Profesa Muhongo aiagiza TANESCO ishushe bei ya umeme

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,990
Reaction score
3,551
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Sio Hapo tu, waondoe kabisa service charge za kila mwezi, Ni bora watuuzie luku bei kubwa na isiwe na makato ya kila mwezi, mtu unatoa elfu 10 unapata unit 5? Hii kitu hatutaki kabisa
 
Tusubiri tuone, ila kusema ukweli professor Muhongo namkubali kwa utendaji kazi wake
 
Sio Hapo tu, waondoe kabisa service charge za kila mwezi, Ni bora watuuzie luku bei kubwa na isiwe na makato ya kila mwezi, mtu unatoa elfu 10 unapata unit 5? Hii kitu hatutaki kabisa

hakuna kitu kinanikera kama hicho hivyi maana halisivya service charge nini? maana zamani kwenye Yale mamita ya zamani kidogo ilikuwa na maana kwasababu ilikuwa lazima waje kwako kusoma..
 
Sio Hapo tu, waondoe kabisa service charge za kila mwezi, Ni bora watuuzie luku bei kubwa na isiwe na makato ya kila mwezi, mtu unatoa elfu 10 unapata unit 5? Hii kitu hatutaki kabisa

wapunguze bei ifike 150/-
service charge ibakie pale pale! maana ndiyo TECHNICAL SUPPORT CHARGE YENYEWE!
 
Hiyo bei ya 180/Unit ni Kilo Watt ama ni nini mbona hazina uhalisia maana nikipiga hesabu kwa pesa nayotoa kwa mwezi kwa ajili ya malipo ni tsh 40,000,baada ya makato yote ni Tsh kama 13,000 hivi bei ya umeme ni Tsh 27,000 napata uniti 91.5Kwt sasa ukipiga mahesabu ya uniti moja unapata kama 295 hivi.sasa hii ya 180 ni ya wapi au kuna tusioyajua juu ya gharama halisi za umeme
 
Huyu jamaa namvulia kofia ila kunawatu hawataki hata kulisikia hilo jina huyu mtu bila majungu tungefika nae mbali sana.
 
Hv nikisema umeme uwe bure bt kodi za kila mwez kwa kila anaetumia umeme kwa nchi kama tanzania alipishwe shs 15000 hv itashindikana kweli wakiwa sirias?, i mean tumia umeme unavyojua bt hakikisha mwez unapoisha unapeleka 15000 hv its not pocbo kwa wanaojua tushare mawazo!!
 
Gharama za service charge tulilipa kabla umeme kufungwa but cha ajabu kila mwezi tunalipia the same thing, siwaelewi Tanesco, Muhongo tusaidie
 
Hiyo bei ya 180/Unit ni Kilo Watt ama ni nini mbona hazina uhalisia maana nikipiga hesabu kwa pesa nayotoa kwa mwezi kwa ajili ya malipo ni tsh 40,000,baada ya makato yote ni Tsh kama 13,000 hivi bei ya umeme ni Tsh 27,000 napata uniti 91.5Kwt sasa ukipiga mahesabu ya uniti moja unapata kama 295 hivi.sasa hii ya 180 ni ya wapi au kuna tusioyajua juu ya gharama halisi za umeme
Hiyo bei ya 180 ni bei tanesco inayowalipa hao wezi kina pap, symbion nk kwa 1kwh (ambayo ndiyo unit ya umeme). Muhongo aishauri serikali iiwezeshe tanesco kumiliki mitambo yake ya kuzalisha umeme na huyo aliyewaongeza mkataba iptl akamatwe mara moja, kinyume na hapo hata umeme ukishushwa bei bado serikali itabidi kulipa ruzuku kufidia pengo.
 
Hapa watuuzie umeme shs 130 na service charges zibakie pale pale. Maana shs 40 ukizidisha kwa watanzania wote wanao tumia umeme kwa siku moja ni hela nyingi sana.
 
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE

Asubiri tu maazimio ya wabunge kumtemesha hicho kibarua
 
Wakati Wa Jk Mimi Nilimchukia Siku Ile Alipopandisha Bei Ya Umeme. Nikafurahia Alipokatwa. Thank God, Amerudi, Akiwa Mpya Katika Hili.
 
Kushuka kwa bei ya umeme kwa unit itakua ni hatua moja katika kupunguza ukali wa gharama za umeme.

Hatua nyingine iwe ni kupunguza makato kama service charge n.k

Jiulize kidogo; hivi pamoja na bei kubwa wanayotoza Tanesco kwa unit na service charge kwa nini shirika hili linakabiliwa na madeni?
 
DSC00065.jpg
 
Tanesco ni chaka la mafisadi
 
Back
Top Bottom