Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Barubaru,

..Makamu Mwenyekiti wa Tume iliyofanyia utafiti wa suala hili ni Mzanzibari.

..Ujumbe wa Tanzania uliowasilisha ombi letu UN yupo Afisa toka serikali ya mapinduzi Zanzibar, na Mama Zhakia Meghji ambao ni Wazanzibari.

..Hata sasa hivi tunavyozungumza Naibu Balozi wa Tanzania UN ni Mzanzibari.

..Zanzibar kama "nchi" isingeweza kuwasilisha ombi hilo kwasababu haitambuliki UN. kinachotakiwa kufanyika ktk mazingira haya ni kusubiri kwanza ombi hilo la kuongezewa mipaka ya bahari lipite. Baada ya hapo SMZ na SMT zinaweza kukaa na kuchanganua mgawanyo wa eneo lililoongezeka kwa kuzingatia mipaka ya Zanzibar na Tanganyika.
 
Hamjamstukia Jusa, chokochoko zote hizi anataka CUF ifunge ndoa nyingine! Baada ya mapenzi kunoga ktk SUK,sasa wanataka kufunga ndoa na braza mkubwa, JMT!
 
Je unajuwa mamlaka ya rasi wa Znz kwa mujibu wa katiba ya muungano?

Mamlaka ya rais wa JMTz ni kwa mambo yote yaliyomo ndani ya mkataba wa muungano na mambo yote yanayokhusu Tanganyika (kwenye katiba yenu wameita Tanganyika kama Tz Bara)
Mkuu unajichanganya kwa hili. Kosa la Prof. Tibaijuka lipo wapi? Mbona mnapenda kucomplicate mambo? Chuki haitakusaidia. Be realistic hizi njozi za mchana zitakuumiza bila sababu. Hakuna nchi inaitwa Zanzibar. Hata UN watawashangaa actually so far wanawashangaa. Acheni kuwapotosha wananchi kwa propaganda zenu kwa kujineemesha wenyewe kwa chuki zisizo na msingi wowote. Tanzania ni ya watanzania wa bara na visiwani.
 
CUF na siasa zao za msimu,lol! Siku hizi hawana cha kuongea. Wamevamia meli inayoutwa muungano, ili tujue nao bado wapo.
 
Hivi Zanzibar inatambuliwa UN kama nchi? Hivi UN waweza pokea ombi toka kwa mwanachama ambaye si nchi akiishtaki nchi? Zanzibar kwenda kupinga UN wataenda kama nani hadi UN wawasikilize? Hivi CUF wanajua wanachoongea? Hivi UN wanafikiri ni Jimbo la Wawi ambako mwana CUF yeyote aweza enda na kusema lolote.CUF hata wakienda UN nobody will listen to them after all CUF is not a UN member.

Umeona kama Dr Slaa kuhudhuria NEC ya CCM
 
Mzee, hapa pana nchi mbili ati au unajifanya hujui? Pana Tanzania na Zanzibar hili hata halihitaji kwenda shule.
Katiba mpya inacheleweshwa tu watu wanataka kieleweke mapema wajipange kuliko kuendelea hivi kama wasanii wa maigizo.
 
Sera ya CUF ni kuvunja muungano tangu zamani. Lakini ni ukweli kabisa kuwa Jusa ni msemaji wao mkuu ambaye mara nyingi nashindwa kutafakari na kupima anayoyaropoka. Maalim Sefu kwa sasa hatamani sana kujiweka mbele kwenye hili. Hata hivyo wazanzibari wasiopenda muungano asilimia kubwa ni wapemba matajiri, wenye uhusiano na uarabuni wakisaidiana na na wale matajiri na wenye madaraka serikalini wa Unguja. Lengo kubwa ni manufaa yao ya binafsi ambayo kwa kiukweli ni kuona karibu na pua zao tu, mafanikio yao kiuchumi yanategemea sana bara.

Tanzania inatakiwa iwe nchi moja na wala siyo tatu
 
Barubaru,

..Makamu Mwenyekiti wa Tume iliyofanyia utafiti wa suala hili ni Mzanzibari.

