Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
Bhas kazi zote afanye yeye.kulikuwa na umuhimu gani wa kumpa hyo kazi?alikuwa anataka afanye siri.
 
Wataalamu wamefanya utafiti kwa miezi kadhaa leo anayepinga kutokuwepo kwa vimelea vya ZIKA ametumia masaa machache tena bila utafiti.
 
Na huyu professor nilishagundua English not richebo.

Badala ya kuandika exclamation mark "!" kaandika kama swali "?" ("What an attack on academic and intellectual freedom?" (sic).)

Halafu angeandika in English only.

Exclamation mark ndiyo Kiingereza? Acha ujanja wa Form One wewe. Kama kosa la kiuandishi basi Professor amefanya kosa ktk matumizi ya "panctuation marks", which is common even among native English speakers, lakini siyo Kiingereza.
 
When you call yourself a Prof.yet you make unbearable grammatical errors.

Uwezo wa Prof.sio kabisa

First of all, Prof. Kitila is not calling himself a Prof. He earned professorship through his academic work. He didn't simply just start calling himself a professor. Second, a punctuation mark error is common and can simply be an oversight or a typing error. So, for you to conclude that "Uwezo wa Prof. sio kabisa" just because of a punctuation mark error ni kudhihirisha uj.inga wako wewe mwenyewe.
 
Ebu SOMENI hili andiko Mwana JF mmoja kaandika na Prof.asome pia.

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.
[HASHTAG]#JUSTICE[/HASHTAG] FOR LEMA
[HASHTAG]#BRING[/HASHTAG] BACK OUR BEN ALIVE
[HASHTAG]#FREE[/HASHTAG] MAXENCE MELLO
 
Kugundua nigundue mie kutangaza utangaze wewe kweli majanga

Sasa huyo dr ndie alie fanya au Wafanyakazi katika kitengo cha utafiti.Kwa nini mmoja wa hao Wafanyakazi (researcher) asitangaze aliye tangaza dr Malecela?
 
Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
Utaratibu wakudanganya! Ugonjwa upo waseme hakuna
 
Tusubiri watatatungazia mpaka tuhathirike kwanza,!! But sijaona sababu yakumfukuza.....mkubwa anafanya maamuzi while in panic something which for his position very bad!! Ugonjwa upo muda mrefu na ulianzia Uganda tangu ,early 90s,!
 
Here in tz tafiti is for degree and uprofessor only,!! In our politics we can accept or not, it depends on president wisdom!!
 
Nadhani upeo wako ni mdogo sana katika suala hili.
Ngoja nikupe ufafanuzi.

1/NIMR ndio chombo rasmi cha serikali katika kusimamia tafiti zote za Afya hapa Tanzania. Kipo chini ya wizara ya Afya Makao makuu, na kinajukumu la kuanzisha, kuendesha na kuhitimisha mwenendo wowote wa tafiti zote za Afya hapa Tanzania.

2/Ni kosa kubwa sana kwa taasisi yoyote kufanya tafiti za kisayansi na mwisho wa siku kutokutoa matokeo ya tafiti hizo au kuchelewesha kwa makusudi matokeo ya tafiti hizo au kupotosha kwa makusudi matokeo ya Tafiti hizo (Kitaalamu inaitwa Research Misconduct, na moja ya adhabu yake kimataifa ni kuzuia kabisa kwa taasisi husika kufanya utafiti tena).

3/Utafiti wa kisayansi ni mali ya jamii iliyohusika katika utafiti huo. Utafiti sio mali ya mtu au serikali. Sio jukumu la serikali au mtu binafsi kuamua kutoa au kutokutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi uliokwisha kufanyika. Kuzuia au kuchelewesha kutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi ni sawa na kuiba haki ya jamii.

4/Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kutangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika(Research Findings) na kutangaza mlipuko wa ugonjwa kwenye jamii(Epidemic).
Mkurugenzi wa NIMR alitangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika na wala hakutangaza mlipuko wa Zika hapa Tanzania.
Politicizing everything, the dwindling of everything!!!
 
Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
Mwele ni mtu wa Mungu huyu hivyo kusema uongo ni mwiko. Yeye sio watafiti wa siasa wa pale udsm
 
Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
Zika kuwepo Tanzania kulitangazwa na watafiti wa hospitali ya Bugando kwenye kongamano la 8 la wanasayansi mwezi wa 11 tarehe 16 na hawakuchukuliwa hatua. Utafiti huo uko katika chapisho lilo andikwa na Mariam Mirambo na wenzie..kwanini huyu aliye rejelea huo utafiti awe na kosa?
 
