Profesa Shivji na wafanyabiashara kwenye siasa nadhani hajavuta kumbukumbu zake vizuri

Mfanyabiashara hafai kuwa sehemu ya uendeshaji wa taasisi za serikali kwa mfumo wa Tanzania ni upenyo kuwapa nafuu ya gharama za biashara zao huku wananchi wa kawaida hakuna chochote wanachosaidia maana hajui shida zao na sio sehemu ya kusikiliza kero zao kwa upande mwingine wengine wao hawajawahi kuishi maisha ya shida na uhitaji hivyo sio rahisi kwao kufahamu kwa yakini ni kitu gani wanachokitaka lakini pia serikali inakuwa na usalama kiasi gani kwa rasirimali zake.

1. Mwananchi ndio mwajiri wa wanasiasa wote

2. Mwananchi dio mlaji mkubwa wa bidhaa za mfanyabiashara

3. Mwananchi ndio mhanga mkubwa wa kukwama kwa uchumi na maendeleo bianfsi

4. Mwananchi ndio uhai wa taifa lolote sio mwansiasa au mfanyabiashara
Unaweza kuwapa nafuu ya gharama za biashara zao lakini angalia masuala kwa upana wake. Mfanyabiashara anaingiza uzoefu wake kibiashara kwa maoni mapana na uzoefu wake.
Tusitazame kutazama kwake maslahi yake tutazame uhusika wake wa masuala nyeti na mtazamo wake wa kiutendaji.

Nimetoa mfano wa Erick Hamisi wa TPA jinsi anavyowahusisha wafanyabiashara kama wadau wake wa karibu namna anavyopokea maoni yao ya kikazi badala ya kuwaona kama maadui wenye kutakiwa kumnyenyekea yeye kama bosi anayepita tu kama upepo upitao.

Upeo wa Mohamed Dewji huwezi kuulinganisha na ule wa mbunge fulani wa kawaida tu asiye na uzoefu wala ushawishi mkubwa wa kimataifa hata kama anayo maslahi yake ya kibiashara.a
 
Wewe inavyoonesha ni mtumwa wa fikra na ubwanyenye
 
hata mm sijamwelewa naona kahama mada kabisa yaani katuondoa kwenye mstari.
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
 
Jitahidi kurudia kusoma ulichoandika ndipo utume jumbe zako
 
Huyu Prof.anaishi Kwa fikra za kizamani Sana, NI wale wanaoamini kuwa mtumishi wa UMMA lazima awe maskini ,ndio kigezo cha uzalenfo!
 
Kwani yeye Profesa wakati anatoa hoja yake, alikuwa anatumia kichwa chake tu au alikuwa anaangalia kanuni ambayo ipo siku zote kama guide ya kuwaongoza watumishi wa umma ili kuepusha mgongano wa maslahi kwenye kazi zao?

Mimi naona Profesa yuko sahihi ukizingatia kuwa mara zote ni muumini wa sera za Mwalimu Nyerere, Ujamaa na Kujitegemea. Hata hivyo, kwa sababu tulishaingia kwenye ubepari kimya kimya, wewe pia nawe uko sahihi.

Kwa hiyo nachelea kusema kuwa wote mko sahihi, Profesa yuko sahihi na wewe pia uko sahihi.
Sijui kama hoja yangu nimeitoa kwa-usahihi kwa sababu mimi ni layman perce kwenye haya mambo ya Political science
Unyerere ndio urithi mbovu kuwahi kutokea. Siku urithi huu ukitoka kwa vichwa vya watanzanja itaja kuwa nchi bora sana
 
Kwenye hii bodi kakosekana Rugemalila wa pitieli ili team ikamilike tayari kwa kuupiga mwingi. Huyu angesaidiia kutoa ushauri jadidu kwa Tanesco juu ya njia za kupambana na tatizo la umeme inapotokea ukame ama maji kufunguliwa kwenye mabwawa na kupungua kushindwa kuzalisha umeme.
Kama zile nafasi za kuteua wabunge bado zipo, amteue Karamagi na kumpa nafasi kwenye cabinet.

Atamsaidia sana kwenye masuala ya nishati.
 