..Ujumbe wa Tanzania uliowasilisha ombi letu UN yupo Afisa toka serikali ya mapinduzi Zanzibar, na Mama Zhakia Meghji ambao ni Wazanzibari.

..Hata sasa hivi tunavyozungumza Naibu Balozi wa Tanzania UN ni Mzanzibari.

..Zanzibar kama "nchi" isingeweza kuwasilisha ombi hilo kwasababu haitambuliki UN. kinachotakiwa kufanyika ktk mazingira haya ni kusubiri kwanza ombi hilo la kuongezewa mipaka ya bahari lipite. Baada ya hapo SMZ na SMT zinaweza kukaa na kuchanganua mgawanyo wa eneo lililoongezeka kwa kuzingatia mipaka ya Zanzibar na Tanganyika.

Ahsante Joka Kuu , hizo zako ndizo zinazoitwa busara. Na mtu akikosa busara ni hatari kubwa sana. akiwa ni Kiongozi kama Bw. Jussa basi ni balaa tupu. Inawezekana ana hoja ya nguvu lakini "presentation na approach" iliyotawaliwa na jazba inashusha hadhi yake licha ya kuwa na nvuto kwa kundi dogo la watu wachache wenye hulka kama yake.
 
Wewe naona umejazwa ujinga na Jussa Ladhu

Tanzania citizen number one JK alisema hivi ukiwa ndani ya mipaka ya JMT , ZNZ ni nchi, ukiwa nje ya mipaka ya JMT, ZNZ sio nchi. Ngoja niachane na JK because he is un reliable.

Lakini chombo chenye Jukumu la kutafisiri sheria zetu including katiba i.e mahakama kuu ilisema kwamba ZNZ sio nchi na uhaini hauwezi kutendwa ZNZ. Hiyo hukumu hadi hii leo ina stand and can be referred at any tea time.

Sasa kati yako na Mahakamu kuu nani anafahamu katiba zaidi?!

Acha masaburi bana!


Si yale yale Mahakama kuu ya nani? Zanzibar ina mahakama kuu yake na unapozungumzia nje ya nchi aliyozungumza Kikwete unakusudia hiyo mahakama Kuu ni ya nje Pia?

Angalia wewe unapojipiga kifuwa usiwe mjinga wa kuffahamu. Kesi ya Uhaini unayoitaja ilifanywa kisiasa tu na kama hu mtoto kama ninavyodhania basi ungejuwa kuwa Zanzibar kumeshafanywa uhaini mara nyingi na hukumu zimeshatolewa na hiyo Mahakama yako haikuwahi hata siku moja kuingilia kati.
 
Kuna watu hapa wanaona karibu sana. Mhanga mkubwa wa kuvunjika kwa muungano sio Tanzania bara. Time will tell mtakavyoanza kuona makali ya kuja kujibanza na kuchuma Tanganyika halafu mnaenda kula Zenj. Huyo Jussa mwenyewe si ajabu ana majumba Tanganyika...awahi kuuvunja ili turithi bila kutolea jasho

Nionavyo mimi kuna watu hapa ni wa ajabu! Iwapo wao sio watakaohasirika sasa nini kulazimisha kila siku? Hili tunalozungumza ni moja ya sababu ya watu hao kungangania hicho unachojidai kuwa ni hasara kwa wasioona mbele> Nakubaliana nawe kuwa kuona mbele kwenu ndio kunakotufikisha kwenye mjadala huu. Si mnataka kuhodhi kisicho chenu kwa kisingizio cha udugu? Sasa huo mnaofanya ni wizi ambao haungewezekana kama si kungangania huu muungano.
 
si na wao waende wakaombe kama ni nchi? kwanini wapige kelele?waende UN wakaombe wapewe kama nchi sio kama sehemu ya muungano. full stop. braza Barobaro mi nafurahi mnatusaidia kuipata Tanganyika yetu. Hapa wala hatutatumia nguvu na bado mtalalamika kuwa mmefanya tanganyika imerudi pasipo watanganyika kuidai
 
My Take:

Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti
anajua fika suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.

