Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Unajua kuna watu wanajua kuongea, kupangilia maneno na ustaa. Mwanakijiji nilishamwonaga ni mjanja tu wa mjini.
Kama mnabisha atuweke hapa cv yake. Ni mtu wa kuropokaropoka maneno marefu yasiyo na mwisho, lacks coherence,solid point and too vague.
Kwahiyo sipotezi kumsoma hata siku moja. Wajinga mlio chinibhake ndio mnapoteza muda.
 
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 niliamini kuwa Tanzania inahitaji mabadliko makubwa ya kiuongozi. Niliamini kabisa kuwa kiongozi atakayekuja atatakiwa kuwa mtu mwenye kukubaliwa na wananchi na ambaye atatumia kukubaliwa huko kuanzisha program ya haraka ya mabadiliko ili kuchochea maendeleo Tanzania. Sikumuona kiongozi huyo katika upinzani. Nilikuwa sahihi.
Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana. Wakati ule niliandika makala kadhaa kwenye mitandao ambazo zilielezea jukumu hili. Katika makala moja nilielezea kuwa Kikwete anaingia katika uongozi wa taifa letu wakati wananchi wanahitaji kiongozi atakayewaamsha kujiletea maendeleo. Nilisema ni mzigo tuliomtwisha Kikwete. Na nikatoa angalizo wakati ule endapo Kikwete atashindwa kukidhi matamanio ya Watanzania hakuna tena mwanasiasa mwingine yeyote ndani ya CCM atakayeweza kufanya hivyo kwa siku za karibuni.
Ushindi wake wa asilimia 80 ya wapiga kura ulikuwa ni ushindi wenye kurindima. Uliacha mwangwi wa kila nchi. Tuliomuunga mkono tuliamini kuwa atasimama na kuliongoza taifa letu vizuri zaidi akitumia mandate aliyokuwa ameipata. Furaha za Kikwete kuingia madarakani hazikudumu. Kikwete hakuitikia wito wa historia na badala yake alianza kuonesha udhaifu ambao wale waliokuwa wanamjua kabla walikuwa wanautambua; hakuwa kiongozi mwenye kuhamasisha (inspire) wananchi wake. Akaanza kufanya mambo ambayo mara moja mimi binafsi nilitambua ni alama za kiongozi dhaifu.
Hiki ndicho kilichotokea; ni kutambua kuwa CCM haiwezi kuleta mabadiliko tunayoyataka ; ni kutambua kuwa mabadiliko tunayoyataka yanatakiwa yaongozwe na fikra maridhawa ambazo zinaweza kugusa wananchi na wakazielewa. Siyo uzuri wa watu, na utamu wa majina yao bali uzuri na ukweli wa hoja zao.
Ni muumini wa fikra na si mfuasi wa watu
Sasa mtu anaweza kufikiria kuwa mimi nilikuwa mfuasi wa Kikwete; hapana. Mimi ni mfuasi wa fikra na kwa wanaonijua wanafahamu kuwa ni muumini wa fikra sahihi za Mwalimu Nyerere. Fikra hizi ambazo nimejifunza kwa kina na ninaendelea kujifunza siku kwa siku ninaamini ni sehemu ya alama za taifa letu. Baada ya Kikwete kushindwa kuonesha uongozi wa taifa letu na kutuhamasisha kujenga jamii ya kisasa niliamua wakati ule kuanzisha harakati za mapambano ya kifikra; yaani wananchi wetu ili waweze kubadilisha kura ni lazima kwanza wabadilishe fikra!
Ninaamini kimsingi mambo yafuatayo ambayo nimetokeo ya kujifunza Fikra za Mwalimu Nyerere:
a. Usawa wa watu wote unaotokana na usawa wa utu: Nimewahi kuliandika hili baadaye kuwa Nyerere aliona usawa siyo ule wa kisheria kutokana na wote kuwa "sawa mbele ya sheria" kama ilivyo Marekani bali ni usawa ambao unatokana na wote kuwa ‘sawa sababu ya utu wao'. Kwamba hakuna binadamu mwenye utu zaidi ya mwingine
b. Uongozi ni utumishi siyo ulazimishi: Ninaamini kuwa mtu anayetaka kuwa kiongozi anapaswa kuwa mtu anayetaka kutumika siyo kutumiwa au kutumikisha wengine.
c. Maendeleo ni ya watu siyo vitu: Mojawapo ya mambo makubwa kabisa niliyojifunza kutokana na fikra za Mwalimu ni dhana kuwa maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu ni udikteta wa vitu. Watu ndio msingi, kiini, sababu, lengo na njia ya maendeleo. Utawala wa CCM (hasa kuanzia Mkapa) umeweka mkazo mkubwa sana kwenye kuendeleza vitu; wanajivunia vitu, wanatuonesha vitu. Siyo watu walioendelea!
d. Siasa ni chombo tu cha kuchochea mabadiliko. Binafsi nachukulia siasa kama chombo cha kusaidia kuleta mabadiliko. Ninaamini siasa ikitumiwa vizuri kama kisu inaweza kutumika kumchuna ng'ombe vizuri, kukata majani, na hata kuchimba ardhini ili kuleta tunachotaka. Ikitumiwa vibaya inakuwa kama jambia mikononi mwa kichaa! Ina madhara. Hivyo ni muumini wa "siasa bora" na siyo "bora siasa".
e. Wenye kushika madaraka wanashika kama dhamana si haki. Mojawapo ya mambo muhimu yanayoniongoza ni kuwa sina heshima ya kutukuza mtu mwenye madaraka kwa sababu anapigiwa saluti au anaitwa mheshimiwa. Wote kwangu hawa ni watu waliopewa dhamana na dhamana yenyewe ni ile inayotokana na wananchi. Sijali sana nani anashika cheo gani; ninachojali ni nini anafanya mwenye cheo hicho kutumikia wananchi.
f. Raslimali za Tanzania ni kwa ajili ya kunufaisha Watanzania. Msingi huu kwangu ni msingi mkubwa wa mawazo yangu juu ya uchumi. Siamini kabisa kuwa raslimali zetu ni kwa ajili ya kunufaisha mataifa ya kigeni.
g. Viongozi ni lazima wawajibike kwa wananchi na wasipowajibika wawajibishwe na wasipowajibishwa wabishiwe! Sipendi kabisa watu wanaokubali kauli za viongozi au watu wenye madaraka kwa sababu wanawaheshimu.
Sasa kutokana na hizo hapo juu (nyingine nimeziweka pembeni) nilijikuta nabadili mawazo. Nirudi kwenye hoja iliyotolewa kuhusu ile insha ya Mbowe na kwanini sikuamini kuwa ameonesha uongozi (na bado naamini niko sahihi).
Ikumbukwe kuwa makala ya Mbowe iliandikwa mwishoni mwa mwaka 2009 (Disemba 2). Lakini kabla ya kuandika makala yake hiyo ni vizuri kujiuliza nini kilikuwa kinatokea nchini na kwa kiasi gani kilishabadilisha mwelekeo wangu wa kumuona Kikwete kama sehemu ya suluhisho la matatizo yetu na kuwa yeye na chama chake ni sehemu yatatizo.
Nilianzisha mada yenye kujadili bajeti ya kwanza ya Kikwete (ile ya 2006/2007). Hii ndiyo ilikuwa bajeti ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Nilisema hivi wakati ule kuhusiana na hilo "Ni kutokana na utekelezaji wa bajeti hii ndo tunaweza kwa haki kuanza kumhukumu Kikwete na watendaji wake." Nilihitimisha kuwa ilikuwa ni "bajeti ya kiinimacho".
Lakini kitu kingine ambacho kilitokea na ambacho kiliniaminisha kuwa Kikwete na CCM ni tatizo ni mwitikio wa serikali ya Kikwete na Bunge la CCM juu ya filamu ya "Darwin's Nightmare". Nilishangazwa na mwitikio huo na hasa kitendo cha Kikwete kukanusha kuwa watu wetu hawali mapanki (makayabo) na vile vile kukataa kuwa silaha zilikuwa hazisafirishwi katika ardhi yetu kama ile filamu ilivyodokeza. Hili lilinishangaza. Na nilishangaa zaidi pale Bunge lililokuwa kwenye kikao cha bajeti lilipotoa kauli ya kumuunga mkono Kikwete.
Kwa wanaokumbuka ndio ripoti ile ya "Tanzania's Role in Arms trafficking" nilipoandika ikikusanya taarifa mbalimbali. Mpaka mkubwa ulizidi kati yangu na watawala na kwa kiasi fulani na watu ambao mwanzoni tuliwahi kuwa marafiki (japo si wakaribu).
Niliewa tatizo ni zaidi ya mtu mmoja ni chama chenyewe!
Novemba ya mwaka ule (mwezi mmoja kabla ya makala ya Mbowe) niliandika ile makala ya "The arrogance of power). Nilielezea mle ni kwanini tunasumbuka sana na hiki kiburi cha wenye madaraka.
Sasa tukio jingine ambalo siwezi kulisahau ni tukio la Mauaji ya wale wafanyabiashara wa vito vya thamani katika ile kesi maarufu ya Zomba. Wakati ule nilielewa kwa undani zaidi pia jeshi la polisi ni tatizo kubwa zaidi na nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutaka IGP Mahita aondolewe na ndio nilitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.
Sasa hadi wakati ule nilikuwa nalenga katika kuamsha watu ndani ya watawala kuanza mabadiliko ya kuongoza vizuri. Mwaka 2006 ulipoisha kitu kimoja kilikuwa dhahiri; viiongozi wabovu hawageuki kuwa wazuri wakishika madaraka bali wanathibitisha ubovu wao zaidi. Na hili ni kwa sababu wakati ule sakata la Richmond lilikuwa limeiva na tukaona mwitikio wa serikali. Mwaka 2007 ulipokuja nilikuwa nimeshaweka mawazo yangu sawa zaidi kuwa kanuni ninazozipigania haziwezekani tena chini ya CCM! Kumbuka sikubadilika msimamo wangu au fikra zangu; nilibadilika ni wapi naweza kuona fikra hizo zinatekelezeka zaidi!
Mapema mwaka 2007 ilipatikana picha ambayo wengi labda mnaikumbuka. Ilikuwa ni katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ambapo viongozi waliokuwa jukwaani walionekana wamechoka na kusinzia akibakia Seif Sharrif tu akiwa macho. Niliandika mada wakati ule na kuiita "Taifa la viongozi waliolala".
Lakini ni ile makala ya "Kuanguka kwa CCM Unabii utatimia" ndiyo ambayo labda iligusa fikra za watu wengi zaidi. Ni makala ambayo ilikuja mapema 2007 (Januari 20). Kwa yeyote anayeweza kusoma anajua kabisa kuwa ni wazi kuwa makala yangu ilikuwa inautenganisha moyo wangu toka CCM kuufanya ukubaliane na fikra zangu. Nilikulia ndani ya CCM, nimekuwa Chipukizi na kushiriki hata mbio za mwenge. Kwa hiyo hisia zangu zimechukua muda kukubaliana na kile ambacho nilikuwa nakiona kiakili. Labda niseme akili yangu ilishaikataa CCM mapema zaidi kabla ya hisia zangu kufanya hivyo.
Mojawapo ya makala zangu ambazo labda wengi hawakuisoma ni ile ya Pongezi ya Miaka 30 ya CCM. Hii ilikuwa ni Februari 2007. Makala ile ilichora kwa upande wangu mpaka wa kifikra (ikumbukwe ni baada ya kauli yangu kuwa moyo bado ulikuwa CCM). Katika makala ile nilisema hivi "Hata hivyo kama nilivyosema, ni bora uungane nami kutoa pongezi hizo sasa na leo kwani kuanzia wiki ijayo, miaka mingine thelathini inaanza, miaka ambayo itakuwa ni tofauti. Anayedhania kuwa miaka thelathini ijayo itakuwa ni ya hadaa na utawala wa CCM mtu huyo hajui kusoma ishara za nyakati."
