Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,896
- 3,206
Habari wana JamiiForums.
Rejea kichwa cha habari chahusika.
Lengo la kuandika uzi huu ni kutoa maoni yangu juu ya wanaopinga mkataba kati ya DPW na serikali yetu ya Tanzania.
Kwa maoni yangu, naona wale wanaopinga mkataba huu wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono.
Wale wanaopinga wanatoa hoja za msingi kabisa kama vile mkataba kutokuwa na ukomo, mkataba kujumisha bandari zote za Tanzania bara (zile za bahari na maziwa), mkataba kuweka chini ya usimamizi wa DPW njia zote za kimkakati wa kiuchumi, mkataba kuipendelea zaidi DPW kulinganisha na serikali, Mkataba kutoainisha kiasi gani tutapata kama nchi tukishaingia mkataba n.k.
Kwa upande wa wale wanaouunga mkono, wengi hawana hoja zaidi ya kuwapinga wale wanaoupinga na kuingiza masuala ya Uarabu na dini ya Kiislamu.
Naomba kuwasilisha.