Propaganda za uongo: Elimu bure, CHADEMA ikishinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za uongo: Elimu bure, CHADEMA ikishinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Oct 18, 2011.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mwalimu NYerere alitoa elimu bure, matokeo yake baada ya miaka 20 nchi ilitembelea magoti. CHADEMA (Mh Slaa) japo ya kujua hilo bado ilisisitiza kutoa Elimu bure kwa watanzania wote ili ishinde uchaguzi 2010, lakini ikaanguka. Hii ni kutokana na ueleo mkubwa wa watanzania na kuelewa kuwa hizo ni PROPAGANDA ZA UONGO.

  Wiki iliyopita nilipoandika Thread "CHADEMA NI CHAMA CHA PROPAGANDA" wengi walidai nilete ushahidi au vyanzo vya taarifa hizo. Sikufanya hivyo kwa kuogopa Mod kuifuta habari hiyo. Leo nimeamua kuandika ushahidi wa Propaganda hizo za uongo tukianzia kwenye kipengele cha ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE.

  Ili twende hatua kwa hatua naona vyema tuanzie na mkoa wa Kilimanjaro ambako ndio Ngome ya CHADEMA ilikojikita. Naomba waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA aeleze kinaga ubaga ni vipi kwa kutumia kodi ya mkoa wa Kilimanjaro itamudu kutoa elimu bure kwa wananchi wa mkoa huo kabla hatujazungumzia Tanzania nzima.

  Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania nzima kwa kuwa na shule za Sekondari nyingi kuliko mikoa yote ya Tanzania. Una sekondari 288 wakati hata Dar es salaam ina sekondari 252 tu (Chanzo: www.moe.go.tz/NectaResuls). Wakazi wa kilimanjaro ni 1441000 ukilinganisha na Dar es salaam ambao ni takriban 2,809,000 (Chanzo: Tanzania: Regions, Major Cities & Urban Localities - Statistics & Maps on City Population). Pato la kodi la mkoa wa Kilimanjaro (Rombo, Hai, Mwanga, Same, Mosho mjini na Moshi vijijini) ni 14,236.4 Milioni (Tzsh) wakati lile la Dar es salaam ni 441,000.5 Milioni (Tzsh) (Chanzo: Tanzania Revenue Authority - Kigoma).

  Kabla sijaandika zaidi naomba huyu waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA akisaidiana na wapambe wake hapa JF wanieleze ni vipi watazigawanya hizo 14,236.4 milioni Tzsh katika huduma za matibabu (hospitali, zahanati na elimu ya afya), Polisi, utawala mkoa na wilayani, pembejeo, na Elimu (mishahara ya walimu, ukarabati na stationaries).

  Mkishindwa kufanya hivyo maana yake ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE NI PROPAGANDA YA UONGO. Vinginevyo mlitaka kutumia pesa ya walipa kodi wa mikoa mingine kuendeleza mkoa wenu maana kiuchumi haiwezekani Kilimanjaro yenye wakazi 1441000 iwe na shule kupita Dar es salaam yenye wakazi 2,809,000.

  Nasubiri majibu yenu kabla sijaendelea na sekta nyingine.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tanzania haikutembea magoti kwa sababu Nyerere alitoa elimu bure. Tanzania tulianza kutembea magoti baada ya vita vya Idi Amin. Be factual.
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Really? kwanini alienda vitani?
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  wewe ni boya sana
  Hivi unajua serikali yetu inawasaidia wafanyabiashara wakubwa kufanya TAX AVOIDANCE/EVASION??? tena katika mpaka wa Kilimanjaro na Kenya usiseme yaani ukiwa kada wa CCM biashara zako hulipi kodi.

  Hivi unajua ni kiasi gani KAMPUNI iliyobinafsishiwa Uwanja wa ndege wa KIA inapora kila mwaka???
  Hivi unajua katika kipindi cha mwaka 2009-2010 kampuni hii haionekani katika orodha ya waingiza mapato wa Tanzania wakati 2008-2009 iliingiza bilioni kadhaa???
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  alienda vitani kumwondoa muislam mpuuzi aliyekuwa anauwa watu kwa amri za shehe uganda
   
 6. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona sasa kuna haja ya kuwachunguza baadhi ya watu,naona kuna wengine sio raia wa nchi hii kabisa,we mleta mada unatokea nchi gani?
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huhitaji kwenda shule kuelewa hiyo hoja ya elimu bure!! Elimu bure inawezekana, fanya homework yako vizuri tutakuelewa kama utatuletea facts siyo kuturudisha nyuma wakati tuko karne ya 21.
   
