Profesa Shivji na wafanyabiashara kwenye siasa nadhani hajavuta kumbukumbu zake vizuri

..lakini kwa upande mwingine performance mbaya ya waliokabidhiwa kuendesha Tanesco ndio inayowapa kauli wanaotaka kuibinafsisha.
Tatizo ni ubinafsishaji kama ule wa NBC ambao hautakuwa na manufaa yoyote kwa taifa.
 
Je, Prof Shivji anaweza kutupatia option ya kuendeleza Tanesco?
Objective criticism or views need options??

Prof Shivji ni mwanasheria labda wamtumie kwenye kesi za Tanesco. Ninavyo jua Tanesco wako na wanasheria wazuri mfano Mh Mkono enzi hizo na hii timu ya bodi imelishughulikia hilo. Sio rahisi kuishinda Tanesco kwenye kesi watakuwa wanashinda mashauri yao na kulipwa fidia nyingi zitakazo mnufaisha mlengwa ambaye ni mwananchi.
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Unapotosha. Profesa shivji hajakosa imani na sekta binafsi ila na wafanya biashara wakubwa kwenye nafasi za juu za uongozi kama vile executive yaani uwaziri na uongozi wa mashirika makubwa ya umma.
Kwenye uwakilishi tu wabunge wafanyabiashara wakubwa wamekua hawaaminiki kwa shida ya conlict of interest.
Ukweli mama anachukua njia isiyo na maslahi ya umma. Hii sio njia ya magufuli.
 
Siku zote maskini muonyeshe kuwa nia yako ni njema, ukishafanya hivyo umemaliza kazi. Huo ni ujanja wa Nyerere, Mwinyi na wengi wa afrika hii. Kwamba ulikuwa na nia fulani nzuri tu lakini utimizaji wako ni tatizo na wao watakusamehe tu kwani nia yako ilikuwa ni njema tangu mwanzo.

Kibaya zaidi Mama hana uwezo wa mawasiliano yanayompa ukaribu na mwananchi, hana zile sarakasi wala sanaa za kila siku zinazomuweka karibu na moyo wa mnyonge. Anaweza kufanya mengi na makubwa lakini akawa sio maarufu kama mtu maalum wa wanyonge.
 
Sikujua kama huyo philipo ni bwege kiasi hicho. Wanasiasa anaotuhadithia si ndio hao waliotulisha mchele mbovu na kuuondoa uhai wa mkemia mkuu?!
Nimekusoma kiumbe mwenye akili nyingi. Unakuja na siasa za kulishana mchele mbovu za miaka karibu 25 iliyopita. Wewe umekariri maisha.
 
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
+Njia nzima imejaa conflict of interest. Ndio maana tunazalisha kashfa nyingi za rushwa kwa sababu tunadharau hii issue ya conflict of interest
 
Nimekusoma kiumbe mwenye akili nyingi. Unakuja na siasa za kulishana mchele mbovu za miaka karibu 25 iliyopita. Wewe umekariri maisha.
A conflict of interest in business normally refers to a situation in which an individual's personal interests conflict with the professional interests owed to their employer or the company in which they are invested.

Conflict of Interest. A conflict of interest exists when a volunteer leader has a direct or indirect business, professional, or personal interest or relationship that might influence, or might be perceived to influence, the judgment or actions of the leader when serving the Association.
 
Unamzungumzia Mzindakaya aliyepora ardhi ya wananchi na kuohodhi pasipo kuiendeleza huku walala hoi wakikosa sehemu za kulima? Mleta uzi aliyekutuma kazi hii, ungemwomba akupe data za ukweli.
 
Umebugi mleta maada wewe na Makamba kichwani bado vidampa sana, kwenye infant states kama TZ maswala ya conflict of interests yanapuuzwa sana. Na hii ni taa ya wazi kwa makamba urais asahau kbsa hata uwaziri mkuu ni never never. Ndio basi tena kalivaa tego la usinga. Chilo chiswano watu wa January
 
Amesikika Profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar Issa Shivji akiongelea namna wafanyabiashara wakishakuwa wametajirika wanavyovyamia masuala ya kisiasa na kitaalam. Labda ni baada ya kusoma majina ya wale wajumbe wa bodi ya TANESCO ndio akajenga hoja alizozijenga. Kwamba wafanyabiashara wenye akili za kibiashara ni ngumu kuwa na ufanisi wenye kujikita katika kutatua matatizo ya walio wengi pasipo kutanguliza nia zake za kisiasa.

