voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.
Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.
Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.
Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi.
"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo".
Mwisho wa kunukuu.
Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.
Kwanini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?
CCM acheni kucheza na akili za watanzania.