Nilihitimisha kwa maneno haya "miaka thelathini iliyopita tunasema hongera CCM, kwani si kidogo, lakini inatosha"! Mstari ulikuwa umekamilika.
Sikurukia behewa la chama kingine
Kinyume na watu wengine ambao wanatoka huku na kuingia kule mimi niliendelea na nimeendelea kubakia kuwa huru kifikra. Kanuni zangu zikibaki pale pale lakini nikitamani sana kuona chombo kipya chenye kuweza kubeba matumaini ya Watanzania kinatokea. Sikuwa muumini wa CDM ilivyokuwa wakati ule na sikuamini kwa muda mrefu kama inaweza kutuongoza kuelekea matumaini. Hata sasa hofu yangu hii bado ipo na inanisumbua sana.
Baada ya kuibuka kwa ile ripoti ya Mafia wa Tanzania niliweza kuona matumaini; niliandika makala ile ya "Twawapa Notisi watawala wetu". Ikumbukwe kuwa ni mimi ndiye niliyebadilisha kauli ya "viongozi wetu" na kuwa "watawala wetu". Leo hii wananchi wetu wengi (wanasiasa na wasio wanasiasa) wanajua tofauti ya haya mawili.
Mwezi wa tano mwaka 2007 niliandika makala ya "Je wapinzani watatuongoza". Makala hii iliangalia wakati ule kama kuna tumaini katika upinzani. Na shauri watu wasome makala hiyo kuweza kuangalia nilichokuwa ninakisema wakati ule wakati tunaangalia ujio wa uchaguzi wa 2010.
Kuelekea uchaguzi wa 2010
Kuelekea uchaguzi wa 2010 nilikuwa nimeshaamua kuwa upinzani unahitaji kupewa nafasi; lakini siyo kupewa nafasi kama hisani bali kustahili nafasi. Niliandika ile makala ya "CHADEMA kutoka hapa mpaka kule" na wiki chache kabla ya uchaguzi niliandika ile makala ya "Pembetatu ya Ushindi". Makala hizi mbili zilikuwa na lengo la kukichochea CDM kuweza kuonesha kweli kinataka kushika hatamu za uongozi wa taifa hili.
Bahati mbaya sana uongozi wa CDM haukuwa na lengo hasa la kushika hatamu za uongozi wa taifa wakati ule. Hawakujipanga kushika utawala na hili kwa kweli lilisikitisha sana kwa sababu kama ilivyo leo hii bado wanafikiria kwa msingi wa "mimi nipate"! Matokeo yake leo CDM kiko katika hali iliyokuwepo 2007! Kikipendwa zaidi, kikikubalika zaidi lakini kikifanya sifuri kujipanga kushika madaraka!
Mojawapo ya swali kubwa zaidi ambalo yapaswa kujibiwa ni ilikuwaje nilikuwa naiunga mkono CCJ? Kwanza ni kwa sababu za ukweli kwamba nilishakata tamaa na CDM na niliamini kuwa ili CDM iamke inahitaji chama kingine cha upinzani ambacho kingeiwashia moto nyuma. CCJ kilikuwa ni chama ambacho endapo kingepata usajili wa kudumu kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 basi mazingira ya kisiasa yangebadilika sana. Lakini kitu kingine ambacho wengi walikuwa hawakijui ni kuwa katika vita kuna mbinu; kwangu CCJ ilikuwa ni diversion tactic ya kunipa uhuru kufanya kitu kikubwa zaidi ya kuisadia CDM ishinde. Na nilifanikiwa sana kwani wakati watu wanahangaika na mimi na CCJ, CDM ilikuwa inapangwa kufanya vizuri zaidi!
Nimebadilika?
Ningeweza kuandika kwa kirefu sana juu ya hili lakini sijioni kama nimebadilika. Vile ninavyovisimamia bado ni vile vile na imani yangu kuhusu uwezekano wa kujenga taifa la kisasa bado ipo pale pale. Kilichobadilika zaidi ni kuwa ninaelewa zaidi kuwa wanasiasa wanataka mabadaraka zaidi kwa ajili ya madaraka. Ni kama Kikwete alivyoutaka Urais kwa ajili ya Urais. Mbowe bado hajaonesha uongozi na kipimo cha kushindwa kwake kilionekana 2010; viongozi wengine ndani ya CDM nao wanapata shida ya kuonesha uongozi na badala yake kuelekea 2015 CDM inaweza kwenda ikiwa imegawanyika kuliko CCM!
Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015. Badala yake mwaka huu tumeshuhudia malumbano ya ajabu sana na visa vya ajabu vikitokea. Utagundua kuwa sijawahi kwa mwaka huu kutoa maoni yangu kuhusu hili kabisa na labda nitalitolea maoni lakini naendelea kukata tamaa na inakatisha tamaa! Nilisema wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ningekuwa na uwezo ningewatia bakora viongozi wa CDM na nilimaanisha! Na nilisema wangepoteza Arumeru Mashariki Mbowe na uongozi wote wa juu wangetakiwa kujiuzulu; na hata sasa labda kesi inaweza kujengwa ya kwanini wajiuzulu mapema zaidi (bado sijamaliza kuijenga hii hoja, inshallah).
Inawezekana nimebadilika; lakini mwenyewe sijioni hivyo.
Mkuu huwa nakurespect sana na wewe ni mmojawapo wa walionifanya nikavutiwa kujiunga na JF,lakini mkuu niseme ukweli,umeamuwa wazi kabisa kuionea chadema na kutumia siasa kuukandamiza upinzani na kuzififisha ndoto ama matumaini ya watanzania kuhusiana na mabadiliko ya nchi yao.

