Watoto wafundishwe uraia, au tuendelee kutumia fedha vibaya kwenye uchaguzi na Katiba mpya

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Matokeo ya kidato cha nne yameacha kujadiliwa, kama kawaida waandishi wameripoti bila kwenda kiundani zaidi kusema matokeo haya yana maanisha nini kwa jamii. Hata hivyo kuna mtu ndani ya JF alienda mbali kufananisha ufaulu wa hisabati na Urai na aliangalia pia fedha zinazowekwa kwenye hisabati na uraia. Soma Je, uwekezaji finyu kwenye somo la Uraia, ni nia ya kuwafanya watu wasijue haki na wajibu wao ili kuiwajibisha Serikali?

Kutokana na hayo nimepata masuala kadhaa ambayo ni muhimu kufikiria. Serikali yetu kila inapofika mwaka wa Uchaguzi huwa kuna kuwa na fungu la Kutoa Elimu kwa umma kuhusu Uchaguzi na Elimu ya Mpiga kura. Elimu ya Mpiga kura ni jambo dogo sana kwenye elimu ya uraia lakini kwa namna ya kipekee limekuwa likipewa upekee usiostahili ambao unawezekana kuwa mzuri kwao wanaopewa tenda ya kufanya hayo. Nimeona Ripoti za Tume ya uchaguzi ikionesha jinsi wasanii na vyombo vya habari vinavyotumika kutoa elimu ya mpiga kura.

Hili sio shida, hadi ufikirie swali hili.

Elimu ya Mpiga Kura ni elimu ya Uraia kwanini isifundishwe shuleni kwa kuongeza uwekezaji kwenye somo la uraia?

Hadi sasa bajeti ya uchaguzi ni kubwa kuliko fedha zinazopelekwa shuleni. Mfano Kwa elimu Msingi(Nursery hadi kidato cha sita) huwa wanapokea takriban Bilioni 18 kila mwaka. Lakini, Shilingi bilioni 180.0 zilitengwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

SHIDA IKO WAPI
Kwa muda mrefu kumekuwa na hitaji kubwa la muda mrefu la Katiba Mpya ambalo hivi karibuni serikali imeridhia suala la kuanza mchakato wa katiba mpya. Hata hivyo wameweka sharti la kwanza waanze kuwaelimisha watu kuhusu katiba kabla ya kuanza mchakato huo ambao ulihitimishwa zamani sana.

Hata hivyo, suala la katiba ni suala la uraia, kwa maana ya kwamba kama watoto wangesoma vyema kuhusu katiba kwenye somo la uraia kusingekuwa na sababu ya kusema kuwa inabidi watoto waelimishwe kuhusu katiba. Maana yangu ni kwamba kwa muda mrefu tumefurahia serikali ikitoa elimu ya mpiga kura, na sasa itakuwa ngumu kukataa wasitoe elimu kuhusu Katiba.

Lakini tumesahau vitu hivi vyote ni basic sana, kila mwananchi inabidi avifahamu sio kupitia kampeni za muda mfupi bali mambo haya yawepo shuleni ili mtu kujifunza kuhusu haki na wajibu wake. Ila pia ni kweli kabisa kwamba kutokana na elimu mbovu ya uraia vijana wetu hawana ufahamu wa katiba, uchaguzi kwa ujumla na masuala mengi ya uwajibikaji na utawala bora.

Naona iko haja hapa ya Wanaopambania Haki za Kielimu kupiga kampeni kuhusu watoto kufundishwa vyema kuhusu uraia, ili tusiwe na mambo kama haya ya ajabu ajabu ambayo sio tu yanatumia fedha vibaya bali pia yanachelewesha michakato muhimu ya kufikia maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom