Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Nimepitia link zote za Mwanakijiji na mabandiko ya wachangiaji, tofauti niliyoiona Mwanakijiji anajalibu kujenga hoja na kutoa ushauri kwa CDM bahati mbaya wafuasi wa CDM hawataki chama chao kukosolewa hilo ni tatizo kubwa watu wanaitaji kusikia na kusoma mapambio kutoka kwa Mwanakijiji, yeyote yule atakayebingana na CDM lazima aonekane mwenye kuitakia mabaya CDM.
 
MMM ni writer mzuri sana, ila bado tunabaki katika ukweli ule ule kuwa, saa ingine anaandika mawazo yake binafsi na yenye msingi wa kuelekewa anapo amini yeye, ingawaje mara nyingi anaandika katika ukweli zaidi. Mabadiliko hutokea katika hali zote, kimwili, kifikra, kimawazo na kimtazamo. Kila mtu hubadilika, leo hii CCM ikiwa imara na kuchukua hatua kali dhidi ya mafisadi (kitu ambacho kwa sasa ni sawa na ndoto za Alinacha) nahisi watu wengi sana hata akina Dr. Rweitama ambao ni CCM mfu watabadili mawazo. Leo hii CDM ikiwa kama CUF (nadiriki kusema hili) hakika tutabadili mawazo! Hakika kumbukeni msemo huu; "ONLY A FOOL CANNOT CHANGE HIS / HER MIND"
 
Nimepitia link zote za Mwanakijiji na mabandiko ya wachangiaji, tofauti niliyoiona Mwanakijiji anajalibu kujenga hoja na kutoa ushauri kwa CDM bahati mbaya wafuasi wa CDM hawataki chama chao kukosolewa hilo ni tatizo kubwa watu wanaitaji kusikia na kusoma mapambio kutoka kwa Mwanakijiji, yeyote yule atakayebingana na CDM lazima aonekane mwenye kuitakia mabaya CDM.

Ni kweli mkuu, na hapa ndipo hata mimi sometimes nakwazika na CDM kidogo, huwa hawakubali kushauriwa kwa urahisi, tena wanapokosea, siyo kila move ya CDM haina makosa, kubalini mabadiliko pia ya kushauriwa na kukosolewa, hayo ndo mabadiliko makubwa sana katika mapambano!
 
sidhani kama nimesema kuna umimi; CDM ndicho chama pekee sasa hivi kinachoweza kujipanga na kuchukua madaraka ya nchi. Kumbuka kina mtaji mkubwa sana wa mapenzi ya watu wengi. Wapo watu wengi ambao wamejitolea na wanaendelea kujitolea hali na mali kukijenga. Lakini hili peke yake la kupendwa halitoshi kufanya wawe wanastahili. Fikiria hapa ninachokisema vizuri.

Mzee Mwanakijiji, unasomeka kama hutaki kueleweka, umetuambia kuwa ulimkubali jk kwa kuwa alikuwa anakubalika miongoni mwa watanzania wengi isipokuwa mimi, nakugundua kuwa hukuwa unajua kwa makusudi kuwa huyo uliyemkubali alikuwa anapewa ridhaa kuongoza nchi kupitia genge lenye sura mbili, sura ya kwanza ya genge hili ccm imejifutika kiupole sana kwenye "ridhaa" ya wananchi kanakwamba inakubalika, na sura ya pili ipo kwenye mali,

inasomeka wazi kuwa tafsiri ya ccm, kupewa "ridhaa" ni kumilikishwa mali za tanzania, na afikiriye kinyume ni mkosefu anastahili kulipuliwa kwa bomu, Tukatae hili.

Imefaa kuwakubali cdm angalau kwa sasa kwa kuwa wanajipambanua na kutuhimiza kukataa kuonewa, kukataa kunyonywa na mnyonyaji yeyote, kukataa kudharauliwa na mtu yeyote, kukataa kupuuzwa na mpuuzi yeyote, kukataa kuibiwa na mwizi yeyote.

tuikate ccm kwa sababu inatuhimiza kuwapuuza wengine isipokuwa yenyewe inayotupuuza, ukitengeneza kanuni kuuhusu upuuzi, unakuta cdm ni wazuri kuzidi ya ccm kwani inatuhimiza kumkataa yeyote miongoni mwa wapuuzi, kwa sasa ccm ndiyo wapuuzi, na ikitokea cdm nao wakawa wapuuzi tuwakatae!