Ndugu barubaru,
100% it's none of ur shit business! umekuwa ukijiita kuwa ni raia wa oman, sasa mambo ya Tanzania yanakuhusu nini wewe? we don't need any of ur garbage opinion, we know exactly that shallow minded like you,jussa and the like r trying to instigate something and you always seem to be against the prosperity of our nation, what an advice can a cockroach give to a butterfly!? feed on filthy shit!? NO HELL NO, a butterfly feeds on succulent flowers! it should stick firmly in ur pale mind now and forever that TZ issues are none of oman issues!
Hapo kwenye red, waziri ameomba kuongeza mipaka ya bahari na si ardhi, huko kwenu oman sijui mnatofautishaje kati ya ardhi na bahari!? na kama katiba inasema ni suala ardhi(zanzibar) tu kuwa si la muungano bila kutaja bahari basi hapo ujue waziri ametumia loophole na hivyo hana makosa!
Nakutakia siku njema barubaru bin waruwaru![/QUOTE]

Urithi ni urithi tu! What do you mmean by instigation here? If you follow the daily occurancy of this issue you would realise that those who are against the whole piracy scheme are not the like of Jussas as you want us to believe. It is a common stand for all Zanzibarians.
On the other hand you cant distinguish land and sea in these days as many countries even among the developed, have been claiming even Antartic.
 
barubaru is just a coward,.rats always dump a sinking ship,mapambano ya ukombozi zanzibar yalipokuwa makali,waruwaru akakimbilia kwao uarabuni,now he talks like a true patriot...shut the hell up waachie wazalendo wanaomenyeka kule pemba na unguja waamue kuhusu the so called nchi yao sio raia wa nchi ya kigeni kama wewe..


On the same pick Tibaijuka si Mzalendo wa Zanzibar au wewe for that matter! Naona ungekuwa na busara kwa kuanza kutekeleza ushauri wako! Kwa nyote Hand off Zanzibar and its resources!
 
CCM ndio wanajua ku-deal na hawa wenzao. Seif Sharif Hamad ndio alikuwa anaongoza kwa kidomodomo, siku hizi tangu apewe ruksa kunywa chai Ikulu unamsikia tena? Huyo Jusi Mwitu akipewa kacheo kidogo tu, mambo yoote atayasahau. Ni njaa tu inamsumbua

Hili domo lako litisha hapo 2020 Raila atakapokutawaleni ili muone raha ya kutawaliwa!
 
Nadhani hapa mtamuonea bure tu huyu mama. Hakuna nchi mbili au mataifa mawili. Kuna nchi moja tu nayo inaitwa Tanzania. Prof. Tibaijuka anatumikia Jamhuri ya Muungano wa TAnzania. Na kinyume na wanasiasa wa CUF wanavyojaribu kushawishi, uamuzi huo ulipewa baraka na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndio maana Waziri toka kwenye serikali hiyo naye alikuwepo UN wakati wa kupeleka ombi hilo. Lakini vile vile kwa wanaofahamu mchakato wa mambo haya wanajua kabisa kuwa maamuzi haya ya kimataifa toka chini ngazi za wataalamu hadi inapofikia ngazi ya mawaziri serikali zote mbili hushirikiana vizuri sana.

Kuongeza eneo la bahari haiongezi eneo la bahari ya Tanganyika! Linaonekana eneo la bahari ya Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake. Kwa hiyo labda kama kuna sababu nyingine. Sioni mahali popote ambapo pana msingi wa kuliuliza Baraza la Wawakilishi juu ya hili kwani suala la eneo la Muungano ni eneo zima la Tanzania. Hakuna bahari ya Zanzibar!

Kama wapo watu wa CUF au wengine wanaoamini kitendo hiki kiko nje ya madaraka ya serikali ya Muungano; wafungue kesi ya Kikatiba kukipinga na kukizuia. Of course, I know no one will.
Uwezi kuwa maharufu bila kuihusisha serikali na haijalishi nikwa mabaya au kwa mazuri na hasa kama unaona unapoteza mwelekeo njia ya CUF iliyobaki ni karata ya muungano kwani karata ya amani na usawa zanzibar imeshatatuliwa na Maalim seif kuwa madarakani!!Kilichobaki ni chokochoko!
 
