Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

REA Hiyo 1% nayo ni kubwa sana maana project za umeme vijijini wananchi nao uchangia huduma,wanatoa offer kwa watu wachache wengine wanachangia nguzo na meter ya Luku.

Ewura kuchukua 3% nayo ni kubwa yaani kupanga bei tu ndio tuwalipe 3%? Serikali kwa sasa inapata mapato mengi tunaomba impunguzie mzigo mwananchi.
 
Sio Hapo tu, waondoe kabisa service charge za kila mwezi, Ni bora watuuzie luku bei kubwa na isiwe na makato ya kila mwezi, mtu unatoa elfu 10 unapata unit 5? Hii kitu hatutaki kabisa

Service charge kuondolewa sii rahisi kwasababu service charge ni ghalama ambayo mteja anatakiwa kulipa pale mafundi wa tanesco watakuja kumtengenezea endapo akipata tatizo baada ya kuunganishiwa umeme. Mfano nguzo uliyoilipia wakati unaunganishiwa umeme kwa mara ya kwanza ikioza na ikaonesha inaweza leta madhara wao tanesco watakuja kukubadilishia bila malipo yeyote au mita yako ikihalibika hautalipia ghalama ya mita na ya kuwalipa mafundi wao watakija kukubadilishia bila ghalama yeyote. Mifano ya matengenezo ni mengi ambayo mteja unahitaji kufanyiwa baada ya kuunganishiwa umeme. Wao waliona haitakuwa rahisi kumchaji mteja pale atakapo pata tatizo wakaona waiweke kila unapo nunua umeme na mteja analipia mara moja tu kila mwezi haijalishi ametumia unit ngapi na iko fixed kwa wateja wa aina moja
 
Hivi unajua ni kiasi gani wanakata kila mwezi kwa hiyo service line?
Nina miaka 10 nyumba ya mzee wangu nimeweka umeme sijawahi kuwaita kwa service yyte ile na walivuta nguzo 6 mpaka kufika kwa mzee, sasa chaji waliyonikata miaka 10 italingana na gharama za nguzo zao hata kama nikitaka wabadili zote?
 
kama mi mteja mdogo nafikili ghalama yake mpaka saizi haitakuwazaidi ya 8.4 mils. Ukipata tatizo la loose na matatizo mengine mfano ikitokea leo nguzo hizo sita zimeungua na moto na ukaambiwa ili umeme wakuunganishie unatakiwa kulipa mil 2.4 ya nguzo mil 4.8 ya waya mil 2.1 ya vifaa ya kushika waya na kuzui usifike kwenye nguzo yaan insulator na mil 2.1 ya mafundi na ghalama ya mafuta utaweza kulipa leo? Jumla nikama zaidi ya mil10
 
Najua unachotetea, hivi inawezekana vp nguzo 6 zote ziuungue na waya zote zibadilishwe, sioni kipi unatetea hapa, muhimu service charge ni aina nyingine ya wizi ambao hatuutaki na tutaupigia kampeni mpaka uondolewe tu
 
Sitetei chochote lakini tambua ikitolewa kisiasa itarajie ufanisi wa kuwahudumia wateja kupungua labda watafute namna ya kuificha kwenye ghalama ya kila unit japo ufanisi bado sio mzuri sana
 
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE

Suluhisho ni moja tu + mojA,

1. Magufuli awaagize SSiT wawape wamiliki offer ambayo hawawezi kukataa kwa kuwahakikishia ama risasi itaingia vichwani mwao ama wakubali kwa hiari yao kubadilisha mikataba inayo wanyonya wananchi.

1+. Serikali inunue mitambo yake ya kuzalisha umeme, na waitawanye sehemu mbalimbali nchi nzima sio Dar pekeyake, na mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ipate ajali kama vituo vya Aljazeera huko mashariki ya kati.

Hii ni kwasababu, wanaomiliki system ya Tanzania ndio wenye mikono na wanufaika wakubwa na mitambo ya umeme inayotunyonya wananchi!
 
Pia kuna kodi nyingi sana kwenye umeme mara ewura sijui rea bado vat
 
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.
Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE

Nani alipanga wauze kwa bei hiyo na alitumia vigezo gani?
 
Hamjaelewa. Ipo hivi, IPTL wanazalisha umeme kwa sh 90/unit, wanaiuzia Tanesco kwa sh 180/unit, Tanesco wanauzia raia kwa sh 305/unit.

Na je kwa umeme unaozalishwa nje ya IPTL bei za unit zipoje? mana sio power nzima tunaitegemea IPTL tuna vyanzo vyetu pia
 
Namkubali sana prof.muhongo kwa utendaji wake, katika jambo zuri tunaungana pamoja tunaijenga nchi yetu. Pia ajaribu kufumua service charge nayo ni mzigo kwa walaji.
 
Mbwembwe anahoji kama hajui?Aliwahi kuwa waziri ndo umeme ukapanda kipindi chake leo anahoji!!! Tusubiri
 
Hili jipu la umeme linatakiwa kutumbuliwa tena haraka sana. Gas tunayo wanakuja wanyonyaji wanatu-charge kwa 100% kwenye rasilimali zetu. Nyerere hakukosea aliposema njia kuu za uchumi zimilikiwe na serikali.
 
Kipindi hiki, hata shetani ni lazima awe na tabia za malaika.
 
Huyu Waziri Muhongo ni Kichwa.Unajua Serekali iliyopita,ilishindwa kwenda nae na kasi aliyokuwa anaitaka.Sasa ukifanya vizuri wanakufanyia hujma.Ilikuwa hujma Mbaya sana kwa waziri huyu.Ninayo hakika alikuwa Anaingiliwa Na walio jui yake
 
Tumechoka na maigizo huyu alishasema tz umeme kukatika itakuwa historia
 
Back
Top Bottom