first na ame attack pasipo sababu ya kufanya hivyo.
 
Ila kibongobongo huyo aliyepigwa
Ndy ashakuwa maarufu,ngoja wakina
Millard global na wambea wengine
Wamtafute wamhoji wampe airtime

Ova
 
Inasikitisha Askari huyo kufanya hivyo mbele ya jeneza la Marehemu Mh. Lowassa. Na muombelezaji Hana silaha yoyote ya kutisha uhai wa mtu..

Apewe adhabu au aachishwe kazi.. na walinzi wengine hata kumcheki jamaa.. walimlipie matibabu 100% na pesa za kumjeruhi..
Mama Samia atasema huyo siyo askari wa aliyeajiriwa na kufundishwa na Chama Cha Mapinduzi, askari wa CCM hawezi akakupiga ukaamka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom