Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Uwezi kuwa maharufu bila kuihusisha serikali na haijalishi nikwa mabaya au kwa mazuri na hasa kama unaona unapoteza mwelekeo njia ya CUF iliyobaki ni karata ya muungano kwani karata ya amani na usawa zanzibar imeshatatuliwa na Maalim seif kuwa madarakani!!Kilichobaki ni chokochoko!

Huu ndio mwisho wa hoja zako? Kwani pale Mnapodai nchi isitawalike mnakuwa mmpoteza muelekeo?
 
Barubaru na Wana JF,
Hivi nina swali, ni wananchi wangapi wanajua au kuusoma ule Muungano wa Kwanza waliofikia akina Mwalimu Nyerere na Karume ???? Kwa jinsi nilivyosoma hii post/topic/mada na kuielewa kuna Harufu ya Ubaguzi na Zanzibar kutaka kujitenga.
Angesema Jamhuri ya Tanganyika na sio Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Maana Tanganyika, Zanzibar na Pemba ndio zilizozaa TANZANIA. na penye Tanzania angesema Tanganyika.
Sisi Watanganyika wao Wazanzibar, wakitengana hawatakaa salama, watasema Wao Wapemba na sisi Wazanzibar
My Take: Mbona sisi hatudai Tanganyika yetu ??? Hili suala naliona ni kubwa na linalohitaji tuelimishwe zaidi na zaidi
Mtoto akililia wembe mpe ...........
Nawakilisha
Mtakuwa mna wazimu sana! Hebu angalia kama si uwepo wa Zanzibar kwenye Muungano mgefanya wizi huu? Mgefanya kwa njia gani nanyi mipaka yenu ya bahari inkingwa kila upande? Mkienda kusini mnakuta Msumbiji na mkienda juu Kaskazi mnakutana na Kenya niambie mgedai wapi hizo maili mnazotaka mzidishiwe?
 
Mamlaka ya JMT ni kamili. Eneo la jamhuri ya Muungano ni eneo zima la bara na visiwani. Hakuna eneo lolote la 'nchi ya Zanzibar' ambalo si eneo la JMT. Kama lipo niambie. Katiba ya ZNZ inaweza kusema lolote lakini ikipingana na ile ya Muungano vipengele vyake ni batili. Zanzibar ni nchi kwa Wazanzibari tu; siyo nchi inayotambulika mahal popote duniani. Kuwa na jeshi, mahakama, na rais (mihimili mitatu ya dola) hakuifanyi ZNZ kuwa nchi vinginevyo miye ningetamba niko "nchi" ya Michigan! Kuongeza eneo la bahari kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar na kwa Tanzania nzima. Wananchi wa ZNZ yawapasa wafurahi na kuunga mkono uamuzi huu wa serikali ya JMT.

WAZANZIBARI WENZETU WANAPIGANIA KULIRUDISHA JINA LA NCHI YAO NDANI YA UNITED NATION
]
images

Zanzibar ikiwasilishwa katika umoja wa mataifa 1963

KAMA WEWE NI MTANGANYIKA HALISI BASI IJUE HISTORIA YA NCHI YAKO KULIKO KUBERULIWA BERULIWA
TUU NA MAJACUC:focus:


A%20S%20465.gif
THEY ALWAYS PROUD TO BE ZANZIBARIS EVERY WHERE THE GO AROUND THE WORLD
A%20S%20465.gif

 
Nadhani hapa mtamuonea bure tu huyu mama....Lakini vile vile kwa wanaofahamu mchakato wa mambo haya wanajua kabisa kuwa maamuzi haya ya kimataifa toka chini ngazi za wataalamu hadi inapofikia ngazi ya mawaziri serikali zote mbili hushirikiana vizuri sana.
Lakini hili nalo ni kosa la msingi, unaliita kushirikiana lakini ni dereliction of duty na kutapanya mamlaka, Mama Waziri amekosea na amevunja Katiba. Hii inatokana complexity ya structure of Union inayofanya watu kutoelewa nguzo zinazounda Muungano.

Hati ya Muungano na Katiba ya Jamhuri. Nyaraka hizo zimetaja mambo ya mahusiano ya kimataifa, Mambo ya Nje, kwa lugha ya Katiba, kuwa ni suala la Muungano. Na Kikatiba, na pia kwenye Hati ya Muungano, hakuna jambo la umma linalotakiwa kushughulikiwa na serikali mbili.

Kuna maswala ya Zanzibar yasiyokuwa ya Muungano, yanayoshughulikiwa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na masuala ya Tanzania Bara yaliyokorogwa na yale ya Muungano, yanayoshughulikwa na serikali ya Jamhuri. Hakuna "ku share"! Sijui mpaka hapo nimekosea? Siwezi kukosea kwa sababu nime state only the facts so far, Katiba ni kama Msahafu, kila mtu anayo.

