Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Na huyu professor nilishagundua English not richebo.

Badala ya kuandika exclamation mark "!" kaandika kama swali "?" ("What an attack on academic and intellectual freedom?" (sic).)

Halafu angeandika in English only.
Kuwa kwamba alichoandika hujakielewa au?!
 
View attachment 447321hii ndio sharia iliyotumika na Serikali kuchukua uamuzi huo. Alitakiwa kuwasiliana na Serikali kupitia wizara ya Afya ili Serikali nayo ione kama upo umuhimu na pia ijipange Kwa ajili ya kukabiliana na tatizo. Pia kuangalia na ukubwa wa tatizo lenyewe.
Hii sheria ukiisoma vizuri kwenye citation na interpretation yake utaona kwamba ilikuwa inawalenga kada fulani (Ma bwana afya) kwa maana hiyo haiwezi kuwa generally imposed kwenye kila sekta ya afya.

Hata hivyo na hii ni mojawapo ya utitiri wa sheria mbaya na kandamizi zinazotungwa kila asubuhi nchini Tanzania!
 
mm najiuliza, mbona serikali imetumia nguvu sana kukanusha na kumchulia hatua hyou mkrugenzi, kwana hakuna taratibu za kumuonya kiongz kama hyo, kuitna na kukosoana au hvyo vitu utawala huu hakuana?
Huu ni utawala wa traffic barabarani, ukipigwa mkono tu jua hilo bao!!
 
Alichosahau Pro. Mkumbo ni kuwa NIMR ni taasisi ya serikali na wala si taasisi binafsi ya Dr. Mwele. Ingekuwa ni taasisi binafsi ya Dr. Mwele basi ingekuwa sahihi kwake kutangaza matokeo ya tafiti bila kumshirikisha mtu yoyote, ila kwa sababu NIMR ni chombo cha serikali basi hana budi kufuata taratibu zilizowekwa na mwenye taasisi. Huwezi kutangaza tafiti hasa ya suala nyeti kama Zika bila kuwahusisha walio juu yake. Ishu ya zika si suala la ugonjwa tu ila linaathiri mambo mengi including natioanal security. Sasa unapokurupuka tu kama mkurugenzi kutangaza eti kisa wewe ni scientist wakati upo kwenye taasisi yenye mamlaka ya kufanya tafiti na kuishauri serikali unategemea nini kama sio kufukuzwa kwenye taasisi husika?
Mbona huwa wanatangaza tafiti zote wanazofanya tangia kuundwa kwake NIMR?!

Halafu mimi siamini kama zika ni tishio kuliko malaria kuliko kipindupindu kuliko hepatitis, sababu ya kuipa headline kubwa kiasi cha kugharimu kibarua cha mtu siioni kabisa!
 
lakini mwisho wa siku serikali imekanusha uwepo wa huo ugonjwa hapa nchini, je huo utafiti ulikuwa ni batili? na kama ni batili ni nini hatma ya hizi taasisi ambazo zinatoa utafiti batili?
na kama huo utafiti upo sahihi je serikali inatuweka rehani sisi wananchi wake kwa kuficha uwepo wa ugonjwa hapa TZ..

[HASHTAG]#thinkingoutloud[/HASHTAG] 😵😵😵
Na kwa kuongezea NIMR imefanya utafiti, je na serikali nayo imefanya utafiti??
 
Uzalendo ni kuongea uongo au kuongea ukweli ili kuweka mazingira mazuri ya kuweza kujilinda dhidi ya hatari inayoweza kutokana na ili jambo.
..Hivi kati ya Dr.Mwele na Magufuli nani mzalendo ? Vipi huyu aliyesema waliokutwa wamekufa mto Ruvu ni wahamiaji haramu ....unadhani nchi nyingine wanalichukuliaje
Huyo alifanya utafiti unaotakiwa na sirikali teh teh teh!
 
Remember also that a professorship is not just a post but a measurement smartness in anything especially in his official language of communication.
As you can see that even your grammar do not support your argument!
 
