Sipingi utafiti wa NIMR hata kidogo, na siwezi kupingana nao, ila tatizo ni uropokaji wake kwenye media, huwezi kuropoka tu hilo swala hadharani tena sasa ilikuwa haijawa rasmi kuwa kweli upo Tanzania...
Wewe unajua media za Tanzania zilivyo, zingeanza kuandika mambo ya kuwaogofya na kuwatia hofu wananchi bure, kuna namna ya kuwaandaa wananchi kupokea taarifa nzito, na serikali inajua mbinu za kuwaeleza wananchi ili wasishtuke sana.
Wewe hao NIMR wamekuonesha wagonjwa wa ZIKA?
Kama ilikuwa ni utafiti wa awali kwa nini watangaze?
Issue ya ZIKA ni nzito, itoshe tu kusema kuwa, Tanzania hakuna ZIKA, mbona Zanzibar kuna MBU anayeambukiza ZIKA lakini hakuna ZIKA Zanzibar?
Yaan kuwe na ugonjwa wa ZIKA lakini Wagonjwa wasiwepo? mbona NIMR hawakutuonesha hao wagonjwa?
Hutu prof. Kitila naye bure kabisa, ZIKA siyo kama malaria ambayo mtu unajitangazia tu...ZIKA ina taratibu zake, kwanza, kufanya utafiti tena utafiti shirikishi, baada ya hapo WHO ndio inautangaza rasmi, kwa hiyo si kitu kidogo,