Anaweza kuwa na hoja lakini naziona zimejikita katika kutaka kumpaisha yeye Shivji kama yeye lakini sizioni zikiwa zikitazama mbali. Ni hoja nyepesi kama tukiamua kuiangalia historia ya wabunge ambao ni wafanyabiashara na hata kuingia kwao bungeni hakukuondoa ule ukweli kwamba wao ni watu wa sekta binafsi.

Ipo mifano mingi ya wafanyabiashara na namna walivyokuwa ni sehemu ya utungaji wa sera na sehemu ya utatuzi wa matatizo sugu ya wananchi. Mifano ni mingi, miaka ile ya 1990 alikuwepo hayati Abbas Gulamali, aliyeanzia Yanga kama mdhamini halafu akaingia bungeni akiwa mbunge wa jimbo moja la Morogoro.

Hayati Gulamali aliweza kuchanganya siasa na maslahi yake mapana ya biashara pasipo kuharibu upande wowote kati ya hizo mbili. RIP Gulamali alikuwa ni mmoja wa matajiri wa kwanza kabisa kusimama na kutetea wakazi wa Morogoro akiwa Bungeni, wala usingeweza kuutambua ule ufanyabiashara wake wa kiwango cha juu aliokuwa nao kipindi kile.

Mzee Mzindakaya ni mfano mwingine ya namna ujasiriamali unavyoweza kuchanganywa na masuala ya kisiasa, huyu amekuwa mbunge kwa miongo kama minne na zaidi kidogo. Ni mkulima mkubwa na wakati huo huo ni mtunga seramahiri, mwenye kuchanganya vyema masuala hayo mawili.

Mohamed Dewji ni mfano mwingin wa tajiri anavyoweza kuwa mwanasiasa hapa Tanzania. Alianzia michezoni akaenda siasani na baadae amerudi michezoni. Na akiwa siasani aliweza kuchagiza maendeleo makubwa ya jimbo lake la Singida. Mohamed ni mmoja wa wajasiriamali wenye uchungu na maisha ya kawaida ya mtanzania. Misaada yote aliyoitoa jimboni kwake haina nia za kulikuza jina lake mwenyewe zaidi ya kuukuza ubinadamu wa wapiga kura wake.

Mwingine ni Shabiby wa Morogoro. Tajiri huyu akisimama bungeni anachokiongelea kina uhusiano na utetezi wa moja kwa moja wa shida za wakazi wa Morogoro. Ni mpaka uambiwe kuwa huyu mzungumzaji wa sasa ni mmiliki wa mabasi mengi na ni mjasiriamali mkubwa wa mkoa wa Morogoro.

Kuamini kwamba mfanyabiashara ni mtu wa kumhisi vibaya haswa pale anapokuwa na maslahi kwenye taasisi za kisiasa ni imani potofu.Ni mtazamo wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwamba ubepari ni unyama. Profes Shivji akiwa ni mfuasi kindakindaki wa Mwalimu Nyerere anaweza kueleweka akiwa na mitazamo ya kutowaamini wafanyabiashara.

Lakini dunia ya sasa ambayo kuna wale wasemaji wenye kuwapa moyo wananchi (Motivational Speakers) huwezi kuukwepa ushawishi wa tajiri kwenye siasa. Dunia hii ya mtu kuanza maisha kama muuzaji wa bidhaa za kutembeza karibu na taa za magari mijini na mpaka kufika hatua ya kusimama kama mjasiriamali mkubwa, huwezi kuukwepa ushawishi wake wala simulizi nzito zenye kutia moyo.

Tujaribu kutazama kile chanya kinachoweza kuwa ni mchango wa tajiri anapopewa nafasi ndani ya taasisi nyeti za kiserikali kuliko kutanguliza kwanza ile hofu ya yeye kuweza kuitumia vibaya taasisi hiyo kwa masuala ya kibinafsi. Tajiri siku zote tunamuona kama ni mwizi kwanza kabla ya kuwa tajiri, tunamuona ni mtu siye wa kumuamini kwanza kwa ubinadamu wake na uzoefu wake wa kibiashara. Hizi dhana za kijamaa zinatunyima mengi na zinaendelea kutokosesha ule uhuru wa kiushindani wenye kuanzia kichwani kwanza kabla ya kushuka kwenye matendo yetu.

