Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Nitakuambia kitu kimoja (au viwili) na vinahusiana. Watu wengi wana mapenzi sana na CDM si kwa sababu wanajua CDM itafanya nini; wana mapenzi kwa sababu wanajua CCM imefanya nini. NI mapenzi yanayotokana na chuki. Mapenzi haya hayakuanzia CDM; baada ya vyama vingi kurudi wale waliokuwa wamechoshwa na CCM mara moja wakajitambua kuwa ni wapinzani na wakaenda nyuma ya wale waliokuwa wanaipinga CCM. Nakumbuka vizuri sana 1995 nilimpigia kura Mrema; tulikuwepo watu wengi ambao tulichagua NCCR kwa sababu ya kuchoshwa na CCM na kutaka kitu kipya.
Kuna vitu vingine ni rahisi thibitisha.Mimi sikuipenda CDM kwa hayo uliyosema.Halafu unacholinganisha ni Ni past ya CCM na future ya CDM.Ni rahisi kuona wapi hujaelewa au kuchanganya vitu.Im sure pia hujui nini CCM watafanya
kama ungelinganisha hivyo.Na pia unajua nini CDM wamefanya na wanafanya.Otherwise utakuwa ukituambia huijui CDM halafu unataka ishauri.
Lakini na pili na hili ni kubwa sana natumaini utalizingatia; wengi ambao tumekuja kuiunga mkono CDM na kuisaidia tunafanya hivyo kwa sababu ya kuamini kuna potential ya kuweza kuja kushika madaraka. Ni potential hii ambayo inawapa watu wengi matumaini kuwa CDM ikitulia, ikajipanga na kujitengeneza kweli inaweza kuwa chama cha kuweza kushika madaraka. Sasa usifikirie kupendwa kunakotokana na hili kunatosha. La hasha! Na itakuwa ni makosa makubwa zaidi kufurahia vigelegele, chereko na shangwe na kuamini kuwa hawa watu watakuwa pale siku zote kwa vile CDM inapendwa.
Sidhani kama kinachoonekan literally ndicho ulichomaanisha?Kama ndivyo basi sitoogopa kusema kuwa kati yenu wengi (wengi kati ya kundi lako na si la wana CDM) ni opportunistic.Yaani mnaangalia chama kinachoonekana kwenda chukua nchi.Sipendi amini hivyo ila ndicho unachokisema hapa kw atafsiri literally.Na hii itanisikitisha sana

Watu wanaipenda kwa sababu wanaichukia CCM na hawaoni mwingine wa kumpenda na wanaipenda kwa sababu inawapa matumaini kuwa inaweza kuwa. Binafsi, sasa hivi nitafanya yote ninayoweza kuweza kusaidia CDM ishinde na kufanya vizuri zaidi 2015. Lakini siko tayari kusaidia ili ipate wabunge wengi na ijipange tena kwa 2020! utakuwa ni wazimu. Kama haitajipanga kushika madaraka ya nchi 2015 wakaendeleea na status quo itakuwa ni jukumu la dhamiri kuanza kuipinga kwa sababu itakuwa inasimama kama kikwazo; watu wanatumaini lakini tumaini halilipi!
Ni vigumu kuthibitisha kuwa watu wote wanaipenda CDM kwa sababu wanaichukia CCM.Pengine kitu ulichochanganya hapa ni kwamba.Kuna kupenda, kuchukia, na kutopenda wala kuchukia,na hivi vyote vinaweza shawishi choices za watu au lah.Wapo watu wanaochagua watu wasiowapenda ili wawe katika timu yao ingawa hawawapendi ila kwa vile wanavikubali vipawa vyao au hata ni convenient kufanya hivyo.

