Hapana, sitakataa ukinieleza mipango yenu. Namba hazidanganyi hata siku moja. Ukinieleza kuwa utakusanya jumla ya sh 100 hapa na pale, na utatumia sh 90 hapo sina ubishi, na haya ndio mahesabu ninayoyaomba hapa JF. Lakini ukasema kuwa utakusanya sh 100 na utatumia sh 110, hapo tutahitilafiana. Ninachohitaji ni kujua jinsi CHADEMA walivyojipanga kupata mapato na matumizi yake katika mahesabu ya karibu ya mwananchi.
Ukisema tutapunguza mishahara ya wabunge na viongozi wa serikali, ok. Lakini ninachohitaji kujua mimi ni NAMBA kuwa katika mapunguzo hayo utakusanya sh ngapi. Ninachotaka kuepuka ni kuzungumzia kuserve sh mil 100 wakati matumizi tunayoyazungumzia ni sh mil 200.
Mategemeo yangu ni kwamba mjadala ungekuwa wa kiuchumi zaidi kuliko wa kisiasa, pamoja na kuwa maamuzi ya kisiasa ndio yataongoza mfumo husika.
Kifupi bado sijapata kile nilichokitegemea huenda baadae kidogo.
Shukran sana nimekuelewa vizuri sana lakini hapa JF sii mahala pake kwa sababu haiwezekani kupata namba sahihi, hata mimi siwezi kupata jibu kwa nini Elimu bure haiwezekani kwa mahesabu ya CCM. Na hata kama nitauliza hapa sidhani kama nitalipata jibu sahihi, isipokuwa mara zote swali kama hili hutolewa wakati wa uchaguzi na namba zikatolewa kulingana na makusudio ya chama ktk kukusanya fedha hizo na matumizi yake..
Hivyo kama kweli wewe ni mwelewaji ktk vitu nilivyokupa hapo nyuma, nikikupa namba yoyote utaweza vipi kuhakikisha kama kweli ndicho kiwango kitakacho kusanywa?.. tuwe wakweli maanake Chadema wanaweza kusema kwamba watategemea kukusanya nusu Trilioni tokana na makato ya matumizi ya serikali! Kwa mfano ktk misamaha wa kodi tunapoteza billioni 700, wewe na mimi tutaweza vipi kuhakikisha ukweli huu.. Hivi tulipo, hatufahamu rais wetu analipwa na kutumia kiasi gani, mawaziri wetu, wabunge wetu na kadhalika maanake haya yote ni maswala nyeti wao wakidai "Confidential" hatupaswi kujua pamoja na mikataba yake.
Leo tunakwenda walipa Dowans mabilioni, hizi fedha zinatoka wapi? Mlitwambia au nisema CCM walituambia huu ndio mwisho wa mahotel kubadilisha majina ili walipe kodi stahiki, lakini ndio kwanza Kilimanjaro na Sheraton zinazidi kubadilisha majina wakitumia Francise names ili tusipate kuwajua viongozi wanaomiliki hotel hizi tukiendelea kufikiria sijui za Mwarabu au Msomali alowekwa kupumbaza watu...
Kifupi mkuu wangu Elimu haichukui sehemu kubwa ya bajeti ya serikali hata Canada ambako Elimu ni bure utaona ni asimia ndogo sana ya bajeti yao inatumika ukilinganisha na matumizi ya wizara nyinginezo kwa sababu nyumba (madarasa) na vitabu ni vitu ambavyo vinadumu na elimu haiozi. Ukisha weka msingi bora matumizi yake makubwa yapo ktk mishahara na vifaa vya kufundishia.
Swala la majimbo ambalo wengi wanalizungumzia hapa, naweza kukubaliana nao ktk maswala mengine lakini sio Elimu kwa sababu jimbo moja linakuwa na mikoa zaidi ya minne hivyo pato la Jimbo moja linaweza kabisa kuwa kubwa kiasi cha kuweza kutosheleza Elimu pamoja na marekebisho makubwa ya ukusanyaji kodi...hili halina ubishi kabisa yaani ni aibu iliyoje kwa nchi kama Tanzania wanaolipa kodi hawafiki millioni 3 wakati hesabu ya watu waliojiandikisha tu kupiga kura ni millioni 19!. Eeeeh! yaani siasa ni muhimu zaidi ya kusisitiza ulipaji kodi, sasa tunategemea vipi kuendelea kiuchumi ikiwa siasa ndio zinatawala Uchumi..
Halafu pia tukumbuke Chadema hawajatueleza mpango huo utaanza rasmi lini? Hata wangeshinda uchaguzi ulopita wasingeweza kubadilisha kila kitu ikiwa ni pamoja na kuondoa sheria ya Mawaziri kuwa wabunge, kufuta kazi za wakuu wa mikoa, wilaya na kadhalika - both nature and the legal system must be moving gradually.
Kitu kimoja muhimu ambacho nakuomba tuwe pamoja.. Tanzania fedha ipo, isipokuwa tumekuwa na kiburi cha umaskini hata tukikopeshwa fedha tunataka tusipangiwe jinsi ya kuzitumia kwa sababu tunamiadi nje ya maendeleo ya nchi yetu. Miaka ya Nyerere na tulipewa mikopo ya maendeleo kwa jina la Tanzania, tukajenga reli ya Tazara, tukaanzisha shirika la ndege, tukajenga viwanda vya Ufi, Pamba, Kahawa, Korosho n.k na hata baiskeli zilitengenezwa Tanzania..Leo hii hawa wachawi wanatuambia - Hatuwezi kupata mikopo isipokuwa kwa kupitia mashirika ya nje. Tazama mikataba ya leo ikiwa ni pamoja na huu wa Mchuchuma..tunashindwa kupewa mkopo sisi kwa sababu hatuaminiki!..tunaficha nini ukweli huu, tumeuza uhuru wetu kwa sababu tumeharibu wenyewe jina la nchi yetu kwa matumizi mabaya ya mikopo! Nchi kibao zimetukatia na pengine hata WB nao hawatuamini tena isipokuwa kwa masharti yao..
Halafu hawa viongozi wanakuja bila aibu na ujasiri wa kutuambia mkataba huu ni mzuri sana hali sii mkataba wetu sisi na Bank wakopeshaji kisha hao wawekezaji wakawa contracted, bali ni mkataba wa wawekezaji na bank ambao wanatumia mali yetu kama dhamana yao na wanachukua asilimia kubwa ya pato!..Upuuzi kama huu hata siku moja siwezi kukubaliana nao hata kidogo pamoja na kwamba tunahitaji umeme!
Asikudanganye mtu, hakuna kitu kisichowezekana maadam tutaweka nia kinawezekana kabisa.