Tunahitaji kuwa wamoja zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya nchi yetu kwani adui yetu wa sasa yupo miongoni mwetu.
 
Last edited by a moderator:
Wakati kipindi kile bongo5 chat ipo juu mzee mwanakijiji alikuwa anaingia kule na kuleta mada tujadili.. habari chini ya kapeti zilikuwa mzee mwanakijiji ni usalama wa taifa anacheki upepo... Kipindi kile alikuwa Pro CCM haswa...
 
Kwa mimi fikra zangu zinanituma kuwaambia watu wa CHADEMA kuwa hawana wanachama wengi ila kuna lundo la watu wasioipenda CCM na kwa sasa wana moyo laini kuelekea CHADEMA ila wengi hawajafika chadema bado, kwa mwendo uliopo watu wengi wanaweza fika 2012 wakiwa stranded kimawazo and un decided.
 
Mwanakijiji nadhani umejieleza sana vizuri tena sana. Lakini niliwahi kukutaka upime zaidi mawazo yako kwa manufaa ya Taifa. Kama ukiweza kuondoa kabisa ubinafsi wako katika fikra na maono yako kisiasa kuhusu Tanzania, utaona kuwa mpaka sasa hakuna sababu yoyote kubakia CCM maana si chama kitakacho leta mabadiliko yoyote kwa raia wa Tanzania, bali kitalenga tu kuleta mabadiliko ya vitu na siasa. Sasa nilitaka upime je kuendelea kukikataa chama pekee kilichojitutumua hadi leo kumvalisha paka kengele unalisaidia Taifa kiasi gani?
Je ungetumia umahiri na uzoefu wa kisiasa kukishauri hiki chama au chama kingine chochote ili kiimarike zaidi na kuepesha huo utabiri wako wa mgawanyiko isingekuwa manufaa zaidi kwa Taifa lako? Kwanini unataka kuona vimeshaundwa na vimeshaimarika ndiyo uingie kwa mbwembwe na sifa? Au usifu? Wakati wapiganaji wanapambana wewe unakaa pembeni na kuwabeza? NAdhani inafaa ukae ujiulize zaidi. Hawa CDM kazi wanayoifanya siyo ya kubeza hata kidogo. Kama unabisha jaribu kufuatana nao uombe kuwa mgeni rasmi, ukaone wanavyokumbana navyo. Nadharia ni nyingi mno kupitiliza kwenye hii makala yako. Tafadhali acha kunywa chai ndiyo uandike makala, anza kuandika ndiyo unywe chai!
Nawasilisha!
Ujumbe mzuri sana. MMM pls fanyia kazi
 
uzee unanijia kwa kasi; naomba nipe post namba ya mahali hapo niliposema hivyo ili angalau nijikumbushe.

Kati ya nukuu zako kwenye hiyo thread ya Mh. Mbowe ni pamoja na hizi

"Upinzani in Tanzania is irrelevant, wala msiwalaumu ambao hawajajiunga kwa kutokufanikiwa kwenu! Kama ninyi ambao mko upinzani muda huu wote, wale wengine watakaoingia watabadilisha nini? Suala siyo wingi! je mawazo yao yatasikilizwa? Je kuna utaratibu wa kukubali kukosolewa na kubadilika? Nipeni mfano wa mwanachama wa kawaida aliyetoa mawazo ya mabadiliko akasikilizwa!

Na

"Give me a break! Mbowe kama anawajua hao awataje!!!! Mimi mwenyewe mbona viongozi wa ngazi za juu wa Chadema wamenifuata na kutaka nijiunge nao kwa ahadi za vyeo?!! Check link hii.

https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/947-the-only-thing-we-have-to-fear-10.html #post13325
 
ndio inaweza kushinda lakini ishinde ili kiwe nini? siyo ishinde ili CCM iondolewe madarakani

Of course - CDM ishinde ili CCM iondoke madarakani -- yaani iwapishe CDM, au? Yaani unataka kusema CDM ikishinda uchaguzi CCM haitatakiwa kuondoka madarakani?