Mkuu wangu nilishakwambia before kuwa kitu una lack,ni empathy,na hilo linapelekea wewe kuonekana kamavile uko out of touch.Unazungumza kama elite bana?!lol!

Nimepitia hizo links za makala yako,lakini nilichoona ni kile kile,uonevu wa hali ya juu kwa chama cha chadema ambacho wanajitahidi kukijenga kila uchao kuanzia huko vijijini na mijini pia.

Nakubali una busara lakini wewe si mpinzani wa kweli(hopefully i'm wrong),kwasababu ninaamini kwenye mambo haya unahitaji kuwa resolute, kuwa na msimamo dhabiti kabisa.Kuwa na nia na dhamira na msimamo usioyumba kwamba sasa imetosha na ccm should go!

Na kwahiyo kuna walioweka matumaini kwako,mimi ninasema na alaaniwe mwanadamu yeyote amtegemeaye mwanadamu mwenzake.

Kwasababu ndiyo maana tunaona inatokea one individual akihatarisha uhai wa chama na future yake,mfano wa ndugu Zitto.Watu waliweka imani kubwa kwake bila kujuwa na yeye ana mipango yake binafsi haswa ya kupata madaraka makubwa zaidi bila ya kujali anachokikanyaga kwenda huko juu ama hata ikitokea kwamba upinzani haushindi.

Kitendo cha kusema uliiunga mkono ccj ili kuweza kuisaidia chadema ni sawa na uongo mkubwa kabisa!Kwasababu si kweli kwamba chadema ingekuwa imesadiwa na uwepo wa ccj.Chama kile kilikuja kwa nia na madhumuni ya kuzigawa kura za wananchi.Hata kama hilo halikuwa lengo,lakini si kweli kwamba uwepo wake ungeinufaisha chadema.

Kwenye hizo linki ulizoziweka,kuna moja ina kauli ama maswali yanauliza kama wapinzani wakipewa nchi basi kila kitu kitakuwa sawa right away!Hivi hilo ni swali gani mkuu?Ndiyo shida tuliyonayo sisi watanzania na waafrika kwa ujumla,ya kutaka kuona matokeo ya kile tunachokifanya right away,na ndiyo maana huwa hatufukirii kuhusu the next generation!

Tofauti na wezetu ambao hata maendeleo waliyoyapata,ni kwasababu kuna waliofanya kazi kwa bidii kwenye uvumbuzi na mambo megine huku wakijuwa kabisa kuwa matokeo yake hawatayaona on their life time!

Ndiyo maana sayansi iko juu kwa wenzetu,teknolojia,maendeleo ya watu wake kimaisha nk,ni pale wengine walipofanya yale wanayoyaona yanafaa bila hata kujali kama matokeo ama rewards zitaonekana right away or in their life time.So sisi ni wabinafsi sana,na ndiyo maana unauliza maswali ya aina hiyo!Kupanda mbegu ya uwajibikaji kwa kuwawajibisha watawala pale tunapowaondoa madarakani,inawezekana kabisa kwamba tunaweza tusione hayo mabadiliko right away,lakini manufaa yatakuwepo vizazi na vizazi.Mifano ni mingi tu especially kwenye nchi za wenzetu.

Kwa mfano kipengele hicho hapo chini, "chini ya ahadi:wapinzani watatuongoza?",hapo ndipo ulipoonyesha wazi uonevu wako kwa chadema!
Je, Watanzania hawa walioko upinzani wakipewa madaraka ya nchi leo hii (si kupewa kama hisani bali kutwaa kwa kutumia sanduku la kura), matatizo ya Tanzania yatatoweka ghafla?
Je, ndugu zetu hawa wakishikilia Bunge na Ikulu hospitali zetu zote zitakuwa za kisasa, wanafunzi wote watakwenda shule, mishahara italipwa kwa wakati, mikataba haitakuwa na utata na mahekalu ya viongozi yataacha kujengwa?
Je, wananchi hawa wakitwaa madaraka ina maana umaskini wa Tanzania utatoweka ndani ya miaka mitano? Je, Watanzania hawa walioko katika vyama vya upinzani ndiyo wakombozi wa taifa letu tunaowangojea kama wana wa Waisraeli walivyongojea ukombozi kutoka Misri, ili warudishwe kwenye ile nchi ya ahadi, nchi imiminikayo maziwa na asali?
Ni bora ungesema kwamba sera na ilani za chadema,hazionyeshi kwamba watatufikisha huko,kwasababu kiukweli,hatuwezi kujuwa hadi hapo watakapochukuwa madaraka,unless wewe unaona kwamba matatizo yao ni ya kiuongozi,jambo ambalo unapiga danadana tu na hujalielezea na kuwa mkweli kwa kutoa ushauri wa nini kifanyike(endapo ni uongozi).Nina amini una mtizamo mbaya kuhusu viongozi na ndiyo maana unaona kama vile wanachosema siyo kile ambacho watakifanya endapo watapata ridhaa ya wananchi ya kuwaongoza.

Kwamfano kwenye kipengele hicho hapo chini kutoka kwenye makala hiyohiyo,ambapo kwa mbaali naona kama vile ulimaamisha kuwa ndugu Zitto alionewa,pengine ni kutokana na lile la kushauriwa asigombee uenyekiti.Hapo kuna wengi wenye kufanana na mawazo yako.

Lakini je unafahamu kuwa utofauti wao umesababishwa haswa na kitu gani?Ama na wewe pia una imani ni kutokana na ukabila na udini kama ambavyo washabiki na wapenzi wa ndugu Zitto wamekuwa wakisisitizia?

Pia hata misimamo ya ndugu Zitto ya kutokuona umuhimu wa m4c,maandamano na mengineyo kama kuhangaikia katiba kwenye kipengele cha umri,ndiyo kusema amefuata ushauri wako?Je kuonyesha uongozi bora hakuwezi kuenda sambamba na hayo unayosema wanang'ng'ania?
Si kwa kuandaa maandamano, kulalamika au kung'ang'ania katiba mpya kuandikwa (hayo yote yaweza kufaa wakati muafaka), bali kwa kuonyesha uongozi bora katika vyama vyao na katika maeneo wanayoyaongoza, kuwa wa wazi kwa matumizi ya fedha za vyama vyao, kuonyesha kuwa madaraka ndani ya vyama hivyo hayatokani na kitu kingine chochote isipokuwa taratibu za wazi za chama na hayatumiwi vibaya.