Ebu SOMENI hili andiko Mwana JF mmoja kaandika na Prof.asome pia.

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.
1482030373296.jpg
 
Kwa hiyo hapo ndo umeonyesha upeo mkubwa kwa akili yako.
Kama huwezi kuona facts zake hapa no wazi upeo wako mdogo kweli ngosha!
Hapa kaonesha upeo wake mkubwa kwa sababu kama wewe ulishawahi kufanya utafiti huwezi kushangaa alicho comment huyu ndugu.

Ila Mimi huwa naipenda jf maana inatoa matokeo chanya kuhusu vilaza na walio nazo!
 
Hatari sana kuchanganya hisia na uhalisia.

ZIKA ipo nchi nyingi tu na maisha yanaendelea tatizo tumefikia pahala ambapo inatubidi tuulize kwa mfalme kila kitu hata kama kipo kimamlaka yako kukisemea
 
Professor Kitila Mkumbwa anaelewa ni kitu gani hasa Dr Mwele alitangaza? Na analewa protocol za kutangaza magonjwa ya mlipuko kama ZIKO zikoje na kwanini hizo protocol ziliwekwa? Kila kitu kiko wazi, sasa kwanini Prof Mkumbo anashindwa hata kusoma na ku-articulate hizo protocol badala ya kudhalilisha u-professor wake? aibu gani hiyo? Au anafananisha report ya NIRM na report zake za elimu ya jamii anazochapisha kwenye journals?

Ni vema Professor Mkumbo akaelewa watu hawapingani na matokeo ya utafiti ila utaratibu alioutumia Dr Mwele is completely out of order. Dr Mwele angekuwa raia wa nchi nyingine Watanzania wangekuwa na haki ya kumuona kama mtu mwenye njama za kuuwa uchumi na kuleta taharuki kwa jamii. Kosa limefanyika na Dr Mwele na taifa tujifunze.
Haujamsikia Mganga mkuu wa Serikali na Waziri wakisema hamna Zika nchini?au una maana gani unaposema hakuna anayepingana na utafiti?
Siku zinavyokwenda mtaelewa tu!!
 
Sipingi utafiti wa NIMR hata kidogo, na siwezi kupingana nao, ila tatizo ni uropokaji wake kwenye media, huwezi kuropoka tu hilo swala hadharani tena sasa ilikuwa haijawa rasmi kuwa kweli upo Tanzania...

Wewe unajua media za Tanzania zilivyo, zingeanza kuandika mambo ya kuwaogofya na kuwatia hofu wananchi bure, kuna namna ya kuwaandaa wananchi kupokea taarifa nzito, na serikali inajua mbinu za kuwaeleza wananchi ili wasishtuke sana.

Wewe hao NIMR wamekuonesha wagonjwa wa ZIKA?

Kama ilikuwa ni utafiti wa awali kwa nini watangaze?

Issue ya ZIKA ni nzito, itoshe tu kusema kuwa, Tanzania hakuna ZIKA, mbona Zanzibar kuna MBU anayeambukiza ZIKA lakini hakuna ZIKA Zanzibar?

Yaan kuwe na ugonjwa wa ZIKA lakini Wagonjwa wasiwepo? mbona NIMR hawakutuonesha hao wagonjwa?

Hutu prof. Kitila naye bure kabisa, ZIKA siyo kama malaria ambayo mtu unajitangazia tu...ZIKA ina taratibu zake, kwanza, kufanya utafiti tena utafiti shirikishi, baada ya hapo WHO ndio inautangaza rasmi, kwa hiyo si kitu kidogo,
Hivi NIMR unaijua ndugu?! Maana kama unaijua basi huwezi kusema Dr Mwelle karopoka, kuropoka ni kama hivi kujibu au kuongea vitu usivyovijua kwa maana ya kwamba hujavitafiti.

Utafiti huwa hauoneshi physical things bali data hivyo kama ulitaka NIMR wakuoneshe hao wagonjwa wa Zika ilikupasa kwenda binafsi kwa mtafiti uombe akuoneshe.

Unaposema serikali ndio inajua namna nzuri ya kutangaza unamlenga mtu au kitu fulani referred to as serikali??
 
Nchi za kimasikini tuna magonjwa sana ndio maana babu wa Loliondo alipojitokeza tuu alipiga hela sana tunapenda kuficha ukweli wa ugonjwa ili iweje sasa..Nchi masikini fikra za kimasikini tuu..
 
Back
Top Bottom