Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Kila Taifa, kuna matukio fulani ambayo ni mabaya sana au mazuri sana, huwekwa kwenye kumbukumbu. Na kutokana na kumbukumbu hizo, hata wataalam mbalimbali, wa nyakati mbalimbali, hufanya tafiti kuhusiana na matukio hayo.
Fikiria uchaguzi wa mwaka 2020:
1) Robo tatu ya wagombea wote wa ubunge kupitia CCM ambao walipitishwa na wajumbe kuwa wagombea kupitia CCM, majina yao yalikatwa na kuwekwa watu wengine. Watu watatu tu, yaani marehemu (Mungu kwa huruma yake tunamwomba amsamehe kote alikokosea), Bashiru na Polepole walifanya kazi hiyo. Rejea tukio hilo, hakuna mtu yeyote ndani ya CCM aliyeweza kupinga au hata kukemea. Jambo kama hilo katika jamii ya watu wenye akili timamu na utashi, lisingewezekana. Tukio hili ni la pekee na la ajabu.
2) Hao, robo tatu ya wagombea walioteuliwa na watu watatu tu, walifanywa kuwa wabunge bila ya kujaliwa wamechaguliwa, wamepigiwa kura au hawakupigiwa kura hata moja. Tukio hilo la ajabu lilifanyika, wanaCCM na Watanzania zaidi ya milioni 60, walikaa kimya. Hili siyo jambo la kawaida. Na kamwe kwenye jamii yenye watu wenye ubinadamu uliokamilika, haliwezi kufanyika, kwetu lilifanyika.
3) Asilimia 95% ya wagombea wote kupitia vyama vya upinzani, majina yao yalikatwa na Mahela. Na hao 5% waliobakia, huko kwenye uchaguzi, wakurugenzi wa Halmashauri waliamua nani apewe kura kiasi gani ili asitangazwe kuwa mbunge. Hilo lilifanyika, na wananchi wote zaidi ya milioni 60, walikaa kimya! Haya ni miongoni ya maajabu makuu ya Dunia.
4) katiba ya nchi inasema Waziri Mkuu, ni lazima awe miongoni mwa wabunge walioupata ubunge kwa kupigiwa kura. Majaliwa hakupata hata kura moja ya mwananchi, akatangazwa ni Waziri Mkuu. Kwa kushirikiana na Rais wakawateua wenzao wengine kwenye hilo genge la wahuni kuwa mawaziri, wakashika na misahafu, wakaapishwa. Majaliwa mtu asiye na kura hata moja akawa waziri mkuu. Na mahakama ikaja kutoa ufafanuzi kuwa kwenye katiba yetu kuna aina mbili tu za wabunge: wabunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa, hao wanaoitwa wabumge wa kupita bila kuoingwa ni si wabunge. Lakini Majaliwa na waovu wenzie hawakuachia nafasi waluzojipachika, wala wananchi zaidi ya milioni 60, hawakuwafanya lolote. Haya siyo mambo ya kawaida kwa wanaadamu.
Tukio la Tanzania kuongozwa na Serikali batili na Bunge batili, halafu wananchi wakakaa kimya, siyo kitu kidogo. Huko mbeleni, fikiria hata miaka 1,000 ijayo, ambapo sisi sote tuliopo leo, hatutakuwepo, yawezekana watu wa nyakati hizo kutoka mataifa mbalimbali, wakataka kufanya utafiti wa kitaalam kuhusiana na jambo hili. Kama vile kutaka kujua:
1) Iliwezekana vipi watu zaidi ya milioni 60 kuongozwa na Waziri mkuu batili na mawaziri batili, na hivyo Serikali batili, na watu wakawa wametulia, wakipokea mari na maelekezo kutoka kwa waovu.
2) Watataka kujua kulikuwa na mazingira ya namna gani, labda yalisaidia kufifisha uwezo wa akili za watu wa wakati huo.
3) Watataka kujua kama hao wanaoitwa ni watu zaidi ya milioni 60 kama walikuwa ni binadamu kweli au walikuwa ni viumbe vilivyofanana na wanadamu katika maumbile, lakini siyo kwenye utashi. Ifahamike kuwa wakati huo, yumkini jambo hilo halitawezekana kabisa kutokea, na pengine ardhi ya Tanzania itakuwa inakaliwa na mchanganyiko.mkubwa wa wanadamu.
NB:
Ni vema kumbukumbu zetu zikawekwa vizuri kabisa ili watafiti wa wakati huo wasipate shida, (kama inavyotokea sasa katika kutambua mambo kadhaa ya historia ya Wapalestina na Wayahudi).
1) Napendekeza IQ na DNA za viongozi wote, hasa wa Serikali na CCM, wapimwe. Ili nyakati hizo zijazo, ziweze kufananishwa na watu wa wakati huo, lakini pia zinaweza kulinganishwa na za watu wa nyakati hizi tuishizo kutoka mataifa yasiyo na mambo ya ovyo ovyo kama kama haya ya kwetu.