Kwenye makala yako ya "chadema kuanzia hapa mpaka kule",umetoa ushauri mzuri tu,lakini pia umeonekana kijichanganya sana tu,unasema chadema wasijikite kuwa wapinzani,yani wasitake tu kuwa wapinzani wengi bungeni,bali wawe watawala(kumbuka umeshasema ulitoa mfano wa utofauti kati ya watawala na viongozi).

Na kwenye hiyo makala yako,umesema "kutawala siyo lelemama",na ukasema kuwa chadema inatakiwa iwe na wabunge wengi zaidi ili ikiwezekana wapate kumchaguwa waziri mkuu.Sasa watapata vipi wabunge wengi kama wasipojipanga kupata hao wabunge?Watapata vipi idadi ya kumchaguwa waziri mkuu kama wasipotaka kuwa na wapinzani wengi bungeni?Ama watadondoshewa wabunge kutoka mbinguni kama mikate ya mana?

Kipengele hicho hapo chini kinaonyesha hayo...
Kinyume na wale wanaoamini ni muhimu kuongeza idadi ya wabunge ili "kuimarisha ubunge upinzani" mimi ninaamini kama Chadema inataka kuwa na wabunge wengi siyo kwa ajili ya kuongeza 'upinzani Bungeni' bali ni kwa ajili ya kuweza kushika nafasi mbili muhimu sana. Uwaziri Mkuu na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ukweli ni kwamba kuongeza idadi ya wabunge,siyo tu kwamba kutaimarisha bunge pinzani,bali kutatoa huo uwezekano wa hoja yako ya kuweza kumpata waziri mkuu.

Pia the fact kwamba unadoubt chadema kama itafanya mabadiliko,bado kwenye makala hii uliwasisitizia kuwa waachane na fikra za kuwa wapinzani,yani hao hao unaowadoubt kama watakuwa viongozi bora,ndiyo hao hao unawaambia waache kufikiri kama upinzani,what a double standard!

Sidhani kama unafanya makusudi,i hope that is not the case.Kwasababu wewe ni hazina ambayo wanasiasa wanaweza wakaitumia vyema kama wakitaka na kukushirikisha.

Kwenye kuhusu ushauri wako wa muundo wa chadema kufanana na ccm,kwa kweli niweke wazi kabisa kuwa nimekubaliana na wewe especially kwenye issue ya utitiri wa vikao.Licha ya kwamba imani yangu inanituma kwamba,chadema walifanya uamuzi huo ili waweze kudili na serikali ya ccm vyema.However ninakubaliana na wewe,kwa mfano kwenye mpira wa miguu,timu zinaweza zikatumia formation za tofauti,maybe moja ikatumia 4-4-2. na nyingine ikatumia 3-5-2,kila timu ikiwa na malengo yake(eventually ushindi),lakini kwa uhakika,kila mchezaji atapata mchezaji mwenzake wa kumkaba mbali na kwamba timu moja itakuwa imeweka wachezaji wengi kwenye sehemu ya kiungo ama katikati ya uwanja.
Ndiyo hapa tunarudi kwenye hoja ya kwanza kwamba ni muhimu kwa Chadema kuachana na fikra na siasa za kuwa mpinzani na badala yake kuwa chama kinachotaka kushika madaraka ya nchi na madaraka ya nchi yamegawanyika katika nafasi mbalimbali zenye kuweza kusababisha mabadiliko tunayoyataka.
Kwenye makala yako hiyo,pia umezungumzia kuwa chadema hawakuwa wapinga ufisadi hadi pale walipopata zile nyaraka ambazo kwa mara ya kwanza zilitolewa hapa JF,na ukaweka mfano wa jinsi Dr Slaa aliposema kule bungeni kuhusiana na nyaraka zile.

Ukweli ni kwamba ninafahamu fika kabisa kuwa viongozi wa chadema walikuwa wakipinga ufisadi(nilishawahi kuhudhuria mikutano yao nikiwa mdogo),sema tu alitokea whistle blower ndani ya system aliyeweka mambo hayo wazi,sasa je unataka tuwakatishe tamaa watu wa aina hiyo kwa kutoonyesha kwamba tunataka mabadiliko ya kweli?

Wakiona whistle blowing yao haijaleta mabadiliko,je next time watakuwa na incentive gani?(sikubaliani nao kwasababu bado watakuwa wabinafsi kwa kutaka kuona matokeo right away),lakini ndo ukweli wetu watanzania...

Ni sawa tu na watu wanaomkatisha tamaa Uliomboka humu,hata kama next time kuna ambaye atataka kupingana na uonevu wa serikali kwa manufaa ya umma,je atafanya hivyo?je hatakuwa discouraged?

Ni huku kuyumba kwetu kama mbayu wayu na kukosa msimamo ndiko kutatucost!

Hivi kama tuliweza kuyajuwa yale kwasababu tu ya mtu wa ndani aliyetoa siri,je hujui kwamba inawezekana kabisa hayo mambo bado yanaendelea maybe kwa kasi ile ile?

Tutajuwa vipi na ni mambo ya siri ambayo kujulikana kwake ni hadi mtu wa ndani atoe siri hizo?Labda hapa ushauri ungekuwa kwa chadema kwamba wakiingia madarakani,basi wahakikishe wanayapitia yote hayo na kuyafichua na kuwawajibisha viongozi waliotumia madaraka yao vibaya, na kuuangamiza uchumi wetu, na kusababisha umasikini uliokithiri huku viongozi ndiyo wakiwa wamejinufaisha kwa kuhujumu uchumi.

Ungekuwa na empathy na kutambuwa ni kwa jinsi gani maisha ya watanzania walio wengi ni ya shida kwasababu ya ccm,basi wala usingejiuliza maswali mara mbili mbili kuhusu kuiondoa madarakani,kwasababu madhara yao toka uhuru ni makubwa mno!

