Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
Kwa hiyo name wale wa TMA watabiri wa hali ya hewa wanapokuwa na taarifa sahihi za kutokea kimbunga au mvua kubwa zenye kuhatarisha maisha yetu yawapaswa kumwambia waziri husika atangaze na sio kazi ya Dr. Kijazi kuuhabarisha umma?
 
Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
Namna gani ya kuuambia umma au namna gani ya kuuficha umma? yaleyale ya Ukimwi Bukoba uliingia muda mrefu watu wakawa wanaficha na kuupa majina mengine
 
Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
kuuambia au kuudanganya??
 
Hivi Dr.Mwele alikuwa anatangaza kuwa ZIKA ipo au alikuwa anatoa taarifa ya matokeo ya utafiti kuhusu ugonjwa wa ZIKA!!? Hivi matokeo ya utafiti mnataka akayatangaze Ummy Mwalimu!!?

Hayo mambo mengine ya kutangaza rasmi hao wanasiasa yangefuata baadae lkn kwanza taarifa ya kutalaamu lazima iwekwe public na watalaamu wenyewe na ndicho kilichofanyika...!!

Hivi kwa kutangaza ummy mwalimu kuwa ugonjwa wa ZIKA haupo ndo hautakuwepo kweli!? Yaani watalii ni muhimu kuliko sisi??
Yaani upo sahihi kabisa. Mambo ya wataalamu waachiwe wataalamu tu, mambo ya wanasiasa yabakie kwa wanasiasa wenyewe.
Dr. Mwele Malecella alikuwa anatupa matokeo ya utafiti walioufanya(Jambo ambalo ni la kitaalamu), wadau wengine(ikiwemo serikali) ndio tungefuata hatua za kuchukua kulingana na matokeo ya tafiti hizo.

Nami bado najaribu kuwaza tu, je nini kitabadilika katika matokeo hayo hata baada ya Dr.Mwele Mallecela kufukuzwa kazi?
 
Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
Professor anakuwa kama bavicha bana!
 
Mbona Repoa na synovate hutangaza wenyewe matokeo ya tafiti bila kuhusisha mawaziri?kuuliza siyo ujinga
Swali la kufikirisha sana. Yaani REPOA ama ESRF wanapotangaza tafiti zao zenye kuonyesha kiwango cha umasikini wa kutisha, hilo haliwezi kuleta shock, kwa sababu watanzania wamezoea kusikia habari za kwamba wao ni masikini. Lakini NIMR kutangaza preliminary findings za ugonjwa wa Zika kumeonekana kero!

[HASHTAG]#justthinkingaloud[/HASHTAG]
 
Profesa mkumbo aeleww
Hakuna aliyepingana na utafiti
Tatizo ni njia iliyotumika kufikisha taarifa kwa umma
Unasababisha public panic pasipo sababu za msingi
Pia Dr Mwele ilipaswa kupima madhara yanayoweza kusababishwa na habari za utafiti wake huo kwa nchi yetu
Kwa yeyote sio kila kitu hutangazwa hadharani
Ugonjwa wa Zika sio kitu cha kutangazwa na mkurugenzi wa NIMR
huo ni taaruki ya dunia
Am sure imesababisha damage kubwa sana katika sekta ya utalii
Na hii inaweza tumiwa na maadui wa nchi yetu
Uzalendo ni muhimu
Kugundua nigundue mie kutangaza utangaze wewe kweli majanga
 
Nadhani upeo wako ni mdogo sana katika suala hili.
Ngoja nikupe ufafanuzi.

1/NIMR ndio chombo rasmi cha serikali katika kusimamia tafiti zote za Afya hapa Tanzania. Kipo chini ya wizara ya Afya Makao makuu, na kinajukumu la kuanzisha, kuendesha na kuhitimisha mwenendo wowote wa tafiti zote za Afya hapa Tanzania.

