Pamoja sana mkuu!!! kuna mstari kwenye Bible unasema maneno haya yasitoke kinywani mwako Bali yatafakar mchana na usiku...sikumbiki vzru ni kitabu gani but ninachotaka kusema ni iv chochote unachokipa nafasi akilini mwako utaona matunda yake iwe ni meditation ya neno la Mungu au meditation nyingine lakini mwisho itakusaidia nini kuupata ulimwengu na kuikosa nafsi yako!!!Mkuu Amri kuu ni Upendo, kuna vitu havijaandikwa popote kuhusu source of power za Mungu au za Shetani!.
Hii n i tafsiri yangu binafsi.
Kwa maana hiyo vita vyote vya Mungu na shetani, vyote vinapigwana ndani yetu, Mungu is always there ila anayewakaribisha watu wake ni wewe kwa sababu Mungu yuko ndani yetu!. Na shetani pia yupo!, anayewakaribisha watu wake ni wewe mwenyewe!. Ukiwa imara katika Mungu, shetani hawezi kufanya kitu, hata wakuloge, hulogeki hata wakutupia majini, mapepom mashetani, hayawezi kukuingia!. Anayamkaribisha Shetani ni wewe, na anayemfukuza pia ni wewe regardless unatumia jina la nani!.
- Wengi wanadhani kuwa Mungu ndio aliumba vitu vyote!, sii kweli, Mungu hakuumba vitu vyote!, bali ameumba dunia na vyote vilivyomo. Nje ya dunia, sio vyote!. Shetani yuko nje ya dunia!.
- Mwanzo wa Mungu, pia ndio huo huo mwanzo wa shetani!. Alikuwa ni 2nd in command akiwa 2nd with powers, mpaka leo mpaka kesho shetani ameondolewa tuu ile position ya 2nd in command but not his powers!.
- Mungu ni omnipotent na omnipresent, so does shetani!. Hivyo kwa vile Mungu ni power za mwanga (light) ukiwa nazo unaitwa "enlightened", na shetani pia ni power!, nguvu zake ni za giza "powers of darknes" kwa vile Mungu yupo ndani yetu, vivyo hivyo shetani yupo ndani yetu!. Ukitenda mema, ndio unatumia nguvu za Mungu, ukitenda maovu unatumia nguvu za shetani!.
- Mungu ana watumishi wake, mwanaye Yesu Kristo, Malaika na Roho Mtakatifu ambavyo vyote pia ni powers na ukitenda mema, huwakarinisha ndani yetu. Shetani pia anakundi lake la malaika wabaya, mapepo, majini, maruhani, liroho!.
- Ukimtumiakia Shetani, wenyeji wa mwili wako wanakuwa ni watumishi wa shetani, ndipo unaposikia fulani ana mashetani, majini, anatumia nguvu za giza!, wale watumishi wa Mungu, wanakukimbia!. Ukitumia nguvu za Mungu, watumishi wa shetani wanakumbia, na ndio hao mapepo wanaotolewa!. Kinachotolewa kwako ni watumishi tuu wa shetani au watumishi wa Mungu, sio Mungu mwenyewe wala sio shetani mwenyewe!.
Pasco.
Sent using Jamii Forums mobile app