Na nchi zote ulizozitaja ie Malawi,Zambia na Kenya kwamba wameweka wapinzani na hawana maendeleo,bado ni kama unai underestimate potential ya taifa letu!Hakuna nchi hata moja kati ya hizo yenye utajiri tulio nao,na hakuna itakayosimama na sisi kama tukipata uongozi kutoka kwa wananchi na kwaajili ya wananchi.

Na pia mabadiliko ya kwao si lazima yafanane na ya kwetu,pia mabadiliko hayaji kwa siku mbili ama hata miaka miwili au mitano.

Imeichukuwa ccm miaka 50 kutuingiza kwenye hili shimo la ufukara,ujinga na maradhi,lakini na wewe unataka miaka 5(ya chadema), ili tuondoke kwenye shimo la miaka 50?Si uonevu huo mkuu?

Cha msingi hapa, ni kuweka ushindani utakaoondoa kujisahau kwa viongozi wetu kwamba wanastahili kututawala no matter what.Kwamba they can do whatever they want kwasababu kuna kina Mwanakijiji wasiokuwa na imani na wapinzani.

Sitaki kuifanya posti hii kuwa ndefu sana kwasababu kwanza sikutaka kuliquote bandiko lako lote.Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna wanaotumia simu haya.Hivyo basi wakati ninaendelea kuzisoma makala zako nyingine,pia naendelea kutafakari.

Hiyo ni ili niweze kupata context haswa ya kwanini kuna wanaosema umebadilika,ama kuona kama kweli hauionei chadema. kama ninavyodhani.
 
MMK ni Gifted writer,ila sijajua kwanini anawa accuse vingozi wa CDM kwa umimi?Ingawa atakuwa na wakati mgumu kutetea kuwa huo umimi kuwa upo na upo kwa akina nani ktk chama.Ila pia atakuwa na wakati mgumu kutuambia (akina tomaso sisi)kama vyama vyote vina umimi kwanini aone umimi wa CDM kuliko mwingine?

sidhani kama nimesema kuna umimi; CDM ndicho chama pekee sasa hivi kinachoweza kujipanga na kuchukua madaraka ya nchi. Kumbuka kina mtaji mkubwa sana wa mapenzi ya watu wengi. Wapo watu wengi ambao wamejitolea na wanaendelea kujitolea hali na mali kukijenga. Lakini hili peke yake la kupendwa halitoshi kufanya wawe wanastahili. Fikiria hapa ninachokisema vizuri.
 
Mkuu huwa nakurespect sana na wewe ni mmojawapo wa walionifanya nikavutiwa kujiunga na JF,lakini mkuu niseme ukweli,umeamuwa wazi kabisa kuionea chadema na kutumia siasa kuukandamiza upinzani na kuzififisha ndoto ama matumaini ya watanzania kuhusiana na mabadiliko ya nchi yao.

Unajua ni kina nani waliandika ilani ya uchaguzi ya CDM ya 2010? Well, I was one of them. Kusema kuwa hata natumia siasa kufifisha ndoto ama matumaini ya Watanzania kuhusiana na mabadiliko kunaonesha ni kuwa hujafuatilia yale ambayo nimeyasimamia na kuyapigania tangu harakati hizi zianze. Bahati nzuri kama ni ufisadi wa serikali mimi mwenyewe nimeshiriki sana kuufichua; kama ni kuongoza mabadiliko kwa kadiri nilivyoweza nimefanya hivyo. Na kwa vile ulikuwepo muda mrefu hapa ama hutaki kukumbuka au katika kumbukumbu hiyo hutaki kuona.
 
Ukweli ni kuwa MM bado haeleweki, ni kama uwa anabadilika badilika kila mara. Kuna wakati uwa anakuwa mpinzania mzuri wa CCM na serikali yake, ila kuna siku uwa anakuwa mkali dhidi ya upinzani na hasa CDM. Na nadhani bado anashaka dhidi ya uongozi wa CDM, maana kuna kipindi wakati wa uchaguzi wa CDM kule Arumeru Mashariki alisema kuwa kama CDM wakishindwa basi uongozi wa CDM uachie ngazi. Ukweli ni kuwa tulishinda na kwa kweli aliambulia matusi na kejeli toka kwa vijana machachari wa CDM humu JF.

Hapana, unavyonisoma ndio unafikiria nabadilika. Maji ukiyaweka kwenye kibuyu yatachukua nafasi ya kibuyu, ukiyaweka kwenye mtungi yatachukua nafasi ya mtungi, na ukiyaweka kwenye bakuli yatachukua nafasi ya bakuli. Sasa unaweza kusema maji "yanabadilika badilika" kuwa huyaelewi kama yana umbo la mtungi, kibuyu au bakuli. Sasa ukiangalia hivyo utakosa kuelewa sifa ya msingi ya maji. Ukinisoma ninapokosoa CDM unanifikiria ni kwa sababu naiunga mkono CCM, ukinisoma nikikosoa CCM na serikali unafikiria "ni mpinzani huyo" ukiona namtetea Amina Chifupa utasema ni mwana CCM, nikimtetea Sofia Simba ntaonekana anajipendekeza, nikimtetea Zitto utafikiria kuwa kwa vile ni jamaa yake n.k Well.. tatizo huangalii kanuni zinazoniongoza ambazo ndiyo kipimo pekee ninachokitumia katika siasa hizi. Sina ushabiki hewa wa watu au vyama.

Ninaamini nimefikia pale alipofikia Nyerere; CCM siyo mama yangu na hivyo hivyo CDM au chama kingine chochote. Kuna kanuni kubwa zaidi inaongoza kuliko mapenzi ya chama au watu. Vinginevyo, kile tunachokikataa kwa wana CCM ambao wanatukuza chama zaidi ndicho tunaweza kuja kuhangaika nacho pale wana CDM wanapoanza kutukuza zaidi chama!
 
sidhani kama nimesema kuna umimi; CDM ndicho chama pekee sasa hivi kinachoweza kujipanga na kuchukua madaraka ya nchi. Kumbuka kina mtaji mkubwa sana wa mapenzi ya watu wengi. Wapo watu wengi ambao wamejitolea na wanaendelea kujitolea hali na mali kukijenga. Lakini hili peke yake la kupendwa halitoshi kufanya wawe wanastahili. Fikiria hapa ninachokisema vizuri.

