Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

Aisee service charge naichukia sana . Atoe hyo kwanza.

Ndugu wewe endelea kulipa tu usidanganywe na maneno ya hadhara hayo, hicho kitu hakiwezi kutolewa leo. Wewe leo unalalamika gharama ipo juu wakati tanesco wenyewe bado wanakuambia wanaendesha kwa hasara wanafikiria gharama zipande kidogo
 
Haya watanzania wasiojua business hata kidogo katika ubora wao.

Huyu waziri kaanza vibaya, huwezi kuanza na kusema tu shusha bei ya umeme huku hujaanza na kusolve matatizo ya umeme wenyewe ambayo yanahitaji pesa, we unaanza na kukata pesa kwanza, TANESCO ni moja ya mashirika masikini hapa nchini, yanaingiza pesa ndio lakini pesa inayotumika kama matumizi ni kubwa mno ndio maana unaona wamefanya valuation yao kua 100% kufidia pesa inayotoka, Tanzania itakuja kua sehemu mbaya sana ya kufanya biashara, ni as if serikali inataka control ya kila business nchini which is stupid and it will fail kwa kua hatuko kwenye ujamaa.

Angeanza na kusolve tatizo la umeme ukipatikana in abundance ndio bei ipungue tu automatically, sasa hivi maji yakizingua inawalazimu muda mwingine kutumia generators ambazo zinakula mafuta kwa kasi ya ajabu, billions zinatoka daily, huyu ni Profesa hilo lazima atakua analijua.
 
Wakati Wa Jk Mimi Nilimchukia Siku Ile Alipopandisha Bei Ya Umeme. Nikafurahia Alipokatwa. Thank God, Amerudi, Akiwa Mpya Katika Hili.
Si aliwaambia muwashe vibatali?
 
Shs.180/unit

Ukiongeza:
1. EWURA
2. REA
3. VAT
4. Capacity charges ndio kufikia hio shs.295/ unit.

Muhongo atakuwa sahihi kushusha bei iwapo hio gharama shs.90/unit aliyoambiwa itajumuisha na hizo habari za EWURA, REA, etc.
You are totally wrong!

TANESCO ndio inayonunua kwa 180/- alafu wanauza kwa 298/- kwa tariff ya T1 (general usage tariff. Kumbuka kuna tariffs nyingine kama D1, T2, T3-MV, na T3-HV).
Then, juu ya hiyo 298/- unachajiwa 22%, yani VAT 18%, EWURA 1% na REA 3%. Na kila mwezi unalipia service charges kwa 5,520/- plus hiyo 22% tena.

zifuatazo ni current tariffs za TANESCO in details:
1. D1- Low usage tariff (75kWh per month). Single phase only. Any unit exceeding 75kWh is charged at 350/-. No monthly service charges
2. T1- General usage tariff. Power is supplied at either 230V (single phase) or 400V (three phase). Consumption does not exceed 7,500kWh per month. Monthly service charges applicable
3. T2- Power is metered at 400V. Average consumption is more than 7,500kWh per month. Demand does not exceed 500kVA per month. Monthly service charges applicable
4. T3-MV- Applicable to customers connected at Medium Voltage
5. T3-HV- Applicable to customers connected at High Voltage, e.g. ZECO, Bulyanhulu Gold Mine, Twiga Cement, etc,

Na hapa chini unaonyeshwa gharama mbalimbali kwa kila tariff category:
1. D1- Service Charge=0; Energy Charge=100/-; Above 75kWh=350/-
2. T1- Service Charge=5,520/-; Energy Charge= 298/-; Demand Charge=0
3. T2- Service Charge=14,233/-; Energy Charge=200/-; Demand Charge=15,004/- per kW
4. T3-MV- Service Charge=16,769/-; Energy Charge=159/-; Demand Charge=13,200/- per kW
5.T3-HV- Service Charge=14,233/-; Energy Charge=156/-; Demand Charge=16,550/- per kW
 
Kiwango cha T1,kina uwanda mpana sana yaani matumizi mpaka 7500KWh yaani mtu unalipishwa gharama na watu wenye viwanda vidogo vidogo wakati wewe unatumia kwa matumizi ya Nyumbani?Hapa kunahitajika kuwe na jedwali maaalum litakalo onyesha matumizi ya nishati kwa kila mtumiaji husika haiwezekani watu ambao wanatumia umeme mpaka uniti 7500 mkalipa gharama sawa lazima wagawanye ili kupatikane unafuu,kwa mfano kama hiyo inayoonyesha low iwe mpaka unit 100,na medium iwe kuanzia 100-150, n.k,na pia bei kwa unit zipungue kwa jinsi unavyo tumia umeme mdogo sio kama walivyo ainisha hapo juu ni kubebeshana gharama zisizo na uwiano uliokuwa murua.
 
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE

Mimi risiti ninazo nunulia zinaonyesha kuwa unit moja ni sh 298@ unit!
 
Gharama za uzalishaji kwa sasa zimeongezeka kwa kiasi gani?
 
Hii nilipot ya mwaka Jana au mwaka huu maana unit kwetu inauzwa 357 mfano nikiweka 10000 napata unit 28 tu nikigawa naona kila unit inaleta 357
 
Muhongo anasema hivi,EWURA wanasema vile,TANESCOA nao wanasema lao. Yani haya mambo hayapo coordinated kabisa.
 
Hapa mambo yana hayako sawa kidogo - Yaani waziri alikua hajui gharama za uzalishaji umeme nchini mpaka afanye ziara ya kustugiza na meneja ndio amwambie hizo gharama , pili Tanesco wanapandisha umeme bila mashauriano na Wizara ?
 
Hii thread ni ya Dec 2015. Mwaka huu Prof Muhongo inaelekea kawaruhusu kupandisha kwa asilimia 8.5% kwa sababu umeme sasa unatengenezwa kwa kutumia gas ya Ntwara!
 
"Bomba la Ges likifika kinyerez umeme utauzwa kwa being ya chini ambayo mwananchi wa chini kabisa ataimudu", nahisi waliosema bomba limeshafika kinyerez na Ges imeanza kuchakatwa walitudanganya
 
Back
Top Bottom