Profesa Shivji na wafanyabiashara kwenye siasa nadhani hajavuta kumbukumbu zake vizuri

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
 
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
 
Conflict of interest ni sehemu tu ya ufanisi mzima wa mfanyabiashara anapopewa nafasi. Tunahitaji ubunifu mkuu, ni wa muhimu sana.
 
Kwani yeye Profesa wakati anatoa hoja yake, alikuwa anatumia kichwa chake tu au alikuwa anaangalia kanuni ambayo ipo siku zote kama guide ya kuwaongoza watumishi wa umma ili kuepusha mgongano wa maslahi kwenye kazi zao?

Mimi naona Profesa yuko sahihi ukizingatia kuwa mara zote ni muumini wa sera za Mwalimu Nyerere, Ujamaa na Kujitegemea. Hata hivyo, kwa sababu tulishaingia kwenye ubepari kimya kimya, wewe pia nawe uko sahihi.

Kwa hiyo nachelea kusema kuwa wote mko sahihi, Profesa yuko sahihi na wewe pia uko sahihi.
Sijui kama hoja yangu nimeitoa kwa-usahihi kwa sababu mimi ni layman perce kwenye haya mambo ya Political science
 
Hata Aikael ni mfanyabiashara mkubwa tu lakini ni kiongozi wa kisiasa TZ!! Hii mambo ya kuyatenga makundi flani flani kwenye jamii yasipewe nafasi za uongozi ni ya kizamani
 
Mifumo yetu ni dhaifu Sana likitokea suala la conflict of interest tumeliwa huwezi linganisha na nchi za wenzetu ambako unaingia madarakani unakuta utaratibu na ukitaka kufanya vinginevyo utalazimika kuhusisha jopo la wataalamu mwisho utasanda lakini hapa kwetu mtu mmoja anaweza amua hata kuifuta tanesco na akajimilikisha kupitia kampuni yake ambayo ni hewa na akabadili kuanzia uongozi gharama za unit na bado akaendelea kushangiliwa.
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Kwa uchambuzi wako huu nachelea kusema kwamba wewe ni mmojawapo wa vijana wa hovyo kabisa katika kuchambua mada kwa uweledi.
Mifano yako yote ya hao wafanyabiashara umeitoa kwa wao kuwa wabunge. Bunge sio taasisi ya uma, ni muhimili katika serikal. Bila aibu umesema hao wabunge msaada wao walikuwa wanaongea bungeni. What! Shame on you bro.. kuongelea shida za wananchi bungeni ndo msaada? Msaada ni vitendo. Alaf hatuzungumzz ushawshi wa mfabiashara tunazungumzia mfanyabiashara kuongoza taasis ya uma. Hapo ndipo prof.shivji alichokiongelea..ushawsh wa wafanyabiashara hauepukk..lakin sio mfanya biashara kuwa mmoja wa watoa maamuz katika sekta ya uma.
Kwa kifupi tu, kwenye tanesco tumeliwaa..na manyoya yashaanza kuonekana.
Shame to all of us..
 
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
Kwa kwel elimu inahutajika miongoni mwa watz wengi sana. Sasa kama huyuu kijana alichokiongeleaa yaan had nachokaa kwa kwel
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Mfanyabiashara hafai kuwa sehemu ya uendeshaji wa taasisi za serikali kwa mfumo wa Tanzania ni upenyo kuwapa nafuu ya gharama za biashara zao huku wananchi wa kawaida hakuna chochote wanachosaidia maana hajui shida zao na sio sehemu ya kusikiliza kero zao kwa upande mwingine wengine wao hawajawahi kuishi maisha ya shida na uhitaji hivyo sio rahisi kwao kufahamu kwa yakini ni kitu gani wanachokitaka lakini pia serikali inakuwa na usalama kiasi gani kwa rasirimali zake.

1. Mwananchi ndio mwajiri wa wanasiasa wote

2. Mwananchi dio mlaji mkubwa wa bidhaa za mfanyabiashara

3. Mwananchi ndio mhanga mkubwa wa kukwama kwa uchumi na maendeleo bianfsi

4. Mwananchi ndio uhai wa taifa lolote sio mwansiasa au mfanyabiashara
 
Hii debate ya wafanyabiashara kuingia kwenye bodi za mashirika ya umma ni debate ya kijinga sana.

Angeitoa mtu mwingine yeyote asiye na label ya uanazuoni kama alivyo Shivji ingepuuzwa fasta, lakini kwa vile imetoka kwa Prof. Shivji naona imepewa airtime kuliko inavyopaswa.

Hatuwezi kujenga nchi inayoamini kwamba maslahi ya wafanyabiashara ni tofauti na maslahi ya umma. Kwani wafanyabiashara wametoka mwezini? Si ni watanzania? Ni kitu gani kilichomo ndani ya sekta binafsi ambacho kikanuni kinapingana na maslahi ya umma? Ni watu gani wanaopaswa kufaidika na Tanesco imara na umeme wa uhakika zaidi ya wafanyabiashara aina za Bakhresa ambao kimsingi viwanda vyao vinahitaji umeme cheap usiokatikakatika?