 8. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Topical, is it real that you don't know or I'm missing something from your post?
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ala! kumbe haya umefurahi? sasa
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa umenena mkuu
   
 11. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  magawanyo wa rasilimali za nchi hii hutegemei pale zinapotoka, mapato ya Dar es salaam au kwenye migodi yanawafaidisha hata wamakonde wa Newala na wamakua wa Masasi. Sasa jiulize, mapato ya serikali yanakwenda wapi? si ndani ya mifuko ya mafisidi waliorundikana serikalini na kwenye chama cha Magamba?

  Nyerere alisema inchi corrupt haikusanyi kodi, Tanzania ni nchi corrupt, kodi haikusanywi hata kile kidogo kinaishia kugharamia kuiba kura kwenye hata vichaguzi vidogo, sahau Kagoda, Meremeta, EPA n.k Nchi ina viongozi wa ajabu sana (CCM) wawekezaji wanapewa tax relief ya miaka mitano ikiiisha anauza anaingia mwingine naye anapewa miaka mitano mpaka miaka 50 mingine ya uhuru(itakuwa 100) kodi haikusanywi.

  Madini hayatusaidii chochote,tumeshindwa hata kujifunza kwa wenzetu wa Botwsana, Zambia nk. hebu jiulize wewe Ngonda, TZ sasa inaweza jifananisha na Rwanda waliochinjana miaka 15 tu iliyopita? posho za vikao na nguo za bure za kijani zisikufanye upoteze utu wako.
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi nashangaa sana watu wanavyoona CDM jinsi ilivyokuwa waongo wakasahau ahadi za JK zilivyokuwa za uongo na zisizotekelezeka.

  Mimi naamini kabisa kama JK amekasirika kupita kiasi ukimpa mikanda ya kipindi cha kampeni yake ni LAZIMA atacheka sana na hasira kwisha kabisa kwa jinsi atavyojishangaa ujasiri wa uongo kiasi kile aliukoupatai! Hata leo zikifanyika kampeni natumani hawezi kudanganya kama awamu iliyopita.
   
 13. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha ha ha! Nimegundua Kuna Watu Kilimanjaro Inawawasha Kama Upupu!
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Topical mbona unanishangaza? How old are you? Hujui IDD AMIN alichofanya Kagera. Yaani wewe ningekutukana vibaya hujui ndugu zangu na babu zangu waliokufa huko Minziro walikuwa wangapi yaani wewe zuzu. Akili zako kama za JK ambaye haijui Dowans, Hajui kwa nini Tanzania ni Maskini. Na wewe upo upo.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  AHADI ZA KIKWETE KWA WAPIGA KURA KATIKA KAMPENI ZA URAIS 2010.

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
   

  Attached Files:

 16. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180

  Najiuliza kama hoja hii imejengewa kichwani kwa mtu au Kwenye nyonyo!!!! Tunasubiri Meli Mpya aliyoahidi KIkwete kuliplace Mv Bukoba iliyosababisha niwe Orphan.
   
 17. M

  Marytina JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  unaweza kukuta Topical ana masters nzuri tu ila anashinda manzese bakresa kwenye midahalo ya dini manake pale manzese niliwahi kusikia hii hoja ya nyerere aliivamia UGANDA kumwondoa muislam madarakani.Foleni ilisogoa nikashindwa kujua kwa nini shehe alikuwa ya hayo madai.
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sijui bana si wewe una akili sana niambie mkuu wangu?

  Eh kulitokea nini huko kagera? aise nijuze
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Programmed mind
   
 20. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Maneno mengi yanini. Wewe toa makadirio yako ya kodi na unipigie hesabu ya matumizi katika sekta zote mkoani na utoe balance. Usikosoe tu jaribu kuja na majibu mliyonayo kwa data unazozielewa wewe.
   
Loading...