Untahitaji thibisha sababu pekee za watu kuipenda CDM ni kuichukia CCM na kama sivyo basi uonyeshe kwa kiasi gani basi sababu nyingine zisiwe significant.Mojawapo ninayoiona ni karama za viongozi wake, ambayo pia imewachanganya wafuasi wa Zitto na Zitto mwenyewe akadhani kuwa karama zake pekee ndio zimefanya kazi CDM.Kuna mara nyingi hata wewe umeonekana kuegemea ktk hizi fikra.Kuna ambao wamefurahia jinsi CDM wanavyoingia ktk problems na CCM na kuweza toka salama na kwa ushindi mkubwa.Pia uongozi mzuri na mipango mizuri ya CDM imeweza fanya CDM kuwa mbadala katk fikra na mioyo ya watanzania na wageni waliopo nchini.Na hapa ndipo ninapoona unajaribu kwepa ili uweze pana tafsiri zako nyingi sana. Iam sure CDM wasingekuwa na mipango mizuri,uongozi bora ambao kila siku unahitaji thibisha kitu mbele ya critics,isingeweza tulia na viongozi wenye fikra huru na wenye ushawishi binafsi kwa raia kama waliopo sasa hivi.Kwa kiasi fulani naona jinsi mnavyokosa shikilia issue za msingi ndivyo mnavyojikuta mnapata theories nyingi za kuilezea CDM kama vile ni chama kilichotoka mwezini.CDM tupo nayo hapa wanafanya vitu practical zaidi ya maneno.Napata shida kuwasikia wana CCM wakitoa theory nyingi kuhusu CDM kuwaeleza watu watu vitu vinavyoonekana ktk wazi katk mikutano.Mikutano ya CDM nimeingia amani ipo juu,professionals wanachat, vilema wanacheza na watu, halafu huku nje wana CCM wanashupaa kuelezea jinsi CDM wanavyopoteza amani.Tusieelezee hisi zetu tuelezee realities.
Utanielewa baadaye nikimaliza kazi ya tatu ya CDM kuelekea 2015. Usinielewe vibaya kabisa CDM ndani ya miaka hii mitatu imefanya vizuri lakini vile vile tunashuhudia its weakest points na hizo zinatisha zaidi kwani hazikuwepo 2010! think about it.
Okay,nadhani na wewe pia unaamini kuwa neno lako si perfect km lilivyo la CDM na mimi pia.Na wafanyalo CDM mengi huafiki na hukuwahi hafiki(ndio maana hukuwa ukiwakubali).Lakini kila siku wanakwenda mbali sana, wanawashtua CCM na wapinzani.Na milestones zako zinapitwa kwa mafanikio kama CDM walivyopanga.Huoni uwezekano wa kuwa sahihi tukisema theories zako si practical ndio maana CDM hawakuzichukua?CDM walijiwekea malengo ya kuanzia ktk serikali za mitaa,ubunge na baadaye urais.Walipokuwa na wabunge 4 tuu CCM inaanza ona ugumu wa maisha.Wakaongezeka watu wakaona sasa kifo cha CCM kimekaribia,sasa wakiongeza tena CCM itakuwa ktk comma.

Pengine ningependa kushauri km utabase kazi zako katk misingi iliyo nje ya reality utaishia kuandika scripts nzuri sana gramatically and structurally,lakini intellectually ukawa unajilisha uongo.Kwanza rudia sababu zako kwanini watu wanapenda CDM, na takwimu zake kwa asilimia, pia uweze predict factors zitakazoweza shift hizo asilimia kwa watu watu waliopo na watakaoongezeka.

Pia ningependa utuambie maelezo yako yanalenga wapi?Je yanalenga CDM kushinda uchaguzi mkuu?Au yanalenga kuwasaidia ongoza baaa ya ushindi?Au vipi?Mimi sioni kama CDM wanashinda kwa watu kuichukia CCM,a ukuwachukia wana CCM,au kuyachukia matendo ya CCM pekee.Km ingekuwa hivyo basi vyma vingine navyo vingekuwa na nguvu.Otherwise watu wanaipenda CDM kwa vile CDM imeweza wapendezesha watu.This is more plausible.
 
Ukisoma katiba ya chadema huwezi kujuwa watakachokifanya?Ndiyo maana nikasema contextually,wewe hukubaliani na uongozi wa chadema.

