Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Hii kamata kamata ya mama Samia dhidi ya wanahoji na kupinga mkataba mbovu baina ya Tanzania na DP World inaonesha ni mkakati B wa kuzima hoja hiyo.
Wasomi binafsi wa Cuba tulielewa sana matukio yaliyojiri hivi karibuni ambapo jamii iligoma kuhamishwa kutoka kwenye hoja hii yenye utata mkubwa.
Kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude Nyangali na hatimaye jana kukamatwa kwa Dr. W Slaa ambao kwa uwazi upfront wameonesha msimamo wao kupinga namna mkataba huu ulivyoingiwa. Hususani wanapinga hadidu za mkataba ambazo hazitoi unafuu kwa Tanzania huku ikimmilikisha mwekezaji eneo letu la nchi milele jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 28(3) inayokataza siyo tu kusalimisha sehemu au nchi kwa mshindi wa vita bali inakataza mkataba wowote wa kutoa kipande cha nchi kwa nchi, kikundi ama taifa lolote kwa namna ama taathira za kimkataba
Uwezekano mkubwa wa kamatakamata inqyoendelea kuwa imewakumba wengi. Na kwa kuwa wengi siyo maarufu, kwa namna vyombo vyetu vya dola vilivyo na upungufu wa utu na haki za binadamu inawezekana kuna ambao wamepaishwa mawinguni na ushahidi ukafunikwa. Zipo ripoti nyingi za watu waliopotea kwenye mikono ya vyombo vya dola huku serikali ikitulia tuli bila kuchukua hatua.
Nimejiuliza hapa kwa sauti. Je Prof Tibaijuka naye atajumuishwa miongoni mwa matishio ya utawala wa awamu ya 6 au she will be spared lakini akioneshwa tanuru wanalopitia wazalendo wenzake?