Jaji Warioba akosoa Serikali kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa miaka mitatu

Miaka mitatu elimu ya kuandika katiba mpya!!!!!

  • Hi

    Votes: 0 0.0%
  • 1

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    0

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Waziri Mkuu, mstaafu Jaji Joseph Warioba ameeleza wasiwasi wake kuhusu hatua ya Serikali ya kutaka kuanza kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa miaka mitatu, akisema ni muda mrefu kwa mchakato huo.

“Tumefikia mahali kama kuna utashi wa kisiasa, tunaweza kuamua juu ya haya mabadiliko, inanipa wasiwasi, ni kama tunataka kuanza upya mchakato huu. Unaona mijadala hii ya Katiba inavyoingilia shughuli zetu za maendeleo, nadhani imefika wakati tufanye uamuzi,” amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, ameeleza hayo Ijumaa Agosti 31, 2023 katika mahojiano wa Azam TV yaliyofanyika nyumbani kwake wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.

Juzi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro, alisema watatoa elimu ya mabadiliko ya katiba kwa miaka mitatu, akisema kwamba utafiti walioufanya umeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba na hata wengine hawajawahi kuiona.

Kauli hiyo, Dk Ndumbaro iliwaibua wadau mbalimbali wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), waliokosoa hatua hiyo, wakisema inalenga kuchelewesha mchakatao huo.

Katika maelezo yake, Jaji Warioba amesema wakati akiwa mwenyekiti wa tume hiyo, wananchi walishiriki na walitoa elimu ya kutosha kuhusu Katiba Mpya, akisema walisambaza nakala za Katiba za Tanzania na Zanzibar.

Mbali na hilo, walifanya machapisho kueleza yaliyo katika Katiba na kusambamba katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini, akisema kwa namna yanayoendelea hivi sasa huwezi kusema wananchi hawana elimu kuhusu mchakato huo.

“Kwa jinsi walivyoipanga sioni kama wanaweza kutoa mwanga zaidi kuliko walionao hivi sasa, Kamati ya Mukandala (Profesa Rwekiza), imechukua maoni ya kutosha na wananchi wanajua. Mimi natafsiri Serikali ingesema hatuwezi kupata Katiba Mpya sasa hivi, waseme mapema kuliko hivi,” amesema na kuongeza;
 
Anajua hila zao ndo maan ameingia waswas!! Ila wakati wa mabadiliko ukifika hakutakua na janja janja!!
Kabisa mkuu, hivi wanadhani watanzania ni wale wale wa kuwalevya na jimwenge Lao... Tumefika mahali ambapo uvumilivu wa uongozi wa kibabe umefika mwisho. Hapo naona wanataka hadi uchaguzi wa mama upite ndio walete katiba mpya, maana wanahofika ikija mapema huenda hatorudi Ikulu... Wanatuzungusha. Sasa wajue tumewasoma!!
 
Anajua hila zao ndo maan ameingia waswas!! Ila wakati wa mabadiliko ukifika hakutakua na janja janja!!
Wakati wa mabadiliko ndi huu mkuu 'Pac the Don,' hivi wewe bado unayo wasiwasi juu ya mabadiliko yanayokuja karibuni?

Hawa watu wa CCM sasa hivi ni kama wamerogwa hivi, maanake kila wanalosema au kufanya ni maudhi tu kwa waTanzania.

Chukulia kwa mfano wa mtu kama huyo waziri aliyeyasema hayo ya miaka mitatu, kwa watu kufundishwa mambo ya Katiba.

Hivi huyo mtu kweli kichwani zinamtosha?
 
Rasimu yaWarioba imepitwa na wakati

kuna Vijana wengi hivi Leo hawakuweza kushiriki rasimu ya Warioba ya miaka 10 iliyopita

ni vyema Mchakato ukaanza upya kwa kuelimisha Umma walau kwa miezi 36 kabla ya kuanza rasmi mchakato

Jambo zito kama hili hatuna haja ya kulikimbiza na kuharakisha
 
Angalizo: Hapatafanyika uchaguzi wowote bila KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Wajinga waliisha nji hii!!
 
Screenshot_2023-08-31-21-07-31.jpg
 
Ndumbalo alibugi Sana. Mwanasheria mzima unapiyanga vile ili tu kujikomba kwa Rais, na Rais mwenyewe kamtoa kwenye uwaziri na kumtupa huko kwenye michezo.
 
“Kwa jinsi walivyoipanga sioni kama wanaweza kutoa mwanga zaidi kuliko walionao hivi sasa, Kamati ya Mukandala (Profesa Rwekiza), imechukua maoni ya kutosha na wananchi wanajua. Mimi natafsiri Serikali ingesema hatuwezi kupata Katiba Mpya sasa hivi, waseme mapema kuliko hivi,” amesema na kuongeza;
Hawa wahuni wa Ccm hawapo tayari kuruhusu nchi kupata katiba mpya kwa maslahi yao binafsi.
 
Rasimu yaWarioba imepitwa na wakati

kuna Vijana wengi hivi Leo hawakuweza kushiriki rasimu ya Warioba ya miaka 10 iliyopita

ni vyema Mchakato ukaanza upya kwa kuelimisha Umma walau kwa miezi 36 kabla ya kuanza rasmi mchakato

Jambo zito kama hili hatuna haja ya kulikimbiza na kuharakisha
Mnaiogopa kama ukoma!! Ishi humo 👇👇
 
Attachments

  • IMG_20220629_192816.jpg
    IMG_20220629_192816.jpg
    73.4 KB · Views: 7
Wakati wa mabadiliko ndi huu mkuu 'Pac the Don,' hivi wewe bado unayo wasiwasi juu ya mabadiliko yanayokuja karibuni?

Hawa watu wa CCM sasa hivi ni kama wamerogwa hivi, maanake kila wanalosema au kufanya ni maudhi tu kwa waTanzania.

Chukulia kwa mfano wa mtu kama huyo waziri aliyeyasema hayo ya miaka mitatu, kwa watu kufundishwa mambo ya Katiba.

Hivi huyo mtu kweli kichwani zinamtosha?
Cna shaka mkuu, wakati utafika means yaezakua hata leo au kesho!!
 
Dr. Ndumbaro has been transferred to another ministry. We have a new Minister. Those statements of him are gone. Amb. Dr. Pindi Chana will differentiate herself...hopefully.
 
Back
Top Bottom