Profesa Lipumba: Hakuna haja ya elimu ya uraia kuandika upya Katiba

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Profesa Lipumba amesema kuwa hakuna sababu ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kwa miaka mitatu ili kuandika upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Profesa Lipumba ameongeza kuwa Tume ya Jaji Warioba ilishatoa ufafanuzi kuwa wananchi wanaelewa aina ya katiba wanayohitaji na hakuna sababu yoyote ya msingi kuchelewesha mchakato.

lipumba-pic.jpg

Profesa Lipumba​
 
Profesa Lipumba amesema kuwa hakuna sababu ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili kuandika upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Profesa Lipumba ameongeza kuwa Tume ya Jaji Warioba ilishatoa ufafanuzi kuwa wananchi wanaelewa aina ya katiba wanayohitaji na hakuna sababu yoyote ya msingi kuchelewesha mchakato.

Hatupaswi kuwa na adui au rafiki wa kudumu bali agenda.

Ninakazia: Asizodolewe Prof nguli wa uchumi Haruna Lipumba. Pamoja na matatizo yetu naye hoja yake hapa Ina mashiko.
 
Hicho kisingizio cha elimu ya uraia ni kwa mannufaa ya CCM, wanataka waendelee kuvuta muda mpaka ufike wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, ili hii Katiba mbovu iliyopo iwabebe iwape ushindi, ni kisingizio cha kijinga kisicho na maana kabisa.
 
Kuifahamu nia yao ni jambo muhimu sana. Kifuatacho ITV inakuwa kujipanga kuwagaragaza ndani ya ghiliba zao.

Hilo si jambo dogo wala si jepesi.

Hata hivyo penye nia pana njia.
 
Prof, acha uchochezi, elimu ni muhimu maana sisi CCM tumeona wananchi wengi hawaielewi katiba iliyopo na hata ile wanayoitaka itakuwaje.

Miaka 3 tunaona itawatosha, baada ya hapo ndipo tutaanza mchakato rasmi wa Katiba mpya.

Kidumu chama cha Mapinduzi......
 
Kabla ya kuandika hii katiba mwaka 1977 mlitoa elimu ya uraia kwa miaka mingapi ?
 
Maccm yanafanya makusudi tu ili kuwachelewesha wananchi.

Maana yanatambua fika Katiba iliyopo, iliandaliwa kwa ajili ya manufaa yao! Badala ya manufaa ya wananchi, na nchi kwa ujumla.
 
Profesa Lipumba amesema kuwa hakuna sababu ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kwa miaka mitatu ili kuandika upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Profesa Lipumba ameongeza kuwa Tume ya Jaji Warioba ilishatoa ufafanuzi kuwa wananchi wanaelewa aina ya katiba wanayohitaji na hakuna sababu yoyote ya msingi kuchelewesha mchakato.

View attachment 2738598
Profesa Lipumba​
Naunga mkono kauli ya Prof. Lipu!! Mambo ya miaka mitatu ni ili muda wa uongoz ukaribie Kwisha ili aachiwe ataefuata hili zigo la katiba!!
 
Back
Top Bottom