RA ajipongeza kwa tafrija

MENGI3.jpg
 
Mkipanga kutuzuga jitahidini tuzugike.. hao waandishi wa kupewa hongo ya 10,000 wa gazeti gani? au chap chap newspaper!
 
Last edited:
Mkipanga kutuguza jitahidini tuguzige... hao waandishi wa kupewa hongo ya 10,000 wa gazeti gani? au chap chap newspaper!

Yego mkaruka kutiki,
Mimi nilidhani unaichukulia habari yote kuwa ni maskhara kumbe tatizo lako hapa ni kiasi kilichokuweko kwenye bahasha! Bahati mbaya sijui umehoji kwa sababu ni kidogo sana au ni nyingi sana. Lolote litakalo kuwa jibu ni kwamba hao waandishi ndio wa pilau na bia moja wanakupamba ile mbaya.
Na naona umetuijia na msamiati mpya; guza =zuga!!!!???? teh teh teh
 
Yaliyomo ndani ya habari yanapelekea kuifanya habari iwe ina mashiko au laa.... Kama washindwa liona hilo sorry I cant help...

Hongo ya 10,000 ni nyingi sana shilingi 1 ilitosha kabisa!
 
Wala msisituke kabisa; karibu wote wenye pesa, hata wale ambao ni majambazi (meaning waliopata pesa in questionable ways) wanalindwa na usalama wa Taifa. It is a good business for them. This is a Mafia country!!
 
Mimi naona hii habari imekaa kikufikirika vile (ya kutunga). Sijui kama ni kweli.

tatizo tunapenda kuangalia vitu kwa vipande vipande... (fractured)..
Huyu kama si muongo alikuwepo atueleze alipata posho kiasi gani.Isitoshe kama anajiona amepata ushindi ni kweli kwani hadi sasa mengi hajajibu tuhuma zote alizoangushiwa na RA badala yake kapeleka mawakili wazungumze kwa niaba yake kwenye press converence ya waandishi wake ndio maana hawakuuliza maswali kama walivyomuuliza RA.Enyi msiosikia tambueni kuwa wote hawa nimafisadi.au mnamaradhi ya kupenda.Haya washia walimshangilia sana bush alipomundoa SADAM lakini wanayopata sasa ni akher ya SADAM
 
hili la nyumba ya serikali limekaa vp? alinunua toka kwa mtu au vp?? wadau wenye data plz...
 
.....Isitoshe kama anajiona amepata ushindi ni kweli kwani hadi sasa mengi hajajibu tuhuma zote alizoangushiwa na RA badala yake kapeleka mawakili wazungumze kwa niaba yake kwenye press converence ya waandishi ....

We jamaa angu vipi?? Yaani unadhubutu kusema Mengi hajajibu tuhuma za RA. Hao mawakili walikuwa wanazungumza kwa niaba ya nani??? Open up your mind my friend!
 
hili la nyumba ya serikali limekaa vp? alinunua toka kwa mtu au vp?? wadau wenye data plz...

Ni ukweli kwamba nyumba ilikuwa ya serikali na opposite na hiyo nyumba ya RA ni nyumba ya Apson ex UWT boss. Sijui huu mpango wa kuzirudisha hizi nyumba serikalini uliishia wapi!!!!!!

Na huyu aliyeleta hizi habari hapa, kwa kuwa alikuwa mbali kama anavyosema karibu na jengo la Ernest & Young, aliwezaje kuona kwenye bahasha walizopewa waliohudhuria zilikuwa na kiasi gani cha pesa ndani? Au na yeye alikuwepo ila hapa anazuga tu!!!!!!

Tiba
 
Mzambia mmoja aliwahi nitania akisema mawaziri wa TZ ni rahisi mno, kwamba wanafanikisha dili za mabilioni kwa kuhongwa VX au shilingi milioni tano! Jamaa alisema kuwa alilishuhudia hilo kwenye tenda moja iliyohusu nchi mbili hizi ambapo waziri wetu alimuomba mwenzie amsaidie kuipatia kampuni alokuwa na maslahi nayo na weli yule mzambia alimkubalia akijua atavuta kitu ya nguvu lakini alipigwa na mshangao kubaini alipewa shilingi milioni tano!