Marekani ni utajiri wao wote walishindwa kuukwepa ushawishi wa Ross Perot miaka ile ya 1980, akiwa ni mfanyabiashara mkubwa aliyeutafuta na kuupata utajiri kwa nguvu zake mwenyewe. Na ni huko Marekani nchi ya dunia ya kwanza ambapo hatuwezi kuwa na Tanzania pasipo uwepo wa mahusiano hai ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa kweli Profesa Shivji amekosea kutokuwa na imani na sekta binafsi mpaka akaiwekea wasiwasi kichwani mwake. Waendeshaji wa bandari kubwa kubwa kama zile za Afrika ya kusini ni wafanyabiashara wa zamani waliofanikiwa, ndio wenye kuwekeza uzoefu wao wenye kuleta tija. Mfano wa karibu ni Erick Hamisi, Bosi wa TPA wa sasa ambaye msingi wake ni sekta ya benki namna anavyofanya mapinduzi pale bandarini tofauti na Kaka Kakoko aliyekosa uzoefu wa kibiashara na kiuchumi.

Profesa Shivji naamini kujifunza ni daima kwani elimu haina mwisho. Jaribu kusoma kwa kina ushawishi walionao wafanyabiashara kwenye sekta za umma na utajifunza mengi yenye umuhimu.
Dah...dugu yangu..naona haukumuelewa Prof..... Kwa kifupi uliingia chaka 🤭
 
Wafanyabiashara watapoozesha kasi ya ujenzi wa bwawa la Nyerere ili waweze kuikodisha majenereta serikali na wao kulipwa capacity charges.
Dah....yaleyale ya Nesi wa Kijiji kuolewa na muuza majeneza 🤣🤣🤣🤣🤣🤭
 
Yaan ndio maana Lowassa alisema,watanzania wanahitaji elimu!Elimu!!Elimu!!!Kimsingi Prof kaongelea conflict of interest. Kaongea kwa ufupi na kila MTU kaelewa kwa nn huyu mama hasitahiki kuwemo kwenye hiyo bodi.Lakin ndugu,inaonekana hukumwelewa kabisa Prof.Au hauelewi kabisa hiyo concept. Unahibuka na gazeti kubwa ,ambalo halieleweki unachoongea.
WEWE HUNA AU UNAONGEA TU?
 
A conflict of interest in business normally refers to a situation in which an individual's personal interests conflict with the professional interests owed to their employer or the company in which they are invested.

Conflict of Interest. A conflict of interest exists when a volunteer leader has a direct or indirect business, professional, or personal interest or relationship that might influence, or might be perceived to influence, the judgment or actions of the leader when serving the Association.
Tatizo hao wanaotembea nchi nzima kuomba kura wanashindwa kuwa na kundi jingine jipya kabisa la watu wanaowaamini walio kinyume na hao wenye conflict of Interest.

Na siku zote mtu anapopewa cheo kipya akapata connections humu humo ofisini kidogo kidogo hutengeneza mazingira ya conflict of interest. Hua haizaliwi kutoka kusikojulikana.

Ni sawa na wale madaktari wanaokua kwanza kikazi kwa mishahara kuongezeka na kukutana na watu mbalimbali ndio wanaoanzisha hizo conflict of interests.

Kwa hiyo hilo suala ipo tu, iwe kwa mwajiriwa kuja mgeni kabisa ofisini na kuzijenga taratibu iwe kwa mwajiriwa mzoefu, watu humu wanalalamikia mazoea ya hawa waajiriwa wapya wakisahau kuwa hizi conflict of interests ni matokeo ya watu kulindana na nidhamu ya uoga yenye kutengeneza makundi maofisini.
 
Umebugi mleta maada wewe na Makamba kichwani bado vidampa sana, kwenye infant states kama TZ maswala ya conflict of interests yanapuuzwa sana. Na hii ni taa ya wazi kwa makamba urais asahau kbsa hata uwaziri mkuu ni never never. Ndio basi tena kalivaa tego la usinga. Chilo chiswano watu wa January
Mkuu Gaucho naona ujuaji umekujaa.
 
Back
Top Bottom