Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 niliamini kuwa Tanzania inahitaji mabadliko makubwa ya kiuongozi. Niliamini kabisa kuwa kiongozi atakayekuja atatakiwa kuwa mtu mwenye kukubaliwa na wananchi na ambaye atatumia kukubaliwa huko kuanzisha program ya haraka ya mabadiliko ili kuchochea maendeleo Tanzania. Sikumuona kiongozi huyo katika upinzani. Nilikuwa sahihi.
Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana. Wakati ule niliandika makala kadhaa kwenye mitandao ambazo zilielezea jukumu hili. Katika makala moja nilielezea kuwa Kikwete anaingia katika uongozi wa taifa letu wakati wananchi wanahitaji kiongozi atakayewaamsha kujiletea maendeleo. Nilisema ni mzigo tuliomtwisha Kikwete. Na nikatoa angalizo wakati ule endapo Kikwete atashindwa kukidhi matamanio ya Watanzania hakuna tena mwanasiasa mwingine yeyote ndani ya CCM atakayeweza kufanya hivyo kwa siku za karibuni.
Ushindi wake wa asilimia 80 ya wapiga kura ulikuwa ni ushindi wenye kurindima. Uliacha mwangwi wa kila nchi. Tuliomuunga mkono tuliamini kuwa atasimama na kuliongoza taifa letu vizuri zaidi akitumia mandate aliyokuwa ameipata. Furaha za Kikwete kuingia madarakani hazikudumu. Kikwete hakuitikia wito wa historia na badala yake alianza kuonesha udhaifu ambao wale waliokuwa wanamjua kabla walikuwa wanautambua; hakuwa kiongozi mwenye kuhamasisha (inspire) wananchi wake. Akaanza kufanya mambo ambayo mara moja mimi binafsi nilitambua ni alama za kiongozi dhaifu.
Hiki ndicho kilichotokea; ni kutambua kuwa CCM haiwezi kuleta mabadiliko tunayoyataka ; ni kutambua kuwa mabadiliko tunayoyataka yanatakiwa yaongozwe na fikra maridhawa ambazo zinaweza kugusa wananchi na wakazielewa. Siyo uzuri wa watu, na utamu wa majina yao bali uzuri na ukweli wa hoja zao.
Ni muumini wa fikra na si mfuasi wa watu
Sasa mtu anaweza kufikiria kuwa mimi nilikuwa mfuasi wa Kikwete; hapana. Mimi ni mfuasi wa fikra na kwa wanaonijua wanafahamu kuwa ni muumini wa fikra sahihi za Mwalimu Nyerere. Fikra hizi ambazo nimejifunza kwa kina na ninaendelea kujifunza siku kwa siku ninaamini ni sehemu ya alama za taifa letu. Baada ya Kikwete kushindwa kuonesha uongozi wa taifa letu na kutuhamasisha kujenga jamii ya kisasa niliamua wakati ule kuanzisha harakati za mapambano ya kifikra; yaani wananchi wetu ili waweze kubadilisha kura ni lazima kwanza wabadilishe fikra!
Ninaamini kimsingi mambo yafuatayo ambayo nimetokeo ya kujifunza Fikra za Mwalimu Nyerere:
a. Usawa wa watu wote unaotokana na usawa wa utu: Nimewahi kuliandika hili baadaye kuwa Nyerere aliona usawa siyo ule wa kisheria kutokana na wote kuwa sawa mbele ya sheria kama ilivyo Marekani bali ni usawa ambao unatokana na wote kuwa sawa sababu ya utu wao. Kwamba hakuna binadamu mwenye utu zaidi ya mwingine
b. Uongozi ni utumishi siyo ulazimishi: Ninaamini kuwa mtu anayetaka kuwa kiongozi anapaswa kuwa mtu anayetaka kutumika siyo kutumiwa au kutumikisha wengine.
c. Maendeleo ni ya watu siyo vitu: Mojawapo ya mambo makubwa kabisa niliyojifunza kutokana na fikra za Mwalimu ni dhana kuwa maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu ni udikteta wa vitu. Watu ndio msingi, kiini, sababu, lengo na njia ya maendeleo. Utawala wa CCM (hasa kuanzia Mkapa) umeweka mkazo mkubwa sana kwenye kuendeleza vitu; wanajivunia vitu, wanatuonesha vitu. Siyo watu walioendelea!
d. Siasa ni chombo tu cha kuchochea mabadiliko. Binafsi nachukulia siasa kama chombo cha kusaidia kuleta mabadiliko. Ninaamini siasa ikitumiwa vizuri kama kisu inaweza kutumika kumchuna ngombe vizuri, kukata majani, na hata kuchimba ardhini ili kuleta tunachotaka. Ikitumiwa vibaya inakuwa kama jambia mikononi mwa kichaa! Ina madhara. Hivyo ni muumini wa siasa bora na siyo bora siasa.
e. Wenye kushika madaraka wanashika kama dhamana si haki.
Ngoja nipate castle lager moja kwanz