Protase Rugambwa: Askofu Mwandamizi Anayeripoti Kituo chake cha Kazi Jimboni Tabora 25 Juni 2023

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,055
2,602
1687379174039.png
Jumapili ijayo Juni 25, 2023, jimbo la Tabora linampokea askofu mkuu Protase Rugambwa akitokea Roma alikokuwa kwenye jopo linalomsaidia Papa kuongoza kanisa duniani. Jopo hili linaitwa "Roman Curia" lina idara zinaitwa "dicastery" na moja ni ya "Uenezaji Injili Duniani".

Akiwa bado padri Protase Rugambwa alikuwa kwenye idara hiyo akahamishwa kuwa askofu wa Kigoma. Juni 26, 2012, Papa Benedict XVI alimrudisha Roma kuwa katibu msaidizi wa idara hii.

Papa Benedict XVI vilevile alimpa uaskofu mkuu japo hakumpa jimbo kuu kama mwenzake Novatus Rugambwa aliyepewa jimbo kuu la Tagaria. Uaskofu mkuu huu unaitwa "ad personam" yaani ni wa askofu yeyote asiye na jimbo kuu.

Novemba 17, 2017, Protase aliteuliwa kuwa katibu wa hiyo idara. Aprili 13, 2023 Papa Francis alimteua Protase kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Tabora, jimbo linaloongozwa na askofu mkuu Paul Ruzoka.

Protase anakuwa askofu mwandamizi wa pili jimboni Tabora na wa nane hapa nchini, orodha yao na miaka yao walipoteuliwa ni hii, Joseph Sweens (Mwanza, 1910), Henri Leonard (Tabora, 1912), Victor Haelg (Lindi, 1949), Tarcisius Ngalalekumtwa (Sumbawanga, 1988), Polycarp Pengo (Dar Es salaam, 1990), Castor Msemwa (Tunduru-Masasi, 2004), Jude Thadaeus Ruwa'ichi (Dar Es salaam, 2018) na sasa Protase Rugambwa.

Mei 26, 2010, Jose Gomez, alipowasili kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Los Angeles, Marekani, walikuwepo makardinali sita na maaskofu 56.

Hata Jumapili, askofu Protase atakapowasili Tabora inatarajiwa wawepo maaskofu wengi. Hivyo litakuwa ni kosa kubwa televisheni za kanisa zisipolitangaza moja kwa moja tukio hilo.

Je kazi ya askofu mwandamizi ni ipi? Makala hii inajibu swali hili kwa kuanza kuieleza historia ya "uaskofu mwandamizi" ambao kwa Kiingereza unaitwa "coadjutor bishop".

Mwaka 215 askofu Narcissus wa Jerusalem alifikisha umri wa miaka 116 hivyo Alexander akateuliwa kuwa askofu mwandamizi.

Mwaka iliofuata askofu Narcissus alifariki dunia akamwacha askofu Alexander jimboni. Mfano huu wa Jerusalem ndiyo hurejewa kama historia ya uaskofu mwandamizi.

Askofu wa jimbo anapoondoka, kiti kinapata uwazi unaoitwa "sede vacante". Askofu akiwa hajaondoka, kiti hakiwi wazi na hali hiyo inaitwa "sede plena". Kuwasili kwa askofu mwandamizi kunamuweka na yeye kwenye kiti hicho.

Askofu wa jimbo akiondoka kiti hakitabaki wazi kwa sababu kuondoka kwake kumembakisha mwenzake kitini. Hivyo jimbo likishapata askofu mwandamizi haliwezi kuwa wazi hata kwa robo sekunde.

Juni 27, 1912 kifo cha askofu Franbois Gerboin pale Tabora hakikuacha kiti cha Tabora wazi kwani Henri Leonard alishakuwa askofu mwandamizi tangu jana yake.

Watu kadhaa wametafiti madaraka ya askofu mwandamizi, baadhi yao ni David Yallop na John Conroy.

David Yallop anaeleza kwamba askofu mwandamizi akishafika, askofu wa jimbo hilo anakuwa "titular" yaani hana tena mamlaka ya jimbo (In God's Name, toleo la mwaka 2007, uk. 181).

David Yallop anaungwa mkono na utafiti wa John Conroy alioutoa kwenye gazeti "Chicago Reader" la Juni 04, 1987.

Hata ndani ya kanisa wapo walitafiti nafasi hii ya askofu mwandamizi kama Miriam Wijlens na padri Pawel Lewandowski.