2/Ni kosa kubwa sana kwa taasisi yoyote kufanya tafiti za kisayansi na mwisho wa siku kutokutoa matokeo ya tafiti hizo au kuchelewesha kwa makusudi matokeo ya tafiti hizo au kupotosha kwa makusudi matokeo ya Tafiti hizo (Kitaalamu inaitwa Research Misconduct, na moja ya adhabu yake kimataifa ni kuzuia kabisa kwa taasisi husika kufanya utafiti tena).

3/Utafiti wa kisayansi ni mali ya jamii iliyohusika katika utafiti huo. Utafiti sio mali ya mtu au serikali. Sio jukumu la serikali au mtu binafsi kuamua kutoa au kutokutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi uliokwisha kufanyika. Kuzuia au kuchelewesha kutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi ni sawa na kuiba haki ya jamii.

4/Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kutangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika(Research Findings) na kutangaza mlipuko wa ugonjwa kwenye jamii(Epidemic).
Mkurugenzi wa NIMR alitangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika na wala hakutangaza mlipuko wa Zika hapa Tanzania.
Kwa hiyo hapo ndo umeonyesha upeo mkubwa kwa akili yako.
 
Swali la kufikirisha sana. Yaani REPOA ama ESRF wanapotangaza tafiti zao zenye kuonyesha kiwango cha umasikini wa kutisha, hilo haliwezi kuleta shock, kwa sababu watanzania wamezoea kusikia habari za kwamba wao ni masikini. Lakini NIMR kutangaza preliminary findings za ugonjwa wa Zika kumeonekana kero!

[HASHTAG]#justthinkingaloud[/HASHTAG]
Mkuu mimi nimeogopa maana nilikuwa naziamini sana tafiti za uchaguzi kuliko zile tabiri za kina TB Joshua!
 
Tofautisha mbegu za ubuyu na ugonjwa wa zika.


Uwezo wa Prof.ni wa kitilia shaka
Walisema mbegu za ubuyu yale mafuta yake yana athar kubwa kiafya,tangazo la TFDA lilikua likibainisha issue ya mbegu za ubuyu na athar zake kiafya.......
Na ZIKA ni suala la kiafya,sasa hapo tunatofautishaje mdau
 
Sipingi utafiti wa NIMR hata kidogo, na siwezi kupingana nao, ila tatizo ni uropokaji wake kwenye media, huwezi kuropoka tu hilo swala hadharani tena sasa ilikuwa haijawa rasmi kuwa kweli upo Tanzania...

Wewe unajua media za Tanzania zilivyo, zingeanza kuandika mambo ya kuwaogofya na kuwatia hofu wananchi bure, kuna namna ya kuwaandaa wananchi kupokea taarifa nzito, na serikali inajua mbinu za kuwaeleza wananchi ili wasishtuke sana.

Wewe hao NIMR wamekuonesha wagonjwa wa ZIKA?

Kama ilikuwa ni utafiti wa awali kwa nini watangaze?

Issue ya ZIKA ni nzito, itoshe tu kusema kuwa, Tanzania hakuna ZIKA, mbona Zanzibar kuna MBU anayeambukiza ZIKA lakini hakuna ZIKA Zanzibar?

Yaan kuwe na ugonjwa wa ZIKA lakini Wagonjwa wasiwepo? mbona NIMR hawakutuonesha hao wagonjwa?

Hutu prof. Kitila naye bure kabisa, ZIKA siyo kama malaria ambayo mtu unajitangazia tu...ZIKA ina taratibu zake, kwanza, kufanya utafiti tena utafiti shirikishi, baada ya hapo WHO ndio inautangaza rasmi, kwa hiyo si kitu kidogo,
 
Na huyu professor nilishagundua English not richebo.

Badala ya kuandika exclamation mark "!" kaandika kama swali "?" ("What an attack on academic and intellectual freedom?" (sic).)

Halafu angeandika in English only.
 
Back
Top Bottom