Watakachofanya chadema,kila siku viongozi wake wanahubiri majukwaani,ni kinyume kabisa na walichofanya ccm kwa miaka 50 toka uhuru!

well said
 
Pia ningependa utuambie maelezo yako yanalenga wapi?Je yanalenga CDM kushinda uchaguzi mkuu?Au yanalenga kuwasaidia ongoza baaa ya ushindi?Au vipi?Mimi sioni kama CDM wanashinda kwa watu kuichukia CCM,a ukuwachukia wana CCM,au kuyachukia matendo ya CCM pekee.Km ingekuwa hivyo basi vyma vingine navyo vingekuwa na nguvu.Otherwise watu wanaipenda CDM kwa vile CDM imeweza wapendezesha watu.This is more plausible.

whaaat!!? unamsifia mtu kwa kuvaa vizuri na kufikiria ana hela mfukoni? au anasifiwa mwanamke kwa kujipamba ukadhani anaoleka. Ni kweli inawezekana CDM imewapendezesha watu lakini historia ni mwalimu mzuri tu CCM imewahi kuwapendezesha watu, NCCR vile vile imewahi kuwapendezesha watu. Nicholas, we need to want more and demand more kama kweli tunataka CDM ije kushika hatamu za uongozi wa nchi. Don't be blinded by love; it has a blinding force. Wengi wameumia moyoni kwa kufuata moyo zaidi...
 
thats exactly my point...

Unajua watafanya nini kuhusu usalama wa taifa? watafanya nini kuhusu polisi? watafanya nini kuhusu elimu yajuu? hivi umesoma lini kweney hiyo mikutano ya majukwaani ambacho CDM watakifanya. Nitafutie mkutano mmoja wa karibuni ambapo CDM wamesema wao wakiingia madarakani watafanya nini kunipa mfano.
Haya yote huwezi weka details kama haupo madarakani ili kuweza kuwa na access kamili ya current situations.Unless CDM wanaiba taarifa muhimu, hawawezi pat aushirikiano wa kutosha kwenye kupata taarifa muhimu zaelimu ya juu,usalama wa Taifa etc.

Sijui unasema usalama wa taifa kwa mapana gani.ILa kama ujuavyo usalama wa taifa hauwezi wekwa kirahisi ktk katiba ya Chama pinzani ambacho hakijawahi tawala ktk nchi isiyo national Policies.Pia ni wazi usalama wa taifa kama taasisi inayoweza toa taswira halisi ya usalama wa taifa letu ulivyo sasa na tunapoenda.

Pengine Mzee Mwanakijiji unaelezea wasiwasi wa watu wa usalama wa taifa,kuwa CDM inawahakikishia vipi usala,a wao kwa vile wamekuwa wakifanya kazi ya CCM na si ya Taifa.Hii ni wazi Taasisi itavunjwa na kujengwa upya kwa mitizamo ya CDM.Sasa kuna watakaobaki kwa uozoefu wao na maslahi Taifa na kuna watakaobaki kwa maslahi ya CDM.Elimu ya juu pia ndivyo hivyo.
 
whaaat!!? unamsifia mtu kwa kuvaa vizuri na kufikiria ana hela mfukoni? au anasifiwa mwanamke kwa kujipamba ukadhani anaoleka. Ni kweli inawezekana CDM imewapendezesha watu lakini historia ni mwalimu mzuri tu CCM imewahi kuwapendezesha watu, NCCR vile vile imewahi kuwapendezesha watu. Nicholas, we need to want more and demand more kama kweli tunataka CDM ije kushika hatamu za uongozi wa nchi. Don't be blinded by love; it has a blinding force. Wengi wameumia moyoni kwa kufuata moyo zaidi...

Wakuu Mkandara, Pasco, karibuni kwenye munakasha huu.
 
Last edited by a moderator:
1.MKJJ yuko katika payroll ya Serikali katika kazi ya usalama wa Taifa. Majukumu yake hayafuati muundo wa kawaida(organogram) uliopo.

2. MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.

MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Ministry of Defence).

3. Kwa sasa MNKJJ anafanya kazi ya kunusa na kuwachanganya Watanzania kwa kuandika na kuongea kwa style ya kukandia Serikali kwa sana kupitia majamvi na majukwaa mbalimbali kama vile JF na magazeti mbalimbali yaliyo katika mtandao.