MMM nakushukuru sana kwa maelezo yako nimerizika ingawa bado hujaeleza nini hasa CDM imefanya hadi wewe kuipigia chapuo kuliko vyama vingine. Maana back in 2006 ulikuwa na allegations dhidi ya CDM sasa hujaeleza kama kasoro zilizokuwepo zimerekebishwa au laa as far as bado tunaona hulka za urafi wa madaraka miongoni mwa wanasiasa vijana ambao wengi wanaunda team ya CDM.

Isije kuwa umejump in CDM kusaka maslahi bila kuamini katika kuchukua dola maana kumbuka kwanza, umeshakiri kushiriki kuitengeneza ilani ya CDM ya mwaka 2010 (Bila shaka kwa malipo) na kwenye thread hiyo ya Mh.Freeman Mbowe (2006) umekiri kupigiwa simu na viongozi wa CDM wakikuahidi vyeo na maslahi fulani ili ujiunge na chama chao. Ulitoa madai haya baada ya wachangiaji wengi kukituhumu CCM kununua viongozi wa upinzani.

Othewise, maelezo yako sina shaka nayo. Utaendelea kuwa mentor wangu
 
Ni wengi tu wa namna hii, watu maslahi wapo kibao tu. Mfano mzuri yule mtu maarufu Prince Bagenda - fuatilia historia zao, kina muhingo Rweyemanu, hata Rweyemanu wa ikulu. Nakuhakikishia upo kweli sana waandishi wengi hufuata upepo hasa tokana na matamanio ya maslahi. CDM wakiingia leo nafasi ya Rweyemamu wa ikulu au ya yule waziri wa habari ni MMM bila ubishi
 
Kiukweli MM alifanya jambo jema. unajua kwa kipindi kile bado elimu ya ukombozi wa fikra ilikuwa haijaenea saaanaa kama sasa. Kwa hiyo hata mzee wetu MM alikumbana na tatizo la ignorance ya elimu ya Ukombozi, bt now imeshakolea kama kwetu sisi tuliowengi. Hongera MM kwa kukubali mabadiliko. VIVA CDM
 

Nimebadilika?
Ningeweza kuandika kwa kirefu sana juu ya hili lakini sijioni kama nimebadilika na badala yake kuelekea 2015 CDM inaweza kwenda ikiwa imegawanyika kuliko CCM!

Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015.

Mbowe na uongozi wote wa juu wangetakiwa kujiuzulu; na hata sasa labda kesi inaweza kujengwa ya kwanini wajiuzulu mapema zaidi (bado sijamaliza kuijenga hii hoja, inshallah).


Bado siamini kuwa CDM ilivyo sasa iko tayari kushika hatamu za uongozi wa taifa letu.

Chuki haitoshi kuwa sababu ya mabadiliko makubwa; inaweza kuwa kichochea lakini sababu inapaswa kuwa sera bora, dira bora, uongozi bora na mtazamo bora kuliko unaotolewa sasa.

Bahati mbaya CDM imejikita sana katika kuonesha kile ambacho baadhi yetu tulishakijua - CCM haistahili kuendelea kuongoza kwani sera zake zimeshindwa, itikadi yake imekufa na mwelekeo wake ni wa upotofu.

Hitimisho hili hata hivyo, halitufikishi kwenye kukubali CDM kama chama tawala alimradi.
[FONT=Verdana, Arial, Tahoma, Calibri, Geneva, sans-serif][FONT=georgia, Arial, Tahoma, Calibri, Geneva, sans-serif]
[/FONT][/FONT]

Na. M. M. Mwanakijiji
MKUU MM. MWANAKIJIJI, I SALUTE!- umemaliza kila kitu, umejibu kila kitu!. Niliposema Chadema haijajipanga, nilitukanwa sana humu!, maneno yako haya "Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015" nayaweka katika kumbukumbu zangu, tutakuja kuyazungumzia tena baada tuu ya uchaguzi 2015!.
P.
 


Mzee Mwanakijiji:.......Bado siamini kuwa CDM ilivyo sasa iko tayari kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Ndio maana utaona kuwa mimi pia siyo muumini wa "tuiondoe kwanza CCM halafu tutajua mbele ya safari". Siamini katika kuiondoa CCM ili tuingize chama kingine alimradi turidhike kuwa tumeiondoa CCM. Ninaamini yatupasa tuiondoe CCM kwa sababu kuna chama kingine kina sera na dira nzuri kwa taifa; kina viongozi wenye busara, na kinasimamia kanuni za msingi zilizojenga taifa letu.....,


Katu sikubaliani na hilo, ama sivyo kwa hawa wakoloni weusi, ukombozi wa pili hautakuja until kingdom comes. Nkrumah alisema: 'Seek ye political kingdom first' -- yaani kwanza pata utawala. Kwa dictum yako MMK, hata sisi ilitupasa tuwaambie Waingereza kuwa bado hatujawa tayari kuongoza nchi. Nijibu, Nyerere ilikuwa na watu wangapi, wenye kisomo gani wa kuchukuwa madaraka ya nchi kubwa kama Tanganyika?

Kama unakiri CCM inashindwa kuongoza, unaona tu bora ibakie madarakani kwa sababu tu upinzani haijajipanga kwa sera nzuri? Na bila shaka unaamini sasa kwamba ni rushwa tu na ghilba ndiyo huifanya CCM kuishinda katika chaguzi, na siyo ubora au kukubalika kwa sera zake. Nadhani pia utakubaliana nami kwamba iwapo tume ya uchaguzi NEC itakuwa huru kabisa pamoja na watendaji wake (siyo wale makada wa CCM -- aka returning officers) na TISS isiingilie matokeo, na rushwa katika kampeni isimamiwe vyema, basi CDM itashinda tu.

Itashinda pengine siyo kwa sababu ya sera nzuri, bali kutokana na kushindikana kwa sera za CCM.

Au unadhani hali ya namna hii ikitokea katika siasa ni dhambi?