Sasa kwa vile maswala ya kutuma petition Umoja wa Mataifa ni swala la mahusiano ya kimataifa basi swala hili ilibidi lishughulikiwe na uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano tu, au Mama Tibaijuka peke yake! Ndivyo tulivyoandikiana kwenye Katiba! Ndo maana nasema waziri wangu amegawa mamlaka ya kazii kwa vyombo visivyohusika kwa kuwashirikisha Wazanzibar walio nje ya serikali ya Jamhuri, amevunja Katiba. Sio Wazanzibar peke yao wenye grievances na Waziri, na Wabara tupo tunaosema serikali haiheshimu Katiba.

Sioni mahali popote ambapo pana msingi wa kuliuliza Baraza la Wawakilishi juu ya hili kwani suala la eneo la Muungano ni eneo zima la Tanzania. Hakuna bahari ya Zanzibar!
Ambayo ndio hii conclusion uliyoifikia hapo bila kujijua: kwamba, kama swala la Tanzania, la Muungano, halina haja ya kushirikisha Baraza la Wawakilishii wa Zanzibar basi hata ile petition yenyewe ya kuongeza mipaka haikutakiwa kushirikisha serikali ya Zanzibar.

Structure of the Union bado ina confound watu wengi sana. Alipokuwepo Rais Julius Nyerere alikuwa analinda alichokiunda kwa udi na uvumba na dumisho la fikra za Mwenyekiti wa Chama. Lakini sasa tunajifunza kufikiri wenyewe, na kama anavyopenda kusema Rais Ally Mwinyi, "kila enzi la kitabu chake." Turudini kwenye ubao tukachore nchi yetu au nchi zetu upya, hii ya sasa au hizi za sasa, hazi make sense!
 
We MM ni pumba tu siku zote... Kwanza ufahamu kwamba mambo ya ardhi na makazi si mambo ya Muungano, ubaya ni kwamba hii Tanganyika imejificha kwenye mwevuli wa Tanzania, mawaziri wote waTangayika wanaotumikia mambo yasiyo ya muungano, wanaendelea kujiita ni mawaziri wa Tanzania, huu ni upuuzi, Tibaijuka hana mamlaka yakuamuwa mambo yahusuyo muungano, mamlaka yake yanaishia chumbe! Kuhusu kushirikishwa Zanzibar, wahusika wanasema hawajashirikishwa, ndo maana wamemuweka kiti moto waziri mwenye zamana kwa Zanzibar (Shamhuna) aeleze mamlaka ya kuihonga Zanzibar ameyatoa wapi?


Zanzibar haiwezi kunufaika na kuongezwa kwa eneo hilo, sababu tayari hivi sasa hilo eneo liko umbande wake, tungoje katiba mpya kama wananchi wataamuwa serkali 3, Zanzibar itaenda UN kudai kivyake sababu lipo mashairiki ya Zanzibar na huko Tangayika haina mamlaka ya kuomba eneo, sababu ni mbele ya nchi nyengine (Zanzibar)!
 
Tatizo la msingi ni kwamba baadhi ya viongozi wa Zanzibar wamepoteza uwezo wa kuongoza. Hakuna viongozi ambao wana ujasiri wa kusimama dhidi ya watu kama kina Jussa na kuwaambia ukweli; hakuna viongozi Zanzibar wenye uwezo wa kusema na kutetea hoja zao au kupendekeza hoja tofauti na za kina Jussa. Huko kwenye BLW hakuna viongozi wenye ujasiri wa kusimama na kusema hapana!

Wazanzibari wanalazimishwa kuwa na fikra za aina moja na kuwa wasioneshe tofauti yoyote ya mawazo; huu ndio mwanzo wa ule udikteta wenyewe. Wachache ambao wanaweza kuwa ni pro-union wanaogopa kusimama na kuwapinga hawa separasists kama kina Jussa. Hawawezi kwa sababu wamekubali kuingia katika political pandering kwamba kila mmoja akitaka kuonekana ni kiongozi mzuri basi lazima awe against the union, deparaging watu wa bara, kebehi ya Nyerere n.k Matokeo yake watu wenye ujasiri wamekosekana na muungano wao unatokana na chuki sasa.

Hawa Wazanzibar ndugu zetu umoja wao uko kwa sababu wanaonekana kuchukia Muungano na kuichukia Tanzania bara; wanaamini kuwa ni Tanganyika ndio tatizo lao wakati kwa kila kipimo wako wanajiamulia mambo yao mengi wao wenyewe. Wanajiaminisha kuwa wao ni nchi na ina mambo yake na wanataka wawe nchi wakiwa bado kwenye muungano! Bahati mbaya ukweli wameambiwa mara nyingi lakini hawataki kuamini - Zanzibar siyo nchi mahali popote pale isipokuwa kwa Zanzibar yenyewe.