Miriam Wijlens alitoa utafiti wake unaiotwa "The Bishop as Legislator" kwenye jarida "The Jurist 56, no. 1" katika ukurasa wa 68 hadi 87. Januari 25, 1983, Papa John Paul alitangaza sheria inayoitwa "Code of Canon Laws" yaani "Sheria za Kanisa".

Utafiti huu wa Miriam Wijlens alioutoa mwaka 1996 ulikuwa unafafanua kanuni ya 391(2) ya Sheria za Kanisa inayosema kwamba askofu wa jimbo ndiye mtu pekee anayepaswa kutunga sheria jimboni na si mwingine yeyote.

Miriam Wijlens anafafanua kwamba hata askofu mwandamizi ana mamlaka hayo ya kutunga sheria. Askofu anapotunga sheria huwa haitumiki, inasubiri kwanza upite muda unaoitwa "vacatio legis" yaani muda kuanzia siku sheria ilipotangazwa hadi siku itakapoaza kutumika. Kanuni ya 8(2) na 9 ya Sheria za Kanisa inasema muda huu "vacatio legis" ni mwezi mmoja.

Tumeona kwamba kuwasili kwa askofu mwandamizi kunamaanisha askofu wa jimbo anaondoka jimboni sekunde yoyote.

Katika hali hiyo askofu wa jimbo hawezi tena kutunga sheria wakati anaondoka jimboni sekunde yoyote ijayo. Hivyo, askofu mwandamizi ndiye mtunga sheria za jimbo.

Padri Pawel Lewandowski ni mtaalamu wa teolojia na sheria za kanisa na amekuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha John Paul II cha Krakow, Poland. Padri Lewandowski katika utafiti wake wa mwaka 2015 anaiheshimu hoja hii ya Miriam Wijlens.

Januari 24, 2004, Papa John Paul II alileta sheria maalum kwa ajili ya kuwaongoza maaskofu tu. Sheria hiyo inaitwa "Apostolorum Successores" yaani warithi wa mitume. Kanuni ya 70 hadi 74 ya sheria hii imedhibiti matendo ya askofu wa jimbo na askofu msaidizi (auxiliary bishop).

Kanuni ya 70 na 71(d) inaelekeza kwamba askofu msaidizi anapangiwa kazi na askofu wa jimbo na ni mtii kwa askofu wa jimbo.

Kanuni ya 72 ya "Apostorolum successorem" inamzuia askofu wa jimbo kufanya jambo lisilokubaliwa na askofu mwandamizi.

Hivyo jambo tunaloona limefanyika jimboni basi hilo ndilo limekubaliwa au limeruhusiwa yaani halijazuiwa na askofu mwandamizi.

Kanuni hii inamgeuza askofu wa jimbo kuwa muomba ruhusa na kumfanya askofu mwandamizi kuwa mtoa ruhusa jimboni.

Hakuna kanuni hata moja inayomuagiza askofu mwandamizi kwenda kwa askofu wa jimbo ili akubaliwe analolitaka jimboni.

Wapo wanaosema kwamba kazi ya askofu mwandamizi ni kumsaidia askofu wa jimbo. Kazi ya kumsaidia askofu wa jimbo siyo ya askofu mwandamizi (coadjutor bishop) bali ni ya askofu msaidizi (auxiliary bishop).

Hata rais wa baraza la maaskofu hawezi kuwa ni askofu anayemsaidia askofu mwenzake. Askofu mwandamizi akishawasili hata askofu wa jimbo naye hawezi kuwa rais wa baraza la maaskofu wakati askofu mwandamizi anaweza kuwa rais wa baraza hilo.

Pierre Nhon alikuwa rais wa Baraza la Maaskofu la Vietnam mwaka 2010 akiwa ni askofu mwandamizi wa jimbo la Ha Noi. John Njue alikuwa rais wa Baraza la Maaskofu la Kenya mwaka 1996 akiwa ni askofu mwandamizi wa jimbo la Nyeri.

Hivyo Protase Rugambwa anaweza kuwa rais wa Baraza la Maaskofu la Tanzania (TEC) akiwa ni askofu mkuu mwadamizi wa Tabora.

Je, askofu mwandamizi anawasili vipi jimboni? Utaratibu wa kuwasili huelekezwa na Papa mwenyewe kwenye barua ya kumteua askofu mwandamizi.

Mara nyingi barua hiyo huwa inamuagiza askofu mwandamizi akajitangaze kwa waumini wa jimbo analokwenda.