Kwa hiyo wajameni tusishangae sana na hizo elfu kumi kwa waandishi wa habari na laki moja kwa UWT, ndio thamani yao. Ukisha ingia kwenye mtego wa kupokea rushwa na kuitumikia, unaizoea na mwisho unaridhika na chochote atakachokupa mtoaji, kwani ndiye bwana wako na unakosa ujasiri wa kumkatalia jambo.

Kwa kifupi ni aibu na hiyo ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo, hatuna tena ujasiri wa kupigania haki na rasilimali zetu, tunanunulika hata kwa 1,000/=. Kwa waandishi wa habari ndio usiseme, bia zinatosha kumpa mwandishi wa habari ujasiri wa kukiuka maadili ya kazi yake kwa ajili ya kumpamba bwana wake na kuchafua mbaya wa bwana wake, na hili liko wazi kabisa siku hizi kiasi kwamba habari nyingi zinatia kinyaa kuzisoma na sijui kama wenyewe wanalielewa hili.
 
Kila siku tunazidi kwenda chini badala ya kwenda juu lakini maadam ndio inayowapendeza Wakubwa wa humu kanyaga twende.
 
Ama kweli, Nyegela kunu Omutwale yaani waandishi wamevutwa kupokea vibahasha vya shilingi 10,000 kila mmoja.. less tham ten dollar..Wakala na kunywa sana kisha wakaimba nyimbo!... mhhhhnnnn inanikumbusha sana historia ya kukoloniwa..
Kweli - Ndivyo Tulivyo!
 
Huyu kama si muongo alikuwepo atueleze alipata posho kiasi gani.Isitoshe kama anajiona amepata ushindi ni kweli kwani hadi sasa mengi hajajibu tuhuma zote alizoangushiwa na RA badala yake kapeleka mawakili wazungumze kwa niaba yake kwenye press converence ya waandishi wake ndio maana hawakuuliza maswali kama walivyomuuliza RA.Enyi msiosikia tambueni kuwa wote hawa nimafisadi.au mnamaradhi ya kupenda.Haya washia walimshangilia sana bush alipomundoa SADAM lakini wanayopata sasa ni akher ya SADAM

Nimekuwa wazi toka awali kwamba mimi nilipiga chabo tu toka kona ya E&Y. Baada ya kushangazwa na utitiri wa wageni katika eneo hili katika muda fulani ikabidi nifuatilie.

Wakati wageni wanaanza kutoka ilikuwa bahati kumpata rafiki yangu ambaye siku nyingi namfahamu kufanya kazi UWT. Kwa hulka yake (kama vijana wengine wanao ona ufahari kusema wanafanya kazi UWT kinyume na zamani ambapo ilikuwa siri) tukapanga tukutane mahali anipe habari kamili. Ni mtu ninaye mwamini katika habari zote ambazo huropoka au kuniambia. Mida ikafika dogo akaja na kunihabarisha tukaendelea na kilaji. Mimi si mwandishi wa habari niombe vielelezo au maelezo zaidi. Na nitaumia dogo akibaini kwamba habari aliyonipa nimeibandika hapa.
 
Omutwale, ilibaki kidogo nikuulize "Source Please!!" .. ila naona umeweza toa hii habari kabla sijaweka hapa.

Ninaweza amini haya uliyotuhabarisha, nchi yetu hii imekwisha ama kweli. Ni muda wakuitikia wito wa MMM, enuff is enuff.. vita dhidi ya hawa mafisadi inahitaji kupamba moto...
 
Safi sana, baada ya kipati cha Dar aende Igunga kufanya Pati nyingine... Na huyo Nyangumi naye afanye pati yake...
 
Back
Top Bottom