KUna nchi nchi moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 1) ya Katiba Ya Muungano. Na Katiba hiyo inasema wazi kuwa eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na Eneo lote la Tanzania Visiwani na bahari yake! Wazanzibari hawaamini kuwa wao siyo nchi! Wakati umefika tuanze kuwahakikishia ndugu zetu kuwa wao ni sehemu ya Muungano na ni wananchi wa Tanzania. Kama kweli wanaona muungano hauwafahi au ni tatizo wajitokeze tu na kudai kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano.

Lakini wafanye hivi kwa kujiuzulu kwanza nafasi zao kwenye Muungano ili wapiganie kujitenga kwa Zanzibar! Haiwezekani upande mmoja wanafurahia matunda ya Muungano wakati huo huo hawautaki!
 
Wanasiasa wengine wanaongea mambo kwa kuangalia nyuma badala ya kuangalia mbele. Mwishoni watadai kuwa tunataka Deutsch Ostafrika irudi, tuwe na Sultani Zanzibar, tuwe chini ya Malkia ili tusiwe tunaiomba Uingereza misaada tena kwa vile itakuwa ni sehemu ya jukumu lao kutupa misaada hiyo, tuwe na biashara ya utumwa na mambo mengine mengi tuliyokwisha yaacha ili kuangalia mbele. Ningeelewa kama kiongozi huyo angekuwa anatumia historia kurekebisha tunakokwenda badala ya kutumia histotia kuturudisha kule historia ilikotutoa.

Tibaijuka aliomba eneo la International waters linalopakana na Tanzania lipunguzwe ili Tanzania iwe na control kubwa kwenye maji ya bahari yanayoizunguka; je kuna tatizo gani hapo? Nionavyo ni kuwa kwa kiwango kikubwa, iwapo ombi hilo litakubaliwa, basi Zanzibar ndiyo itakayonufaika zaidi ya ndugu zangu wa Tabora; je Zanzibar wanaumziwa na nini?
 
hivi kanini muungano usivunjike? Kama hatuwezi kushare mali asili zetu muungano wa nini kwakuwa that means hakuna umoja.
Na wazanzibar mbona mlikuwa hamlalamiki wakati mlipokuwa mkipewa ela iliyotokana na mapato ya madini yetu mbona hamkuwahi kusema hilo suala halipo kwenye katiba?
Mimi naona tunapotezeana muda tutengene kila nchi iendelee na mambo yake na kila mtu arudi kwao wazanzibari warud zanzibar na watanganyika walioko zenj warudi bara maana naona ina tu cost kuendelea kubishana.
Hata sisi baadhi ya watanganyika muungano hatuutaki na sababu kubwa ni wazenj kulalamika sana na kututukana sana mara machogo, mara sijui nini na dharau zisizo kuwa na msingi.
Wao wanahisi ni waarabu basi tutengane wapate nafasi ya kupractice uarabu vizuri
 
Nina wasi na Uraia wenu! Kwa nini munajenga hofu kubwa ya kurejeshwa nchi ya Tanganyika! Jengine ni kwamba musijitie UJUA wa kutokuona mambo, akili zenu zichuchuzeni kidogo ili zione mbali kabla hazijalemaa; Wapemba (Wazanzibari) hawapo Tanganyika tu bali wameekeza duniani kote.

Very confident about what I say and I am a born hard Tanzanian. Tungekuwa hatuwajui vizuri tungewaogopa na maneno yenu ya rejareja kama vile debe tupu lisiloacha kutika! Dunia nzima mnayoongelea ni dunia gani? Hii hii inayotuzunguka? Msiache mbachao kwa msala upitao mkafikiri Dunia itawaonea huruma kwa kutotumia vema akili zenu mkiamua kuuvunja muungano.
Mtu yuko kigamboni au pale msasani anaishi bila kuhangaishwa, halafu leo anajidai haoni manufaa ya muungano anataka uvunjike. Avunje akiwa Zenj basi maana baada ya kuvunjika atakuwa anaishi huku bila uhalali. Na wanaodai muungano uvunjike ni wanasiasa uchwara ambao wanafikiri watachukua vyeo chap chap muungano ukisambaratika.
 
Huu Muungano ni pasua kichwa!
Haya manung'uniko, malalamishi na "kutunishiana misuli" vitaisha lini?
 
