Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

Hv nikisema umeme uwe bure bt kodi za kila mwez kwa kila anaetumia umeme kwa nchi kama tanzania alipishwe shs 15000 hv itashindikana kweli wakiwa sirias?, i mean tumia umeme unavyojua bt hakikisha mwez unapoisha unapeleka 15000 hv its not pocbo kwa wanaojua tushare mawazo!!

Hapo utakuwa unawaumiza wenye matuminz ya kawaida kuna wengne kw mwez matuminz yao ya umeme ni chin ya elf 5! na wengine ni zaid ya laki moja!
 
Hamjaelewa. Ipo hivi, IPTL wanazalisha umeme kwa sh 90/unit, wanaiuzia Tanesco kwa sh 180/unit, Tanesco wanauzia raia kwa sh 305/unit.

OK good clarification, kuna wengine hapa badala ya kufafanua wanakashifu wenzao.
 
Hiyo bei ya 180/Unit ni Kilo Watt ama ni nini mbona hazina uhalisia maana nikipiga hesabu kwa pesa nayotoa kwa mwezi kwa ajili ya malipo ni tsh 40,000,baada ya makato yote ni Tsh kama 13,000 hivi bei ya umeme ni Tsh 27,000 napata uniti 91.5Kwt sasa ukipiga mahesabu ya uniti moja unapata kama 295 hivi.sasa hii ya 180 ni ya wapi au kuna tusioyajua juu ya gharama halisi za umeme

Nami naungia hapo happ wala usiende mbali

Kwani nilivyosoma hapo juu ikabidi nishangae hiyo bei!!!
Mhe,PMuhongo Embu tudadavulie vizuri.

Kwa maana
Tsh 1,000
-Vat 180
Bal. 820

Total unit= 2.8
Bal 820/2.8 = 292 price/unit

Hayo ni mahesabu ya chin kabisa

180 per unit hii bei ya wap?
 
180 per unit ni bei wanayouziwa tanesco..tanesco nae anapanga bei ya kumuuzia mwananchi....yaani mm nikiangalia nashndwa kuelewa hivi ni kweli miaka yte serikali imeshndwa kuiwezesha tanesco wakawa na mitambo yao wenywe ya uzalishaji...
 
Hilo nalo jipu inabidi litumbuliwe.

Naomba anaye chukua maoni ya Dk JPM awasilishe na hili jipu Ikulu.
 
Mimi sishabikii Mbwembwe zinazoendelea !
Kabla hujakubaliana

Na maagizo ya kushusha umeme anagalia

"Rea "unalipia kiasi gani kila unaponunua umeme ??
Si 40% ?

Je si iko kisheria ?? Je,, 40% imeondolewa ??
Mbwembwe tu ?!!
 
Hiyo bei ya 180/Unit ni Kilo Watt ama ni nini mbona hazina uhalisia maana nikipiga hesabu kwa pesa nayotoa kwa mwezi kwa ajili ya malipo ni tsh 40,000,baada ya makato yote ni Tsh kama 13,000 hivi bei ya umeme ni Tsh 27,000 napata uniti 91.5Kwt sasa ukipiga mahesabu ya uniti moja unapata kama 295 hivi.sasa hii ya 180 ni ya wapi au kuna tusioyajua juu ya gharama halisi za umeme
Hapo ni sawa kabisa kuna kitu kimejificha, nadhani labda wao wanawauzia TANESCO kanda nao wanaongeza kitu hapo.
 
Nami naungia hapo happ wala usiende mbali

Kwani nilivyosoma hapo juu ikabidi nishangae hiyo bei!!!
Mhe,PMuhongo Embu tudadavulie vizuri.

Kwa maana
Tsh 1,000
-Vat 180
Bal. 820

Total unit= 2.8
Bal 820/2.8 = 292 price/unit

Hayo ni mahesabu ya chin kabisa

180 per unit hii bei ya wap?

IPTL wanazalisha umeme kwa sh 90/unit, wao wanawauzia Tanesco kwa sh 180. So 180 ni bei ambayo Tanesco wanauziwa na IPTL, Tanesco wakishanunua kwa 180, wao wanatuuzia raia ka tsh 292 kwa unit.
 
Sawa kupunguza bei,lakini naomba serikali itambue kwamba EWURA ni simba mla nyama.Binafsi sioni haja ya kuwa na shirika kama EWURA kama TANESCO ikifanya kazi yake inavyotakiwa.Undwaji wa EWURA ni endorsement ya uzembe wa mashirika yaliyoko chini ya EWURA.Magufuli say no to this.
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Bei ya sasa ya Luku ukiondoa Kodi ni 297.7 Kwa Unit.
 
Hata Mimi naukubali utendaji kazi wa Muhongo ila alinichoniudhi ni kushiriki dili la ESCROW!
 
Muhongo fanya ufanyavyo kwenye hiko kikao service charges ondoeni kabisa,hatutaki huo upuuzi wa kukatwa 5500 kwa ajili ya kumlipa tapeli Harbinder Seth Singh.
 
IPTL wanazalisha umeme kwa sh 90/unit, wao wanawauzia Tanesco kwa sh 180. So 180 ni bei ambayo Tanesco wanauziwa na IPTL, Tanesco wakishanunua kwa 180, wao wanatuuzia raia ka tsh 292 kwa unit.

Akhasante,
lakini hapo ni kwa sababu ni uzalishaji wa Mafuta, Je kwanini tuendelee kununua Umeme kwa mafuta?
By the way juzi tu hapa alisema almost 70% ya umeme wa sasa ni wa Gas, je bei ya umeme wa gas si chini ya Tshs 90/= ?
 
Kuna sehemu nimesoma,anawakaribisha wazawa waje wawekeze kwenye gesi. Nafikiri dawa imemwingia, anacheza kulingana na mapigo.

mkuu wazawa hata kipindi kile aliwakaribisha lakini waliingia mitini. aliwapa wiki nzima waende ofisini kwake na business plan zao lakini wapiii. investment ile inahitaji mabilioni ya pesa ambayo hakuna mtanzania anaweza kucheza biashara ile ya patapotea. unaweza ukakopa pesa benki uka invest mwisho wa siku ukakosa mafuta. utalipaje deni. watanzania tunaweza udalali tu kwa kweli na biashara hiyo Muhongo alikuwa haitaki. inakuwa biashara binafsi mno. ni bora ikamilikiwa na makampuni ya serikali kama Stamiko na wengine wanunue share tuu. ili liwe faida kwa watanzania wote lakini sio mtu binafsi mmoja mmoja
 
Hiyo bei ya 180/Unit ni Kilo Watt ama ni nini mbona hazina uhalisia maana nikipiga hesabu kwa pesa nayotoa kwa mwezi kwa ajili ya malipo ni tsh 40,000,baada ya makato yote ni Tsh kama 13,000 hivi bei ya umeme ni Tsh 27,000 napata uniti 91.5Kwt sasa ukipiga mahesabu ya uniti moja unapata kama 295 hivi.sasa hii ya 180 ni ya wapi au kuna tusioyajua juu ya gharama halisi za umeme

Unit moja si chn ya 290,mm nilinunua umeme wa laki 1 service charge ilkatwa nkaptwa unit 240 muhongo sijui anazungumzia bei ya wap
 
Hata Mimi naukubali utendaji kazi wa Muhongo ila alinichoniudhi ni kushiriki dili la ESCROW!
kamanda wapii inaonyesha alishiriki dili. mimi sijaona popote. labda tuthibishie nasisi tuelewe. usizungumze kishabiki tuu
 
Back
Top Bottom