Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Miaka yote hiyo walikua wapi bila kufanya tafiti hyo baada ya brazir kutoa taarifa ndo na wao wankurupka kufanya tafiti ili wajurikane....piga chini
Mdau wewe upo dunia gani wewe???baada ya matatizo ya brazil na dunia ni kijiji usidhan ni Tz tu ndo wamefanya dunia imefanya na inapambana na ZIKA na ebola,unataka itokee ndo tufanye???
Hao NIMR hizo ndo kazi zao (MAGONJWA YA BINADAM)
 
Kitila Mkumbo nazani hajaona athari la ili tangazo, mfano mimi nilikua na Mpango na my wife wangu mwezi ujao abebe mimba ila baada ya tangazo la Zika lilitustua, tukasema tusitishe ishu ya kubeba mimba, sasa watanzania wangapi wameathiliwa na ili
Umeskiliza na kuangalia video ya Dr Malecela???
Kauiskilize kwenye mwananchi online.
Amesema kabisa hakuna haja ya kujifanya jambo halipo wakat lipo,
 
Malechela kafanya poa coz wanasiasa wanafichaficha mambo. Poa sana dadake le mutuz
 
Je, aliwa inform ministers kabla ya kuongea na BBC?

..umemsoma vizuri Dr.Kitila?

..taarifa tayari zimechapishwa kwenye ma-journal ya utafiti huko nje.

..serikali itueleze baada ya kumtimua kazi Dr.Mwele inachukua hatua gani? Maana bado wingu la utafiti aliofanya liko palepale?
 
Nadhani upeo wako ni mdogo sana katika suala hili.
Ngoja nikupe ufafanuzi.

1/NIMR ndio chombo rasmi cha serikali katika kusimamia tafiti zote za Afya hapa Tanzania. Kipo chini ya wizara ya Afya Makao makuu, na kinajukumu la kuanzisha, kuendesha na kuhitimisha mwenendo wowote wa tafiti zote za Afya hapa Tanzania.

2/Ni kosa kubwa sana kwa taasisi yoyote kufanya tafiti za kisayansi na mwisho wa siku kutokutoa matokeo ya tafiti hizo au kuchelewesha kwa makusudi matokeo ya tafiti hizo au kupotosha kwa makusudi matokeo ya Tafiti hizo (Kitaalamu inaitwa Research Misconduct, na moja ya adhabu yake kimataifa ni kuzuia kabisa kwa taasisi husika kufanya utafiti tena).

3/Utafiti wa kisayansi ni mali ya jamii iliyohusika katika utafiti huo. Utafiti sio mali ya mtu au serikali. Sio jukumu la serikali au mtu binafsi kuamua kutoa au kutokutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi uliokwisha kufanyika. Kuzuia au kuchelewesha kutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi ni sawa na kuiba haki ya jamii.

4/Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kutangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika(Research Findings) na kutangaza mlipuko wa ugonjwa kwenye jamii(Epidemic).
Mkurugenzi wa NIMR alitangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika na wala hakutangaza mlipuko wa Zika hapa Tanzania.
Nimekuelewa sana mkuu. Hapa ndo watu wamechemka kuelewa.
 
Watanzania hawezi kuwa na taharuki wao wameisha zoea majongwa. Kwanza huu ugonjwa was zika hawaujui walio wengi 95 kwao ungekuwa kama wimbo wa ccm mbele kwa mbele.
 
Katika serikali zetu hizi za kiafrica ambako demokrasi zetu ni complicated, haya mambo ya double standard ni ya kawida kabisa. Huku kwetu wanasiasa wanatafuta platform kwa mbinu zo zote.
Hivi tujiulize huko wizara ya afya hakuna Management meetings!
Je Dr Malechela ilikuwaje akafanya huo utafiti
Alipata wapi fedha za kufanya huo utafiti
Je NIMRI ni autonomous au inasimamiwa na kuregenzi huko wizarani
Kama hizi link zote zipo ilikuwaje mkuu wa taasisi kutoa tamko.
Ina maana mfumo mzima wa serikali una matatizo kwenye utawala.
Kama mfumo wa utawala ungekuwa mzuri kila mtumishi kujua mipaka yake ya kazi haya yote yasingetokea. Hapa mimi naona kuna shida.
Zamani chuo cha Uongozi Mumbe kilikuwa kinatoa management skills kuanzia wakuu wa idara hadi top executive, ESAMI hivyo hivyo. Kivukuni walikuwa wanafundisha skills za siasa. Viongozi walikuwa wanaandaliwa siyo kuteuliwa. Ukiteuliwa umeiva and you real deliver siyo kubebana. Kwenye utawala solution siyo kufukuza ila ni kuelekeza mtumishi asifanye au kurudia makosa. No body is perfect . Hapa Mwele hana makosa makosa wanayo hao wakubwa zake kwa sababu walijua hiyo reseach inafanyika, hivyo ilbidi wawe wanapata progress report kwa kila hatua kwa njia ya vikao.
Mimi nilikuwa nawadmire sana Wilson Mkama, Charles Keenja, Sumaye, Salum, Sokoine, Mkapa, Baba waTaifa hawa viongozi walifanyia haki uongozi. Mara nyingi kiongozi mzuri huwa anajiwekea self check and balance system ili apate muda wa kutumia ubongo wake vizuri kwenye kutatua matatizo ya uendeshaji wa taasisi
Hebu to deal na namna ya kutatua matatizo ya kawaida ya mtz, hayo mengine tuachie check and balance(CAB). Kama hazipo ziwekwe zanazosuit hii AWAMU.
Mwele ni victim of the circumstances apewe kazi nyingine we still need her, alitutoa matende na mabusha. Actual huyu ndiye anayefaa utawala huu, speed yake safi amewazidi hata mabosi zake.
Akiachwa atachukuliwa na wengine , actually she is innovative focused intelligent courageous.
 
Ni sheria gani inayomruhusu mtumishi wa umma kutoa maatokeo ya utafiti bila ya kuelekezwa na Wizara husika au Bodi?
 
Profesa mkumbo aeleww
Hakuna aliyepingana na utafiti
Tatizo ni njia iliyotumika kufikisha taarifa kwa umma
Unasababisha public panic pasipo sababu za msingi
Pia Dr Mwele ilipaswa kupima madhara yanayoweza kusababishwa na habari za utafiti wake huo kwa nchi yetu
Kwa yeyote sio kila kitu hutangazwa hadharani
Ugonjwa wa Zika sio kitu cha kutangazwa na mkurugenzi wa NIMR
huo ni taaruki ya dunia
Am sure imesababisha damage kubwa sana katika sekta ya utalii
Na hii inaweza tumiwa na maadui wa nchi yetu
Uzalendo ni muhimu
Wakati nchi inatangaziwa ugonjwa wa dengue waliotangaza walijali panic itakayoikuta jamii? Leo kukiibuka kipindupindu watu hawapaswi kuambiwa kisa kutatokea panic kwenye jamii?
 
Magufuli ana beef na Familia ya Malechela, Pia anahonga baadhi ya viongozi ili wamuunge mkono, Mfano Mwinyi alijiropokea kuwa Nchi inaenda Kama Gari halina Msukani, Nafikiri Magufuli akamlilia kuwa Unani nahii hivyo Wakati Mwanao nimempa Wizara ya ulinzi, yaani mzee ndio unalilipa kwa hayo!

Basi acha Mwinyi atoke nje na kumwaga misifa! Ila ukimsikiliza unajua ni igizo. How can you turn arround so fast!