Ni hivi, hii nchi imechelewa sana katika kuwapa nafasi wafanyabiashara na matajiri nafasi za maamuzi ya kisera katika mashirika mbalimbali ya serikali. Tumekuwa tukiwapa maskini hizo fursa matokeo yake maskini hao wanatumia hizo fursa kujitajirisha kwanza kupitia hizo taasisi za serikali.

Kimsingi hata halmashauri zetu za kata huku chini zilipaswa kuwa populated na madiwani na wafanya maamuzi matajiri au wanaojiweza kwa kiasi fulani. Tumewajaza madiwani choka na maskini maskini, wanachokiweza ni kupiga maneno tu na kufanya michongo ya kupiga pesa hata ya kujenga barabara za mitaani. Watu matajiri wameshahama kwenye umaskini wa dizaini hiyo.
 
Kwenye hii bodi kakosekana Rugemalila wa pitieli ili team ikamilike tayari kwa kuupiga mwingi. Huyu angesaidiia kutoa ushauri jadidu kwa Tanesco juu ya njia za kupambana na tatizo la umeme inapotokea ukame ama maji kufunguliwa kwenye mabwawa na kupungua kushindwa kuzalisha umeme.
 
Conflict of interest ni sehemu tu ya ufanisi mzima wa mfanyabiashara anapopewa nafasi. Tunahitaji ubunifu mkuu, ni wa muhimu sana.
Ninashawishika kuamini kuwa wewe hujui kitu inagwa unajua kusoma na kuandika. Unatakiwa kuelewa na kisha kuchambua dhana ya mgogoro wa kimaslahi ambayo ndio hoja ya Profesa Emeriti Issa G Shivji.
 
Kwa uchambuzi wako huu nachelea kusema kwamba wewe ni mmojawapo wa vijana wa hovyo kabisa katika kuchambua mada kwa uweledi.
Mifano yako yote ya hao wafanyabiashara umeitoa kwa wao kuwa wabunge. Bunge sio taasisi ya uma, ni muhimili katika serikal. Bila aibu umesema hao wabunge msaada wao walikuwa wanaongea bungeni. What! Shame on you bro.. kuongelea shida za wananchi bungeni ndo msaada? Msaada ni vitendo. Alaf hatuzungumzz ushawshi wa mfabiashara tunazungumzia mfanyabiashara kuongoza taasis ya uma. Hapo ndipo prof.shivji alichokiongelea..ushawsh wa wafanyabiashara hauepukk..lakin sio mfanya biashara kuwa mmoja wa watoa maamuz katika sekta ya uma.
Kwa kifupi tu, kwenye tanesco tumeliwaa..na manyoya yashaanza kuonekana.
Shame to all of us..
Mkuu ukikiweka kila kitu ndani ya uzi utatumia siku nzima na bado hutamaliza. Kumbuka kuchukuwa muhtasari tu kila unaposoma.

Prof Shivji ni mjamaa kama wajamaa wengine wote. Ni mtu mwenye kutilia shaka ile hulka ya kuwaamini wafanyabiashara.
 
Ninashawishika kuamini kuwa wewe hujui kitu inagwa unajua kusoma na kuandika. Unatakiwa kuelewa na kisha kuchambua dhana ya mgogoro wa kimaslahi ambayo ndio hoja ya Profesa Emeriti Issa G Shivji.
Asante sana wewe mjuaji zaidi yangu. Kusahihishwa ni kujua tena na tena na huo ni mzunguko wa maisha. Mfanyabiashara na maslahi yake hakwepeki na ni sehemu tu ya mamia ya wabunge wanaokuwepo mle bungeni.

Hizi dhana za kuamini katika ujamaa peke yake ndio zinazokwamisha baadhi ya taasisi zenye kuhitaji maono yasiyopatikana kirahisi tu.
 
Kwani yeye Profesa wakati anatoa hoja yake, alikuwa anatumia kichwa chake tu au alikuwa anaangalia kanuni ambayo ipo siku zote kama guide ya kuwaongoza watumishi wa umma ili kuepusha mgongano wa maslahi kwenye kazi zao?

Mimi naona Profesa yuko sahihi ukizingatia kuwa mara zote ni muumini wa sera za Mwalimu Nyerere, Ujamaa na Kujitegemea. Hata hivyo, kwa sababu tulishaingia kwenye ubepari kimya kimya, wewe pia nawe uko sahihi.

Kwa hiyo nachelea kusema kuwa wote mko sahihi, Profesa yuko sahihi na wewe pia uko sahihi.
Sijui kama hoja yangu nimeitoa kwa-usahihi kwa sababu mimi ni layman perce kwenye haya mambo ya Political science
Kwa mantiki hiyo inabidi mwenye nguvu ndio apishwe maana wote wako sahihi na yote yanawezekana.
 
Back
Top Bottom