4. Kwa kutumia utaalamu wake wa sanaa na fani ya uandishi na utangazaji, MKJJ anajificha ndani ya mbinu ya kijasusi ijulikanayo kama ‘The Italian Strategy of Tension with False Flag'. Ingawa ni mwanachama CCM lakini anapokuwa mtandaoni huvaa ngozi ya mbwa mwitu na kujiita Mkuu wa Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani (TAKIDEMA). Kazi zake ni kama ifuatavyo:-

a. Kuanzisha mada chokozi (provocative topics) zenye kuleta hisia kali akisukuma makombora kwenye Serikali ikiwa ni namna ya kuwachokoza wananchi ili mnapoanza kusema au kuandika basi yeye anachukuwa notisi zake na kuwakabidhi waliomtuma kwa ajili ya kurekebisha panapotakiwa haraka iwezekanavyo mfano katika moja ya jibu lak leo humu katika thread hii amesema aliyependekeza IGP Mahita aondolewe na ndie alitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.. Hadhira yake kusudiwa ni hasa Watanzania walioko nje na hususani wasomi ambao wanaweza kuleta upinzanina ndio hawa aliokwaruzana nao wakati anapinga swala la uraia wa nchi mbili. sababu iko wazi nayo ni "you are either with us or against us.....I'M out!!

Hasa hapo kwenye red umenigusa kwani ni ukweli kabisa. MMKJ anatuchanganya sana Watanzania wanaofuatilia maandiko yake na ukitaka kuhakikisha namna anavyofanya kazi kwa niaba ya Usalama wa Taifa angalia msimamo wake kuhusu CDM.

Tuliona 2010 wakati anaiponda CDM na kuikumbatia CCJ iliyokuwa imeanzishwa. Mission ya MMKJ ilikuwa ni kujaribu kukidhoofisha CDM ili kmigawanyike na wafuasi wake wengine waende CCJ.

Yaani MMKJ ni mtu hatari sana kwa ukombozi wa pili wa taifa hili. Yuko tayari kuhamisha nguzo ya goli iwapo inaonekana CDM, au chama chochote kingine cha upinzani kinakaribia kufunga goli. Yaani ataiponda serikaliiiiii (ili kujenga imani kwa wanaomsoma)lakini up to a point. Kapangiwa line yake ambayo hatakiwi kuivuka.

MMKJ is a very dangerous specie, I'm sorry to say.
 
Kweli miaka yote hii na utetezi wote huu unachokumbuka ni sementi 5000 na somehow kudeal na inflation? Huna chochote ambacho unajua wamesema watakuja kufanya kwa sababu unaamini watafanya hata kama hujui ni nini? Sasa unawaunga mkono kwanini? Well, kwa sababu wana nia nzuri ya kuiondoa CCM? au kwa sababu wana watu wanaozungumza vizuri sana kuhusu matatizo yetu? ama unawaunga mkono kwa nini? au hujali kutaka kujua nini wanataka kufanya?

Mwanakijiji usipende kuweka viwango ambavyo hata wewe mwenyewe huwezi vifuata.Kwanini unkimbizana na mifano?Mifano ni sehemu ya set kamili na ukamilifu wenyewe.

Kuiondoa CCM ni njia rahisi kuondoa shida zote zihusiano nazo na CCM.Na haki ya watanzania kutokuwa na shida hata kama hawatajenga vitu vipya.Huwezi mlalamikia mtu anayesema kuwa anaweza toa virusi vya ukimwi mwilini,kwa kumtaka aseme ni vipi ataimarisha afya ya mhusika.Kuondoa tatizo na kuwapa watanzania uhuru ni ushindi wa kwanza.Kujenga nchi ni jukumu la pamoja lakila raia.(atakayekuwa kawekwa huru).

So naona Mzee mwanakijiji jikite ktk context sahihi zaidi ya kuweka vitu ktk kapu moja kwani utajikuta ukijipa maeneo mepesi mengi yasiyo hasilia ili kushambulia vitu halisi.
 
.

Kuiondoa CCM ni njia rahisi kuondoa shida zote zihusiano nazo na CCM.Na haki ya watanzania kutokuwa na shida hata kama hawatajenga vitu vipya.

laiti ungejisikia ulichosema hapo!; wewe endelea kwa msimamo huo na miye nitaendelea na wa kwangu; ndio uzuri wa uhuru.
 
Hasa hapo kwenye red umenigusa kwani ni ukweli kabisa. MMKJ anatuchanganya sana Watanzania wanaofuatilia maandiko yake na ukitaka kuhakikisha namna anavyofanya kazi kwa niaba ya Usalama wa Taifa angalia msimamo wake kuhusu CDM.

Tuliona 2010 wakati anaiponda CDM na kuikumbatia CCJ iliyokuwa imeanzishwa. Mission ya MMKJ ilikuwa ni kujaribu kukidhoofisha CDM ili kmigawanyike na wafuasi wake wengine waende CCJ.