Muda wa siku chache baadaye

 
Professor Kitila Mkumbwa anaelewa ni kitu gani hasa Dr Mwele alitangaza? Na analewa protocol za kutangaza magonjwa ya mlipuko kama ZIKO zikoje na kwanini hizo protocol ziliwekwa? Kila kitu kiko wazi, sasa kwanini Prof Mkumbo anashindwa hata kusoma na ku-articulate hizo protocol badala ya kudhalilisha u-professor wake? aibu gani hiyo? Au anafananisha report ya NIRM na report zake za elimu ya jamii anazochapisha kwenye journals?

Ni vema Professor Mkumbo akaelewa watu hawapingani na matokeo ya utafiti ila utaratibu alioutumia Dr Mwele is completely out of order. Dr Mwele angekuwa raia wa nchi nyingine Watanzania wangekuwa na haki ya kumuona kama mtu mwenye njama za kuuwa uchumi na kuleta taharuki kwa jamii. Kosa limefanyika na Dr Mwele na taifa tujifunze.
 
Ebu SOMENI hili andiko Mwana JF mmoja kaandika na Prof.asome pia.

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.

Pole sana, maana uko katika karne ya ujima. Hata sikuelewi unachotaka kutueleza. Ukweli uko mbali sana na unahitaji msaada.

Kwa kukusaidia, suala la taaluma halibadilishwi hata nukta. Kama katika taaluma utaingiza siasa, fanya upendavyo ila la msingi la kuelewa ni kwamba unaweza kuficha ugonjwa lakini kifo kitakuumbua.

Endeleeni kujidanganya hivyo. Acheni wafu wazikane.
 
mm najiuliza, mbona serikali imetumia nguvu sana kukanusha na kumchulia hatua hyou mkrugenzi, kwana hakuna taratibu za kumuonya kiongz kama hyo, kuitna na kukosoana au hvyo vitu utawala huu hakuana?
Kwenye kampeni zake Mh. Rais alihaidi wazi kabisa kwamba kiongozibwa umma akikosea hakuna msamaha. Anaondolewa na anawekwa mwingine. Bila kuangalia sura rangi dini kabila au uhisiano wake na Rais.

Hivyo anayimiza ahadi aliyoitoa hadi ikampatia kura za kuingia ikulu.

Ieleweke kwamba huko nyuma watanzania tulilaumu sana tabia ya kuhamisha viongozi wanaokosea mahala n kuwapeleka pengine.
Nadhani upeo wako ni mdogo sana katika suala hili.
Ngoja nikupe ufafanuzi.

1/NIMR ndio chombo rasmi cha serikali katika kusimamia tafiti zote za Afya hapa Tanzania. Kipo chini ya wizara ya Afya Makao makuu, na kinajukumu la kuanzisha, kuendesha na kuhitimisha mwenendo wowote wa tafiti zote za Afya hapa Tanzania.

2/Ni kosa kubwa sana kwa taasisi yoyote kufanya tafiti za kisayansi na mwisho wa siku kutokutoa matokeo ya tafiti hizo au kuchelewesha kwa makusudi matokeo ya tafiti hizo au kupotosha kwa makusudi matokeo ya Tafiti hizo (Kitaalamu inaitwa Research Misconduct, na moja ya adhabu yake kimataifa ni kuzuia kabisa kwa taasisi husika kufanya utafiti tena).

3/Utafiti wa kisayansi ni mali ya jamii iliyohusika katika utafiti huo. Utafiti sio mali ya mtu au serikali. Sio jukumu la serikali au mtu binafsi kuamua kutoa au kutokutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi uliokwisha kufanyika. Kuzuia au kuchelewesha kutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi ni sawa na kuiba haki ya jamii.

4/Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kutangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika(Research Findings) na kutangaza mlipuko wa ugonjwa kwenye jamii(Epidemic).
Mkurugenzi wa NIMR alitangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika na wala hakutangaza mlipuko wa Zika hapa Tanzania.
 
Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
Mkuu alipokuwa akitangaza alikuwa na Mawaziri wote wa afya, waziri na naibu wake
 
Back
Top Bottom