Si hilo tu, zimeanza kupigwa chapuo za kuibinafsisha TANESCO.

..binafsi napinga ubinafsishaji wa Tanesco.

..lakini kwa upande mwingine performance mbaya ya waliokabidhiwa kuendesha Tanesco ndio inayowapa kauli wanaotaka kuibinafsisha.

..Tumebadili Maraisi, mawaziri wa nishati, ma-dg wa shirika, lakini matatizo ya Tanesco yako palepale. Wote wameshindwa kui-fix Tanesco.

..Binafsi sina amani [ peace of mind ] na management na bodi iliyoletwa Tanesco.
 
Unaweza kuwapa nafuu ya gharama za biashara zao lakini angalia masuala kwa upana wake. Mfanyabiashara anaingiza uzoefu wake kibiashara kwa maoni mapana na uzoefu wake.
Tusitazame kutazama kwake maslahi yake tutazame uhusika wake wa masuala nyeti na mtazamo wake wa kiutendaji.

Nimetoa mfano wa Erick Hamisi wa TPA jinsi anavyowahusisha wafanyabiashara kama wadau wake wa karibu namna anavyopokea maoni yao ya kikazi badala ya kuwaona kama maadui wenye kutakiwa kumnyenyekea yeye kama bosi anayepita tu kama upepo upitao.

Upeo wa Mohamed Dewji huwezi kuulinganisha na ule wa mbunge fulani wa kawaida tu asiye na uzoefu wala ushawishi mkubwa wa kimataifa hata kama anayo maslahi yake ya kibiashara.a

..Nadhani tatizo ni rekodi za walioteuliwa huko Tanesco.

..Wangeteuliwa watu wapya, wenye sifa nzuri machoni mwa jamii, kusingekuwa na lawama unazozisikia.

..Nadhani wengi waliopinga hawataki kuona wateule wa awamu ya 4 wakirudishwa ktk utumishi kwani Magufuli aliwaondoa kwasababu ya ku-underperfom na maadili mabaya.

..Rais SSH alitakiwa kuibua watu wapya, wasafi, na mahiri, kutoka sekta binafsi na kuwaingiza kimkakati ktk mashirika ya umma.
 
Hao aliowaleta JPM na wao wakawa ni wapigaji kwa namna moja au nyingine. Tatizo hakuna msafi hata mmoja. Wanapoteuliwa kwa mara ya kwanza wananukia harufu ya usafi wakishakaa miezi sita au mwaka wanakuwa wamejifunza wizi na ufisadi.
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Uelewa shida "Mgongano wa Kimaslahi"
 
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
Kongole kwa kutoa elimu fupi lakini yenye kueleweka
 
Mkuu ukikiweka kila kitu ndani ya uzi utatumia siku nzima na bado hutamaliza. Kumbuka kuchukuwa muhtasari tu kila unaposoma.

Prof Shivji ni mjamaa kama wajamaa wengine wote. Ni mtu mwenye kutilia shaka ile hulka ya kuwaamini wafanyabiashara.
Issue hapa ni neno dogo lakini linahitaji uelewaaaaaa

Sio paragraph baada ya paragraph za kutokuelewaaa unacho andika ni nini.
 
Hizo paragraph zina maana kwa wenye uelewa mpana kuliko wewe. Mtihani ni ule ule na wote wanafundishwa na mwalimu mmoja, mmoja anapata alama tisini na mwingine arobaini.
 
Kama zile nafasi za kuteua wabunge bado zipo, amteue Karamagi na kumpa nafasi kwenye cabinet.

Atamsaidia sana kwenye masuala ya nishati.

Mh Karamagi nilimsahau naye atasaidia kutoa ushauri mzuri sana kama ule wa kubinafsishwa ticts. Nchi hii ina hazina kubwa ya viongozi wanao wajali wananchi wake. Waheshimiwa washindwe wenyewe kuwatumia kuwapa ushauri. Jaribu kufikiria mfanyabiashara Singasinga Habindra alivyotoa ushauri mzuri kuhusu fedha za Escrow. Uchumi usipopaa itakuwa ni kujitakia wenyewe.
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Profresa Shivji ni mnafiki
 
Back
Top Bottom