Hivi Zanzibar inatambuliwa UN kama nchi? Hivi UN waweza pokea ombi toka kwa mwanachama ambaye si nchi akiishtaki nchi? Zanzibar kwenda kupinga UN wataenda kama nani hadi UN wawasikilize? Hivi CUF wanajua wanachoongea? Hivi UN wanafikiri ni Jimbo la Wawi ambako mwana CUF yeyote aweza enda na kusema lolote.CUF hata wakienda UN nobody will listen to them after all CUF is not a UN member.

Utashanga kuwa UN iliwatambuwa wakombozi wa Libya. Kwenye Piracy hakuna mipaka bali ni sheria za Kimataifa na usifikiri hao UN ni mazuzute kama tulivyo sisi huku kuwa watafanya kitu bila ya kuangalia mikataba ya pande mbili.
 
Ni sawa ulivyosema kuwa Zanzibar ni nchi kamili kwa sharia za Zanzibar sio za UN.Ni kweli hata muungano tunalijua.Ukienda UN unatakiwa uende na faili la sheria za UN huendi na faili la sharia za Zanzibar faili la sharia za Zanzibar mwisho wake ni bandari ya Zanzibar.

Ukienda UN wanaangalia Sheria za kimataifa na moja ya sheria hiyo ni sheria iliyozaa hiyo nchi inayoitwa Tanzania. Nafikiri umesahau ni juzijuzi tu jumuiya ya kimataifa ilingilia usuluhisho wa Zanzibar . Sasa iwapo Zanzibar haitambulik kama unavyodai sijui jumuia za Kimataifa zilingilia vipi?
 
Taaanzania Tanzaniaaaa, nakupenda kwa moyo woooooteeeee. Nchi yangu Tanzaniaaa jina lako ni tamu sanaaa....
Mh! Huu wimbo bado upo kweli?

Huyo Jussa hata haelewi anadai nini. Yupo tu anapiga makelele mengi lakini anachokidai wala hakielewi! Walio karibu nae ni wema wakamfahamisha kuwa eneo hilo linapoongezwa Zanzibar nayo itafaidika! Uchoyo wa mafuta na gas unampofusha mpaka anajinyima mwenyewe fursa ya kupata eneo zaidi la kutafuta hayo mafuta na gas.

Jussa kumbuka kuwa eneo la Zanzibar iko ndani ya JMT!


Huo ni uhalali wa Jussa na ni kosa kwako kuingilia kwani halikuhusu
 
Barubaru na Wana JF,
Hivi nina swali, ni wananchi wangapi wanajua au kuusoma ule Muungano wa Kwanza waliofikia akina Mwalimu Nyerere na Karume ???? Kwa jinsi nilivyosoma hii post/topic/mada na kuielewa kuna Harufu ya Ubaguzi na Zanzibar kutaka kujitenga.
Angesema Jamhuri ya Tanganyika na sio Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Maana Tanganyika, Zanzibar na Pemba ndio zilizozaa TANZANIA. na penye Tanzania angesema Tanganyika.
Sisi Watanganyika wao Wazanzibar, wakitengana hawatakaa salama, watasema Wao Wapemba na sisi Wazanzibar
My Take: Mbona sisi hatudai Tanganyika yetu ??? Hili suala naliona ni kubwa na linalohitaji tuelimishwe zaidi na zaidi
Mtoto akililia wembe mpe ...........
Nawakilisha

Na Mwinyi Sadallah
23rd January 2012

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kwamba kitapinga Umoja wa Mataifa (UN) kuiongezea Tanzania mipaka ya eneo la kiuchumi la bahari Kuu kabla ya kupatikana muafaka kati ya Serikali ya Muungano na Zanzibar.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi mambo ya nje wa Chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale huko kisiwani Pemba jana.

Alisema Serikali ya Muungano imefanya makosa kuandaa kupeleka maombi ya kutaka kuongezewa mipaka ya eneo tengefu la kiuchumi la bahari kuu (EEZ) bila ya kushirikisha Zanzibar.

Jussa alisema wananchi wa Zanzibar wapo tayari kupoteza maisha lakini hawatokubali eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuongezwa na kuwa sehemu ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Wananchi wa Pemba simameni kidete kutetea maslahi ya Zanzibar hata kama tutamalizika sote haiwezekani eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuwa la muungano,” alisema Jussa.