Yaani MMKJ ni mtu hatari sana kwa ukombozi wa pili wa taifa hili. Yuko tayari kuhamisha nguzo ya goli iwapo inaonekana CDM, au chama chochote kingine cha upinzani kinakaribia kufunga goli. Yaani ataiponda serikaliiiiii (ili kujenga imani kwa wanaomsoma)lakini up to a point. Kapangiwa line yake ambayo hatakiwi kuivuka.

MMKJ is a very dangerous specie, I'm sorry to say.

Oh boy.. na wewe kweli umeamini hayo. ukiwauliza wa upande mwingine wata beg to differ.
 
Pengine Mzee Mwanakijiji unaelezea wasiwasi wa watu wa usalama wa taifa,kuwa CDM inawahakikishia vipi usala,a wao kwa vile wamekuwa wakifanya kazi ya CCM na si ya Taifa.Hii ni wazi Taasisi itavunjwa na kujengwa upya kwa mitizamo ya CDM.Sasa kuna watakaobaki kwa uozoefu wao na maslahi Taifa na kuna watakaobaki kwa maslahi ya CDM.Elimu ya juu pia ndivyo hivyo.

sawa; nyinyi subirini waingie madarakani ili wawaambiwa watafanya nini; sisi wengine tutataka tujue watafanya nini ili tujue kama wanastahili kuingia madarakani ili tuwasaidie.
 
whaaat!!? unamsifia mtu kwa kuvaa vizuri na kufikiria ana hela mfukoni? au anasifiwa mwanamke kwa kujipamba ukadhani anaoleka. Ni kweli inawezekana CDM imewapendezesha watu lakini historia ni mwalimu mzuri tu CCM imewahi kuwapendezesha watu, NCCR vile vile imewahi kuwapendezesha watu. Nicholas, we need to want more and demand more kama kweli tunataka CDM ije kushika hatamu za uongozi wa nchi. Don't be blinded by love; it has a blinding force. Wengi wameumia moyoni kwa kufuata moyo zaidi...

teh teh.Naona umeamua chagua cha kujibu na kuelezea.Umeamua chukua "neno pendezesha" ambalo kwa kiasi kikubwa ni wazi pia upo out of context.Neno "kupenda" linalosema ction inayofanywa na anayependa, nimeligeuza kumaanisha CDM kuwafanya hawa watu "wawapende" nikatumia kupendezesha.Wewe kama msomi hukupoteza muda kuangali au ahta kuniuliza tena niweke sawa mambo.Ni busara na haki yako kujiridhisha na swali au kauli kabla ya kuendelea.Umeruka mengi ili uchague unaloona kuwa ni jepesi(huku niku compromise fairness),mbaya nacho umekosea.mimi siongei "pendeza " ya muonekano au attractiveness.Na hata kama ingekuwa hivyo bado pia umekosea kwani mimi nimesema CDM kuwapendezesha watu na si kujipendezesha.kama CDM wamependezesha/wapamba watu wakapendeza hata bila kuolewa hawa watu watawapenda CDM kwa hilo.

The more unajitahidi kuwa dishonest the more unajiweka sehemu ngumu kujibu maswali ya watu wengi.N kadiri unavyoweza act kuwa na fikra huru na honest ndivyo unavyozidi kujiweka ktk mazingira ya kuwa slanderer zaidi ya valuable critic.
 
laiti ungejisikia ulichosema hapo!; wewe endelea kwa msimamo huo na miye nitaendelea na wa kwangu; ndio uzuri wa uhuru.

Sasa mbona unaanza jenga tena hisia za kususa?MMK mimi naamini wewe ni mtu influencial na unaweza ukajikuta sehmu muhimu san aktk hii nchi.Kuna mambo mengi ya nchi kususa si solution il ani problem halisi.Imagine rais au balozi anasusia issue kama Inayohusu mpaka wa malawi?

Nilitegemea uwe na ujasiri na kutokata tamaa kama image uliyojenga inavyweza display.Why are you crashing so quickly?
 
Wakuu Mkandara, Pasco, karibuni kwenye munakasha huu.
Mkuu Ritz, mimi nipo nasoma mstari kwa mstari!, kuna mengi nilishayasema humu ikiwemo Chadema hawajajipanga, nilitukanwa sana humu!, leo yale yale niliyoyasema kayasema Mzee Mwanakijiji, japo Edson, J.Mushi na Nicholas wanaendelea kukaba mpakja kona, ila anaheshimiwa bila kutukanwa!.

Nilisema humu ili Chadema ishinde 2015, inatakiwa kuujua mtaji wake wa ushindi na kuutumia kwa kusema itafanya nini na sio kukomalia tuu maandamano na siasa za chuki dhidi ya CCM, leo hiki kitu kimesemwa humu na Mzee Mwakijiji!.

Niliposema 2015 ni CCM tena, nimebezwa sana humu! ila ukimsoma Mzee Mwanakijiji in between the lines kwa jinsi anavyoilezea Chadema jinsi ambavyo haijajipanga, and by now ilipashwa kuwa imeshajipanga, utajua kuwa anajua wazi 2015 ni CCM tena!.
P.
 
sawa; nyinyi subirini waingie madarakani ili wawaambiwa watafanya nini; sisi wengine tutataka tujue watafanya nini ili tujue kama wanastahili kuingia madarakani ili tuwasaidie.

kwanini una crash ktk mazungumzo amabyo hayajawa hata hot?Sasa CDM wakikufuata wewe si watakuwa kituko sana ndugu yangu?Naomba jikaze na kutoa majibu na challenges za msingi na si kususa susa kama mkandara, huyu mkndara hadi yuko very volatile na sitegemei wewe kuwa hivyo.
 
The more unajitahidi kuwa dishonest the more unajiweka sehemu ngumu kujibu maswali ya watu wengi.N kadiri unavyoweza act kuwa na fikra huru na honest ndivyo unavyozidi kujiweka ktk mazingira ya kuwa slanderer zaidi ya valuable critic.

semantics my friend semantics; unachonicriticize mimi ndicho nawe unakifanya wewe mwenyewe. Ukiangalia mimi na wewe tuko kwenye kitu kile kile. Tofauti ni kuwa I want more kwa wale wanaotaka kutuongoza wawe madarakani sasa au wanaotaka kuja baadaye. Katika hili sina cha kucompromise. CDM au chama kingine chochote kinachotaka kuja kuwaongoza WAtanzania ni lazima kiwe kinastahili; na kustahili hakuja kwa sababu mtu anapendwa au chama kinapendwa. Isije kuwa watu wanafikiria CDM inastahili kushika hatamu za uongozi wa taifa kwa sababu watu wengi wanajiunga nacho wanashangiliwa sana na kuwa viongozi wake wanajenga 'hoja vizuri". Au kwamba kwa sababu watu wengi wanakipenda na kuwa tunaona maelfu ya watu wanajitokeza kuwasikiliza na kuwashangilia basi tusiwakosoe. Tukubali tu na kuwapa nafasi ya kustahili.

Sasa hili ni prerogative ya wengine. Mimi ya kwangu iko wazi sana na ukinisoma utanielewa. Ni kweli inaweza kuwa inawaconfuse wengine lakini kwa wale ambao wamenisoma kwa muda mrefu na kunifuatilia wataona hizi pande mbili ambazo ni za msingi sana. CCM haistahili kuachwa inatawala kwa sababu inapendwa - hata kama inaboronga; na CDM haistahili kupewa utawala kwa sababu inapendwa hata kama tunaona kuna mambo hayako sawa. Ni LAZIMA tujifunze kuwapitisha watawala wa sasa na wa baadaye kwenye tanuru la moto ili wastahili.
 
kwanini una crash ktk mazungumzo amabyo hayajawa hata hot?Sasa CDM wakikufuata wewe si watakuwa kituko sana ndugu yangu?Naomba jikaze na kutoa majibu na challenges za msingi na si kususa susa kama mkandara, huyu mkndara hadi yuko very volatile na sitegemei wewe kuwa hivyo.

Nimesusa tena? ooh no... nimesema tofauti zetu ni za msingi na zitabakia hivyo.
 
Thread hii imenikumbusha mbali sana.

Mwanakijiji, huyu WOWOWO ilitakiwa aanze kukuchimba kule kwa akina ME AGAINST KIKWETE, "SAM", TABASAMU.........akaja CONDOR aka HACK BCS....

Mapambano ya kisiasa ya mtandaoni yalianza zamani sana
 
Back
Top Bottom