Ombi to my fellow Tanganyikans, why dont we giveup on them? naona kama tunaendeshwa hivi! if "For Gods' sake i will be given say a minte to be a president, i will grant them independance, they are never setlled! always blames! oups! Havocts! eveyrthing odd you mention, why dont we give them the thing they want? i mean their total independance? One day people are going to remember what i am writing here! They are not good people, people walkup, tuwape uhuru wao and waende!
 
natamani ningekuwa rais ningeifanya zenj mkoa na hao vimbelembele kama jusa ningewarudisha kwao uaharabuni, hawa ndio wanaotududisha nyuima. Tanahitaji raisi mbabe ndio tuendelee. La sivyo hatutafika mahali. Huyu jussa ni ni mtu hatari na si mzalendo kabisa ni mamluki
Ata vile Zanzibar ni mkoa. Nadhani JK amelegea fulani katika kuitumikia JMT na ndo maana watu wa Z wamejisahau kuwa hiyo si nchi bali ni mkoa. Nadhani kila mkoa wa JMT huwe na tawala kama za Z ili tupeleke maendeleo kwa wananchi. Mf. Serikali ya mkoa wa Z, Serikali ya Mkoa wa Dar, n.k.
 
You cant eat your cake and have it..... Muungano mnajifanya kuupinga wakati huo huo mnataka mtambulike kama nchi ndani ya muungano?? Lol! Ningekuwa raisi wa nji hii... unguja inakuwa mkoa, pemba inakuwa mkoa hawataki lala mbele.
 
Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.

Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.

Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.

sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.


kwenye red kumbe upeo wako wa kufikiri mdogo na tena finyu kabisa! hivi inanifanya hayo ya juu ambayo siyajui nisiamini ubongo wako maana nalolijua wanidanganya je nisilolijua!
 
Jamani mamlaka ya Zanzibar kieneo yanaisha wapi? Yainaisha chumbe au zaidi ya chumbe. Will someone kindly tell /define territorial boundaries within which zanzibar enjoys territorial autonomy
 
Tatizo la msingi ni kwamba baadhi ya viongozi wa Zanzibar wamepoteza uwezo wa kuongoza. Hakuna viongozi ambao wana ujasiri wa kusimama dhidi ya watu kama kina Jussa na kuwaambia ukweli; hakuna viongozi Zanzibar wenye uwezo wa kusema na kutetea hoja zao au kupendekeza hoja tofauti na za kina Jussa. Huko kwenye BLW hakuna viongozi wenye ujasiri wa kusimama na kusema hapana!

Wazanzibari wanalazimishwa kuwa na fikra za aina moja na kuwa wasioneshe tofauti yoyote ya mawazo; huu ndio mwanzo wa ule udikteta wenyewe. Wachache ambao wanaweza kuwa ni pro-union wanaogopa kusimama na kuwapinga hawa separasists kama kina Jussa. Hawawezi kwa sababu wamekubali kuingia katika political pandering kwamba kila mmoja akitaka kuonekana ni kiongozi mzuri basi lazima awe against the union, deparaging watu wa bara, kebehi ya Nyerere n.k Matokeo yake watu wenye ujasiri wamekosekana na muungano wao unatokana na chuki sasa.

Hawa Wazanzibar ndugu zetu umoja wao uko kwa sababu wanaonekana kuchukia Muungano na kuichukia Tanzania bara; wanaamini kuwa ni Tanganyika ndio tatizo lao wakati kwa kila kipimo wako wanajiamulia mambo yao mengi wao wenyewe. Wanajiaminisha kuwa wao ni nchi na ina mambo yake na wanataka wawe nchi wakiwa bado kwenye muungano! Bahati mbaya ukweli wameambiwa mara nyingi lakini hawataki kuamini - Zanzibar siyo nchi mahali popote pale isipokuwa kwa Zanzibar yenyewe.

KUna nchi nchi moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 1) ya Katiba Ya Muungano. Na Katiba hiyo inasema wazi kuwa eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na Eneo lote la Tanzania Visiwani na bahari yake! Wazanzibari hawaamini kuwa wao siyo nchi! Wakati umefika tuanze kuwahakikishia ndugu zetu kuwa wao ni sehemu ya Muungano na ni wananchi wa Tanzania. Kama kweli wanaona muungano hauwafahi au ni tatizo wajitokeze tu na kudai kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano.

Lakini wafanye hivi kwa kujiuzulu kwanza nafasi zao kwenye Muungano ili wapiganie kujitenga kwa Zanzibar! Haiwezekani upande mmoja wanafurahia matunda ya Muungano wakati huo huo hawautaki!
Kilichowafikisha hapa viongozi wa Zanzibar ni chaguzi na matokeo ya kijinga. Sasa hivi wanachukua madaraka kwa ridhaa ya Maalim Seif na Jussa. Hili nalo lina mizizi yake huku bara. CCM bara imekuwa ikiwapelekea Wazanzibar wagombea ambao sio chaguo lao.
Kinachonishangaza zaidi ni vijana kama Jussa kuidharau katiba ya JMT kwa makusudi kabisa. Mipaka ya Tanzania ni suala la katiba ya JMT. Mama Tibaijuka hashughulikii ARDHI kwenye suala hili. Anashughulikia mipaka.
 
Back
Top Bottom