Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
414
877
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa. Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie. Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipigia simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.
Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa.
Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.
Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie.
Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.
Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Unaeza sema umtege ukadelay ukakuta kala mzigo tayari
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbona akitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
 
Back
Top Bottom