Barua ya Papa Francis ilimuagiza askofu Jude Thadaeus Ruwa'ichi kwa maneno haya, "Tunakuagiza kuwajulisha barua hii makleri na watu wote wa Jimbo Kuu la D'Salaam.

Hao wote ni wana wapenzi tunawahimiza, wakupokee na kukuheshimu, wakiungana nawe katika umoja ."

Je ni tukio gani linafuata ikishasomwa barua hiyo ya kumteua askofu mwandamizi? Baraza la maaskofu wa England na Wales limefafanua vizuri katika waraka unaoitwa "Installation of a Bishop".

Sentensi ya mwisho ya ukurasa wa nane wa waraka huo inasema kwamba tukio linalofuata ni kumkalisha askofu mwandamizi kwenye kiti cha uaskofu (https://www.liturgyoffice.org.uk/Resources/Rites/Reception-Bishop.pdf).

Roger Kardinali Mahony alitumia mtindo tofauti siku askofu mwandamizi Jose Gomez alipowasili Los Angeles. Kardinali Mahony alisubiri mwishoni mwa ile misa ndipo akamkalisha kwenye kiti cha askofu. Kitendo hicho cha kumkalisha kitini kinaonekana kwenye video hii (www.youtube.com/watch?v=IB5Ynw8YOgs).

Hivyo, haijajulikana kama askofu Potase Rugambwa naye atakalishwa kwenye kile kiti baada tu ya kusomwa barua ya uteuzi wake kama wanavyofanya maaskofu wa England na Wales au mwishoni mwa misa kama alivyofanya Kardinali Mahony.

Jambo jingine ni matumizi ya hili neno "askofu mwandamizi". Safari hii tangazo la lililotujulisha uteuzi wa askofu Protase Rugambwa limetumia neno "askofu mrithi".

Tupo tunaosita kutumia hili neno "mrithi". Kifungu cha 861 na 862 cha Katekism ya Kanisa Katoliki kimetufundisha wakatoliki kwamba pale Roma papa ni mrithi wa mtume Petro na huku majimboni maaskofu ni warithi wa mitume.

Hivyo hakuna askofu ambaye siyo "mrithi" kwani kila askofu ni mrithi wa mitume. Wenzetu katika Kilatini na Kiingereza kwa karne nyingi wamebaki na neno lilelile "coadjutor". Hata sisi tunaweza kutumia neno "askofu mwenza" ambalo halibadilikibadiliki.

Askofu Protase sasa anarejea Tanzania baada ya kuishi sana Roma tena mara mbili. Majukumu yake kule Roma yalikuwa ni mengi na mazito.

Maaskofu wote wa Afrika, Asia na eneo linaloitwa Ocenia wanasimamiwa na idara hii. Jukumu jipya la kuinjilisha upya Ulaya na kwingine kote kunakoporomoka imani ni la idara hii. Mashirika ya umisionari kama vile Maryknol, Jesuit na wengine, yanaratibiwa na idara hii.

Hivyo askofu Protase Rugambwa kadhihirisha kwamba wapo watanzania ambao wakipewa nafasi wanaonyesha uwezo mkubwa wa kiakili wa kufanya majukumu au mambo makubwa duniani. Hivyo makala hii inasema karibu tena nyumbani askofu mkuu Protase Rugambwa baada ya kazi nzito kule Roma.

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Mwansishi: JOSEPH MAGATA
Email: josephmagata@yahoo.com
Simu: 075 4710684
Mchapishaji: Gazeti la Jamhuri, JUmanne, 20 Juni 2023, uk. 10

Hivyo askofu Protase Rugambwa kadhihirisha kwamba wapo watanzania ambao wakipewa nafasi wanaonyesha uwezo mkubwa wa kiakili wa kufanya majukumu au mambo makubwa duniani.
Effectively demoted.

Karudishwa kwao, kaonekana hafai kupelekwa hata Msumbiji.

Sasa sijui kadhihirisha vipi kwamba "wapo watanzania wakipewa nafasi... wanaonyesha uwezo mkubwa wa kufanya majukumu makubwa duniani.
 
Wewe ndiye mbumbumbu hujui mambo ya Roma,

Nafasi za Roma kama hiyo muda wake ni miaka kumi tu wanapewa wengine.

Pambafu.

Effectively demoted.

Karudishwa kwao, kaonekana hafai hata kupelekwa Msumbiji?.

Makala nzuri... Asante kwa Shule hio
 
Back
Top Bottom