 
MMM nakushukuru sana kwa maelezo yako nimerizika ingawa bado hujaeleza nini hasa CDM imefanya hadi wewe kuipigia chapuo kuliko vyama vingine. Maana back in 2006 ulikuwa na allegations dhidi ya CDM sasa hujaeleza kama kasoro zilizokuwepo zimerekebishwa au laa as far as bado tunaona hulka za urafi wa madaraka miongoni mwa wanasiasa vijana ambao wengi wanaunda team ya CDM.

Isije kuwa umejump in CDM kusaka maslahi bila kuamini katika kuchukua dola maana kumbuka kwanza, umeshakiri kushiriki kuitengeneza ilani ya CDM ya mwaka 2010 (Bila shaka kwa malipo) na kwenye thread hiyo ya Mh.Freeman Mbowe (2006) umekiri kupigiwa simu na viongozi wa CDM wakikuahidi vyeo na maslahi fulani ili ujiunge na chama chao. Ulitoa madai haya baada ya wachangiaji wengi kukituhumu CCM kununua viongozi wa upinzani.

Othewise, maelezo yako sina shaka nayo. Utaendelea kuwa mentor wangu

uzee unanijia kwa kasi; naomba nipe post namba ya mahali hapo niliposema hivyo ili angalau nijikumbushe.
 


Kama unakiri CCM inashindwa kuongoza, unaona tu bora ibakie madarakani kwa sababu tu upinzani haijajipanga kwa sera nzuri? Na bila shaka unaamini sasa kwamba ni rushwa tu na ghilba ndiyo huifanya CCM kuishinda katika chaguzi, na siyo ubora au kukubalika kwa sera zake. Nadhani pia utakubaliana nami kwamba iwapo tume ya uchaguzi NEC itakuwa huru kabisa pamoja na watendaji wake (siyo wale makada wa CCM -- aka returning officers) na TISS isiingilie matokeo, na rushwa katika kampeni isimamiwe vyema, basi CDM itashinda tu.

Itashinda pengine siyo kwa sababu ya sera nzuri, bali kutokana na kushindikana kwa sera za CCM.

Au unadhani hali ya namna hii ikitokea katika siasa ni dhambi?




ndio inaweza kushinda lakini ishinde ili kiwe nini? siyo ishinde ili CCM iondolewe madarakani
 
Ni wengi tu wa namna hii, watu maslahi wapo kibao tu. Mfano mzuri yule mtu maarufu Prince Bagenda - fuatilia historia zao, kina muhingo Rweyemanu, hata Rweyemanu wa ikulu. Nakuhakikishia upo kweli sana waandishi wengi hufuata upepo hasa tokana na matamanio ya maslahi. CDM wakiingia leo nafasi ya Rweyemamu wa ikulu au ya yule waziri wa habari ni MMM bila ubishi

na unafikiria na akili zangu timamu naweza kukubali? mmezoea watu wa maslahi sana kiasi kwamba hamfikririi kuwa mtu anaweza kuongozwa na kanuni zake mwenyewe bila maslahi zaidi.
 
Isije kuwa umejump in CDM kusaka maslahi bila kuamini katika kuchukua dola maana kumbuka kwanza, umeshakiri kushiriki kuitengeneza ilani ya CDM ya mwaka 2010 (Bila shaka kwa malipo)

umejuaje kwa malipo hadi useme "bila ya shaka"? well, free of charge! I could have charged it if I wanted but then ningeambiwa nimefanya kwa malipo!
 
Unajua ni kina nani waliandika ilani ya uchaguzi ya CDM ya 2010? Well, I was one of them. Kusema kuwa hata natumia siasa kufifisha ndoto ama matumaini ya Watanzania kuhusiana na mabadiliko kunaonesha ni kuwa hujafuatilia yale ambayo nimeyasimamia na kuyapigania tangu harakati hizi zianze. Bahati nzuri kama ni ufisadi wa serikali mimi mwenyewe nimeshiriki sana kuufichua; kama ni kuongoza mabadiliko kwa kadiri nilivyoweza nimefanya hivyo. Na kwa vile ulikuwepo muda mrefu hapa ama hutaki kukumbuka au katika kumbukumbu hiyo hutaki kuona.
Uchaguzi wa 2015 is do or die kwa Chadema!. Kuna maeneo niliainisha humu Chadema inahitaji kusaidiwa seriously na nikakushauri usaidie!. Kumbe tayari ulisha saidia kwenye ilani ya 2010!, sasa kuelekea 2015, Chadema needs help now more than at any other time!. Endelea kusaidia by proxy na ukiguswa zaidi, come down to ground zero and be part of the team to play the real game!.

Japo umesema "Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015"!, mimi "bado siamini kuwa by now time is too late too little to do something!. "Something is always better than nothing"!, "Do something!" ili hata itakapofika 2015, likitokea la kutokea, litatokea na dhamira yako haitakusuta kwa sababu utajifariji kwa kusema "At least "I did" something!, hili la kuendelea tuu kusema "something" imetosha sasa do something!.
P.
 
mzee Mwanakijiji hi mafia wa tanzania sijawahi kuiona nimetamani kujua kiliandikwa nini nitaipataje?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mwanakijiji salam,nimesoma kwa kina hatua kwa hatua na kwakweli naona ni busara kwangu kukipa nafasi kichwa changu kutafakari,umekuwa role model wangu kwa miaka minne sasa so kwa fikra jengefu umekuwa ukinijenga sana kiasi huwa najitahidi kusoma na kuwaza kwa mapana labda kuna siku nitakuwa kama wewe,nafaham u will proud kuwa na mfuasi wa fikra chanya.be blessed mkuu!

Acha kuabudu watu wewe mtoto wa kiume, umezaliwa mkamilifu, una akili timamu, unapojidharau kanakwamba akili zako si lolote wala chochote mbele ya mzee mwanakijiji unausikitisha umma!

Nyinyi bado mnagombana na nadharia wenzenu cdm wanatia fikra zao vitendoni, nisubirini ninywe togwa niwashushie mistari.
 
Back
Top Bottom