Labda sijakuelewa mkuu. Ingefaa sasa utueleze maana hasa ya siasa za demokrasia za ushindani (competitive democratic politics) - yaani lengo ni nini. Siyo kwamba chama kikishinda uchaguzi ndiyo kinatwaa madaraka ya nchi?

Katika uchaguzi ujao nchini Uingereza, Labour ikishinda, jee Conservative haitakiwi kuachia serikali?

Please explain maana ya cometitive politics bila kuzungusha.
 
Of course - CDM ishinde ili CCM iondoke madarakani -- yaani iwapishe CDM, au? Yaani unataka kusema CDM ikishinda uchaguzi CCM haitatakiwa kuondoka madarakani?

Labda sijakuelewa mkuu. Ingefaa sasa utueleze maana hasa ya siasa za demokrasia za ushindani (competitive democratic politics) - yaani lengo ni nini. Siyo kwamba chama kikishinda uchaguzi ndiyo kinatwaa madaraka ya nchi?

Katika uchaguzi ujao nchini Uingereza, Labour ikishinda, jee Conservative haitakiwi kuachia serikali?

Please explain maana ya cometitive politics bila kuzungusha.
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Actually muda huo nilikuwa mdogo kiumri (I mean kuweza kupiga kura) lakini nilikuwa nikiifuatilia Jambo Forums by then. Ni kama naona Mzee Mwanakijiji si yule niliyekuwa namsoma enzi hizo hasa ikizingatiwa kwenye thread hiyo alitoa madai mazito ya viongozi wa CDM kutaka kumuahidi vyeo ili ajiunga na chama. Sijui nini kilitokea MMM akabadilika.

Haya ndio baadhi ya makosa ambayo watu wengi huwa wanafanya, hivi kwa sababu tu MMM anaongea saaaana ndio aitiwe uongozi?
 
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.

Acha tabia ya kupindisha pindisha maneno, kama umekosea kubali yaishe, Hayo majukumu unayotaka kuyafanya ndio key kwa CHADEMA hayana tofauti na kuifanya CHADEMA kuwa NGO, Sababu ya kwanza kabisa ya uwapo wa CHAMA CHA SIASA NI KUKAMATA DOLA.
 
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.

Simply put we need a change of power so that someone can do what CCM has failed over the years despite the fact that they could not have failed anyway had they wanted to do exactly what they are supposed to do. Serve the people! Instead they are serving a few who are supporting them to be in power.
 
Umenikumbusha mbali sana, ndio mchakato wenyewe wa mabadiliko huo. Hakuna kisichobadilika isipokuwa mabadiliko

Mkuu hata "mabadiliko yanabadirika" ndiyo maana yanaitwa mabadiliko. Ni kwa sababu maisha ni dynamic siyo static kwa hiyo mabadiliko ni lazima pamoja na "mabadiliko kubadilika".

Kwa Mzee Mwanakijiji hakugeuka nyuma akawa jiwe bali ameitika wito wa mabadiliko na anasonga mbele.

Nampongeza kwa uhuru wa fikra unaozaa mabadiliko.
 
Basi mngepeana number za simu mtextiane meseji badala ya kutuwekea hapa.

Mkuu Sangara heshima mbele. Lengo langu lilikuwa ni kuweka kumbukumbu sahihi humu jamvini. Maana nilihisi anachokisimamia MMM sasa ni tofauti na alichokuwa anakisimamia mwaka 2006 kwenye thread hiyo ya Mh.Mbowe. Sasa nimejua anasimamia nini. Sasa in between the line kama kuna issue zimeibuka bila shaka Mzee Mwanakijiji hana budi kujibu. Nadhani ndiyo maana ya forum na ni sehemu ileile ya kukeep record sahihi.
 
Back
Top Bottom