Bado unajaribu kutumia akili ya Upinzani kuuliza swali. Chadema hata wakikupa maelezo yao maadam wewe unapoingana na sera zao huwezi kuona inawezekana! lazima utaona mapungufu upande wa pili kwa sababu sera zako ni pinzani.Ulianza vizuri lakini umemaliza vibaya. Ninachowaomba mimi ni bajeti yenu kivuli inayoambatana na ukusanyaji kodi (kwa muona wa CHADEMA) na matumizi ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu bure.
Pengine niwe wazi hapa- Kuwa cha BURE KABISA HAKIPO, SWALI ni nani atalipa. Nilivyowaelewa katika kampeni yenu 2010 ni kuwa mtatumia fedha za kodi ya wananchi kutoa elimu bure. Ninachowaomba ni kuiona bajeti hiyo hapa JF ili nielewa kama inawezekana au ni Propaganda za uongo za kuingilia IKULU.
Kwa mfano Chadema wakisema, watapunguza mishahara ya wanasiasa haswa rais, Mawaziri, Wabunge, Kuondoa kabisa manunuzi ya mashangingi na posho za vikao vya bunge, kupunguza gharama za safari na misafara ya rais na mawazirii zisokuwa lazima na kadhalika..Je, utaweza kuelewa na kutoshelezwa?
Hivi vyote, bado hutaelewa kitu kwa sababu huelkewi ni kiasi gani kitakusanywa kutokana na hayo, halafu utaanzisha Ubishi ktk sera ambazo hukubaliani na baadhi ya maamuzi kutokana na mtazamo wako. Halafu, tuacha kuwa wana Chadema au CCM, binafsi naamini kabisa inawezekana kama tukianza na kurekebisha sehemu muhimu za ukusanyaji wa kodi. TRA ifanyiwe marekebisho makubwa sana ktk utendaji kazi wake, iwezeshwe kwa vifaa vya kimataifa. Kila mwananchi awe na TIN namba yake - iwe lazima na ndicho kitambulisho.. Kodi ikishushwa na kuwa asilimia 10 hadi 15. KIla mapato yalipiwe kodi ktk transaction zote zenye kurekodiwa..Nina hakika wananchi na wafanyabiashara wengi watalipa kodi halali kuliko sasa hivi wanapotozwa kodi kubwa sana hivyo hupitia mlango wa nyuma. Kwa kutoza asilimia 10 serikali itaweza kukusanya zaidi pato la taifa kuliko leo hii bila ongezeko la uzalishaji. Licha ya hivyo less than 3 millioni ya wananchi ndio wanalipa kodi hata ukichukua hesabu ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura - Hii ni aibu kwa nchi!
Moja ya sababu kubwa za Udini nchini zimetokana na mfumo tenge wa ELIMU..Mtazungumza yoote mnayoweza kuyasema lakini kwa mfumo wa ELIMU uliopo leo hii nchini, Udini utazidi kupata nguvu kubwa sana na pengine hata itakuja tokea vita. Nawasoma watu wote wanavyoandika hapa JF wenye jazba na majigambo, wengine matusi mazito mazito kwa sababu hakuna tsababu ya ujenzi wa chuki baina ya Muislaam na Mkristu isipokuwa kupitia Elimu..
JK sio sababu ya Udini nchini, yeye anatumia Udini uliopo kwa manufaa yake. Kwa wananchi wasiokuwa na Udini, JK hawezi kuwachonganisha atachekesha.. Hivyo nitawakumbusha tena Udini nchini Tanzania unatokana na mfumo wa elimu duni uliopo unatuathiri sote wazawa Waislaam kwa wakristu wakati wageni wanachukua nafasi hizi kutawala uchumi wetu..