Kwa hali hii wasomi wengi watakwenda kufanyakazi nje ya Tanzania.
Ukimwadhibu msomi mmoja kwa ubabaishaji unawatia hofu wasomi waliopo nje na ndani hivyo kupata maendeleo itakuwa ngumu kweli kwa sababu tutakuwa tunaongozwa na mihemko ya kisiasa.
 
Nchi za kimasikini tuna magonjwa sana ndio maana babu wa Loliondo alipojitokeza tuu alipiga hela sana tunapenda kuficha ukweli wa ugonjwa ili iweje sasa..Nchi masikini fikra za kimasikini tuu..
Na ajabu hakuhojiwa juu ya utafiti wake bali watu akiwemo mukulu walienda kupiga kikombe na hela wakatoa!
 
Ebu SOMENI hili andiko Mwana JF mmoja kaandika na Prof.asome pia.

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.
Word
 
Kitila Mkumbo nazani hajaona athari la ili tangazo, mfano mimi nilikua na Mpango na my wife wangu mwezi ujao abebe mimba ila baada ya tangazo la Zika lilitustua, tukasema tusitishe ishu ya kubeba mimba, sasa watanzania wangapi wameathiliwa na ili
hahaha kwa hiyo dr mwele atasababisha viwanda vya kufyatulia watoto usitisha uzalishaji?
 
Amechemka nini mkuu?!
Kutuambia Zika ipo nchini kwetu???!

Kama ni kwa muktadha wa kunyamazishwa (kama jaribio la kutushona midomo kupitia MAXENCE MELO linavyoratibiwa) nitakuelewa, lakini kuujua ukweli ni haki yetu tena ni ya msingi kikatiba, hizo taratibu nashauri zipelekwe chato kwenye uwanja mpya wa ndege
Hapa namuunga mkono Magu,Mwele kachemka
 
Dr Mwere Malecela alisema Tanzania kuna wagonjwa wa zika au kuna kirusi cha zika? Mkipata jibu hilo, mtaacha kuendelea kumshambulia mama huyu.
 
tumechezewa kiakili,kiuchumi,kielimu na kisiasa.....[emoji45] [emoji45] ....sasa tunakwenda kuchezewa na suala la afya zetu.....[emoji45] [emoji45] .....kwa hilo hapana jamani.....
 
Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
Prof. Mkumbo anataka kutwambia yeye anaweza kuongea lolote linalohusu idara yake pale chuoni bila uongozi wa Chuo kujulishwa!

Ninavyojua hata ukitaka kupresent paper yako kwa academicians wenzako lazima uongozi wa idara, kitivo, shule au chuo ujulishwe.

Sasa kwenye suala kubwa kama hili ndio wasihusishwe? Naanza kuelewa kwanini ni mbaya kwa wasomi kufanya siasa!
 
TFDA waliwah kutangaza mafuta ya mbegu za ubuyu yana madhara bila hata kuishirikisha WHO wala wizara ya afya

Shangaa sasa.

TFDA ni Foood and Drugs AUTHORITY ya Nchi. NIMR ni Research Institute ya NCHI. Hawa wameaminiwa na kupewa mamlaka ya kutafiti ili walinde afya zetu. Sasa hatutaki kuwasikiliza NIMR na tunataka porojo za politicians na WHO wa hapa TZ ambao hawana hata test tube ofisini kwao pale.

Zile research findings tayari zipo published. Ningewaelewa kama labda Dr. Mwele "angeonywa" kama ni kweli hakumpa heads-up Waziri wa Afya lakini si kumuondoa kwenye nafasi yake kwa style ile
 
1482038731165.jpg
 
Nadhan mamlaka ya Rais inapewa taarifa/ushauri ambao haupo sahihi mpaka Mkulu anaonekana kama maamuzi yake ni ya kutokutafakari kwanza.......Nawachukia sana washauri wa aina hii kwani huleta chuki wakati wao wapo pembeni......!!!!! Ushauri, Mkulu tafuta washauri Binafsi wakushauri Pia.......
 
Back
Top Bottom