Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,325
- Thread starter
- #181
Tatizo la msingi ni kwamba baadhi ya viongozi wa Zanzibar wamepoteza uwezo wa kuongoza. Hakuna viongozi ambao wana ujasiri wa kusimama dhidi ya watu kama kina Jussa na kuwaambia ukweli; hakuna viongozi Zanzibar wenye uwezo wa kusema na kutetea hoja zao au kupendekeza hoja tofauti na za kina Jussa. Huko kwenye BLW hakuna viongozi wenye ujasiri wa kusimama na kusema hapana!
Wazanzibari wanalazimishwa kuwa na fikra za aina moja na kuwa wasioneshe tofauti yoyote ya mawazo; huu ndio mwanzo wa ule udikteta wenyewe. Wachache ambao wanaweza kuwa ni pro-union wanaogopa kusimama na kuwapinga hawa separasists kama kina Jussa. Hawawezi kwa sababu wamekubali kuingia katika political pandering kwamba kila mmoja akitaka kuonekana ni kiongozi mzuri basi lazima awe against the union, deparaging watu wa bara, kebehi ya Nyerere n.k Matokeo yake watu wenye ujasiri wamekosekana na muungano wao unatokana na chuki sasa.
Hawa Wazanzibar ndugu zetu umoja wao uko kwa sababu wanaonekana kuchukia Muungano na kuichukia Tanzania bara; wanaamini kuwa ni Tanganyika ndio tatizo lao wakati kwa kila kipimo wako wanajiamulia mambo yao mengi wao wenyewe. Wanajiaminisha kuwa wao ni nchi na ina mambo yake na wanataka wawe nchi wakiwa bado kwenye muungano! Bahati mbaya ukweli wameambiwa mara nyingi lakini hawataki kuamini - Zanzibar siyo nchi mahali popote pale isipokuwa kwa Zanzibar yenyewe.
KUna nchi nchi moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 1) ya Katiba Ya Muungano. Na Katiba hiyo inasema wazi kuwa eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na Eneo lote la Tanzania Visiwani na bahari yake! Wazanzibari hawaamini kuwa wao siyo nchi! Wakati umefika tuanze kuwahakikishia ndugu zetu kuwa wao ni sehemu ya Muungano na ni wananchi wa Tanzania. Kama kweli wanaona muungano hauwafahi au ni tatizo wajitokeze tu na kudai kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano.
Lakini wafanye hivi kwa kujiuzulu kwanza nafasi zao kwenye Muungano ili wapiganie kujitenga kwa Zanzibar! Haiwezekani upande mmoja wanafurahia matunda ya Muungano wakati huo huo hawautaki!
Mwanakijiji,
Ni vizuri kabla kuandika lolote ni vizuri usome katiba zote mbili ili kujiridhisha na kuweka hoja iliyo na mashiko. Na hata unaposoma Katiba moja basi isome vizuri sana na kuona Mamlaka ya rais wa Znz na serikali yake. Kumbuka kuwa kuna ibara maalum inayotambua na kutambulisha uwepo wa Rais wa Znz na Serikali yake. Lakin vile Katiba ya muungano imebainisha kwa ibara maalum uwepo wa Baraza la wawakilishi Znz na shughuli zake.
Nakushauri zisome ibara hizo kisha lete hoja zake. Kwani kuleta hoja kwa kusoma ibara nusu nusu hakuleti maana kwa wanaokusoma na kuleta mtafaruku na kwa watu makini watakuona kama mchochezi.
Lakin vile vile ukisoma Ibara ya kwanza ya katiba ya Znz imejibainisha wazi kueleza eneo la miliki ya Znz na limebainishwa wazi hapo.
Na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:
1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"
Vile vile kumbuka Znz sio wanafiki kwani hata rasimu ya katiba ya Muungano iliyopelekwa kule na Bunge la Muungano ilichanwa hadharani bila kificho kitu ambacho Tanganyika hawakuthubutu kukifanya ila walibaki kughumia tu.
lakin pia wa Znz wapo huru kuujadili muungano kwa mapana yake kuliko Znz. Naweza kusema kuwa mwenye uthubutu wa kusema Muungano ndani ya Bunge ni Tundu Lissu tu wengine woooote wanafiki na waoga wa kuujadili.
Ni vizuri ufikie pahala kuona Bara kuwa kuna ombwe kubwa sana la uongozi sababu kubwa ni kuogopana na unafiki wa baadhi ya watu hususan viongozi. Zanzibar ipo huru.
nafikiri mawazo yako uliyotoa umetoa kwa mfano wa Bara na kuinasibisha Znz kimakosa ima kwa kukusudia ili kuhalalisha mada yako.
Labda nikuulize suala lililopo mezani wewe unalitazamaje? pitia katiba zote kujua mipaka ya kila wizara husika kabla kuleta hoja.