Alifafanua kuwa Januari 16 mwaka huu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alitangaza mpango wa Tanzania kuomba UN kuiongezea maili 150 sawa na kilometa 241.5 kutoka usawa wa mwambao wa Tanzania.

Profesa Tibaijuka alisema kazi ya kukamilisha andiko hilo ilianza mwaka 2007 na kugharimu Sh. Bilioni 5.2 na kushilikisha wataalamu kutoka sekta ya mbalimbali, ili iweze kulifanyia utafiti zaidi kuhusu rasilimali zilizoko chini ya bahari kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

Jussa alisema mpango huo umelenga kuiwezesha serikali ya Muungano kuongezewa eneo hilo ili kufanikisha mpango wake kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta wakati SMZ imekwishaliondoa kwenye orodha ya mambo ya muungano.

Hata hivyo, alisema mpango wa Tanzania kuongezewa eneo la maili 150 kutoka usawa wa bahari ya Hindi umefanyika bila ya kuishilikisha SMZ.

Jussa ambaye pia mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, alisema alipohoji suala hilo ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) alitakiwa na serikali kuwa na subira na kutoa nafasi kwa serikali ya SMZ kulifuatilia.

Alisema suala la mafuta na gesi asilia tayari SMZ imeamua tangu mwaka 2009 kuliondoa katika orodha ya mambo ya muungano na haikuwa muafaka kwa serikali kupeleka maombi hayo bila ya kupata baraka ya Zanzibar.

“Wenzetu wanataka kuchimba mafuta na gesi asilia ya Zanzibar kwa kutumia mlango wa nyuma hatukubali kwa maslahi ya Zanzibar na nchi yetu,” alisema Jussa.

Kuhusu kufukuzwa kwa viongozi wanne wa CUF akiwemo Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed, alisema viongozi hao wamekwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1992.

Alisema CUF ilianzishwa kwa madhumuni makubwa ya kupingania haki za Zanzibar na wananchi wake ikiwemo mfumo wa Muungano.

Jussa alisema katika kupingania haki za Zanzibar ndiyo maana wapo watu wamepoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu ndiyo maana chama kimeamua kuwafukuza viongozi hao baada ya kwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa haki za Binadamu na mahusiano ya umma Salim Biman, alisema kwamba viongozi waliyofukuzwa ndani ya CUF waliweka maslahi binafsi mbele badala ya maslahi ya chama na wanachama wake.

Awali akisoma risala ya mikoa miwili ya wanachama wa CUF Kisiwani Pemba, Ayoub Yussuf Mgeni, alisema wanachama wanaunga mkono maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwatimu viongozi hao.

Alisema viongozi hao ni wasaliti kutokana na kitendo chao cha kutetea maslahi binafsi na kuwapaka matope viongozi wa kitaifa kwa kutaka kuwagawanya kwa mtazamo wa Uunguja, Upemba na Utanzania Bara.

Alisema CUF kimefanya kazi kubwa kupingania misingi ya haki za binadamu na utawala bora hadi kufanikiwa kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Novemba mwaka 2010.

Alisema tangu kundwa kwa serikali hiyo kesi za kisiasa, ubaguzi na ukikwaji haki za binadamu umeondoka kwa wananchi wa Zanzibar.

Aliongeza kuwa hatua kama hizo zinapaswa kuendelea kuchukuliwa kwa mwanachama yoyote anayetaka kuvuruga umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.

Mapema Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia Makamu wa kwanza wa Rais, alipokea maadamano ya amani ambayo yalinzia huko Machomanne kupitia Mkanjuni huku wanachama wakiwa wamebeba mabango ya kumshutumu Mbunge wa Wawi aliyevuliwa uanachama Hamad Rashid Mohammed.

Baadhi ya mabango yalisomeka ‘Tumekukuta Wawi na shuka kiunoni, tumekupeleka Dodoma na suti leo watusaliti’; ‘Tamaa imekuponza, siasa hukuweza rudi Wawi ukavue’ na lingine likisema ‘Hamad umepanda upepo utavuna dhuruba’


CHANZO: NIPASHE

My Take:

Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti anajua fika suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.
 
Back
Top Bottom