Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Kwa mtu ambae kaishia darasa la Saba au form 4 atabeza matakwa ya vijana

Kwasisi watoto wa masikini ambao tulipitia vyuo kwa kuunga unga tunaelewa concern ya vijana wenzetu. Maisha ni magumu mno, ni vile tu hii nchi mtu akiwa kashiba hamkumbuki mwenye njaa. Hakuna kipindi mtu unakatia tamaa masomo, maisha na kujiona mfu Kama kipindi uko chuo huna uwezo wa kifamilia na hela yako ya boom hupewi wakati Kuna gharama za kila siku zinaendelea.

Kuna Stationary costs zipo kila siku. Bado kula , kufua nguo na accommodation (sehemu ya kuishi )

Napitia humu naona Kuna wachache sijui wametumwa wanajaribu kuleta siasa kwenye maisha ya watu

Njaa haina baunsa, kipindi hicho Mimi nilikuwa nimefikia hatua Bora nife kwa kudai haki yangu. So Ndalichako usichukulie poa jua unaongea na watu wenye njaa. Njaa inamuondolea mtu matumaini ya maisha

Tumieni Busara kulimaliza hili sote ni watanzania kwanini tutishane kwa vitu justifiable.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
peno hasegawa,
Rasi Mstaafu Kikwete alimchomoa NECTA baada ya kufanya madudu kwenye mitihani ya Somo la Islamic, watu wakatafsiri udini. Jiwe akabeba wote walioondolewa au walikosana na Mzee Kikwete kuonyesha utofauti

Ni mbaya mno kumfumba wanafunzi msomi kupractise Haki yao ya kikatiba. Tunaandaa Taifa la wanyonge wasioweza kudai haki zao kwa maslahi binafsi ya kutaka sifa kwamba unafanya kazi ili Hali Kuna uozo nyuma.
 
Poropesa Mimi sina digirii lakini uwezo wako wa kufikiria na kutatua haya sija elewa kabisa. Kama ili nalo ni somo basi nimefeli na nisingethubutu kutaka kujifunza maana sipo tayari kuelewa

Kuna shida katika elimu ya maporopesa...
 
Wale waliosoma kwa raha sana miaka ile, ndo hawakumbuki umuhimu wa kulipwa stahiki zote kabla ya masomo kuanza ndo mwanafunzi atulie asome, wamesahau kabisa!! Mtoto katoka Sumbawanga, kapewa pesa ya kula njiani labda 50k, baba anategemea mtoto akifika atalipwa pesa na kuanza masomo; mtoto anafika anakuta eti ndo mipango inaendelea ya malipo, je arudi nyumbani ndo aje baadaye, afunge kula na kulala hadi malipo yawe tayari, au afanyeje?

Mnaojitia kuitetea serikali na Prof. Ndalichako hamjui kwamba hiyo so called Bodi ndio chanzo cha matatizo! Wanazichezea pesa za wanafunzi halafu wanajitia kuwa wakali! Na kwa nini wanafunzi waitwe toka nyumbani, kama mambo hayajakaa sawa?

Halafu ona sasa hii communication breakdown; mwenye chuo anasema kama hujalipa hadi tarehe fulani, basi! Bodi ya Mikopo na Waziri wa Elimu wanajitia wako bize "wanakamilisha mambo"; je, meanwhile, mwanafunzi anapaswa kufanyaje?

Hebu kuweni na busara mtoe mawazo yenye maana ya kuwasaidia wanafunzi. Mnataka wafanyeje ndo mjue wana shida?

Ushauri wangu, bodi ifanye kazi usiku na mchana, mambo yote yawe sawa ndio wanafunzi waitwe kutoka nyumbani kuja kuanza vyuo; short of that, ni ujinga mtupu, ubinafsi na roho mbaya zimetawala!
 
Ilitakiwa hao wanafunzi wajue mbinu za kupambana na waliowashindwa na sio kuwatishia.. wamekariri migomo wasome na alama za nyakati hlf wajue namna ya kula nao sahani moja.. hiyo ni kwa faida yao na wanaelewa wamefata nini,mikopo ndio ni halali yao ila je,ili kuipata walitakiwa wafanye vipi..? Plan A imekuwa ngumu watafute plan B.
 
Naona vijana wa UDSM mmeamua kumiminika humu, ngojen Jiwe awafurahishe
 
KENZY, Wewe una uhakika hiyo plan A hawakuifanya au una uhakika gani kwamba hata B walikuwa hawajafika, sio kila kosa ni kosa, na sio kila sheria ni sheria
 
Wanafunzi kupewa mikopo yao kwa wakati ni muhimu sana, haya mmbo ya kuwafukuza na kuwatisha yanatakiwa kulaaniwa kwa nguvu zote. Halafu, hata kama wamekosea namna ya kudai wanatakiwa wasamehewe, ikumbukwe ni wanafunzi, maana yake wana mengi ya kujifunza!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KARLO MWILAPWA, Kauli gani imedhalilisha serikali? Vijana wanadai haki zao za msingi, by the way pesa yenyewe ni mkopo so watailipa huko baadaye
 
SONGOKA, Ndani ya mipaka ya Tanzania mwenye uwezo na mamlaka wa kutoa agizo kwa serikali ndani ya muda fulani liwe limefanyiwa kazi ni Katiba pekee yake, hata Rais anapewa mamlaka hayo na katiba
 
Back
Top Bottom