Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

usiwe kilaza wewe!!!!!!!!!! Hivi mnataka hiyo bahari ambayo haina mwenyewe ichukuliwe na ndugu zenu waarabu? Unataka kutupotosha tujue kwamba Bunge la Jamhuri ni la Wabunge wa iliyokuwa Tanganyika peke yake?? Hampati kitu!!!!

Msipoangalia tutaanza kuwachunguza uraia wenu!!!!!!

Labda turejeshe pasi ya kusafiria kuja na kwenda Zanzibar?
 
Nimeshindwa Kuelewa wa Znz wanataka nini hasa?
1. Je hawataki mama tibahijuka kupeleka maombi ambayo nao Kama part ya JMT watafaidika??Au hawakubali Kama wao ni sehemu ya Tanzania ?
2. Je hawakubali lolote linaloamuliwa na Tanzania wao wakiwa part ya muungano ? Nadhani wanatakiwa Kuwa wazi kwamba hawahutaki muungano basi?


Kwa Kweli nashindwa Kuelewa nini hasa Tatizo Lao? Naomba kusaidiwa...

Kwa ufupi ni kuwa hawataki kufanyiwa! Jee hilo ni kosa kwako?
Jee Muungano kwako una maana kuwa mmoja ndio awe muamuzi wa mwenziwe? Kwako huo ni Muungano au kunyanganyana?
 
juggle.gif
KATIBA YA SASA YA ZANZIBAR
Ibara ya 3 na 4 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar inasema hivi:canada:

"Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

Vilevile, Ibara ya 4 ya sheria ya mabadiliko ya katiba inasisitiza, "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."


Ibara mpya ya 26(1) inayounda "Afisi" ya rais wa Zanzibar inamtaja rais wa Zanzibar kama "… Mkuu wa nchi ya Zanzibar…"
Ibara mpya ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa rais wa visiwa hivyo mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Ibara mpya ya 24(3) ya katiba ya Zanzibar inasema, kutokana na maombi yanayopelekwa mahakamani kuhusu masuala ya haki za binadamu, uamuzi wa mahakama Kuu ya Zanzibar "… utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania."
juggle.gif
 
Mimi kama ni Mtanganyika mwenyi kutii dini yangu sitopenda kufanya uadui kwa ndugu zetu wa Zanzibari kuwaingilia katika nchi yao wakati ukweli tunaujuwa kama Zanzibar ni Nchi hata na katiba ya nchi yao inasema hivyo hivyo!!!

Watanganyika wenzangu nakwambieni huu Muungano ni wa longo longo hilo tukubali!!!
Ni bora tupiganie Taifa letu la Tanganyika kuliko kudangwanywa na muungano huu FAKE😛oa
 
Mimi sielewi msingi wa malalamiko ya CUF kwani eneo linaloombwa kuongezwa kwa sasa liko ndani ya mipaka ya Zanzibar au ni eneo huru kwa mujibu wa sheria za kimataifa? Pili, kule UN kuna Taifa linaloitwa Zanzibar na tatu hili ombi likikubaliwa si Zanzibar watakuwa na eneo pana la kufanya uvuvi?

Kwanza elewa kuwa hili si la CUF bali ni la Wazanzibari wote na kwa maana hiyo hata CHADEMA kama wanataka wanachama Zanzibar wajuwe kuwa huo ni msimamo wa Wazanzibari bila kujali Chama.

Ama hili la pili ni kuwa eneo linaloombwa ni eneo ambalo linaendelea baada ya kuishia eneo la sasa la Zanzibar. Kwa maana hiyo Tanganyika haima haki ya kudai sehemu hiyo na ndio maana wakatumia jina la Tanzania wakati Katiba au makubaliano ya Muungano yanatambuwa mipaka ya zanzibar. Kitendo hiki bila ya kushirikisha Zanzibar kingekuwa sawasawa na kuomba eneo la bahari baada ya kupita mipaka ya Commoro.
 
Wenzetu kazi ya kupiga domo hamjambo.
Hata mkisaidiwa kufikiri mnalalamika utafikiri dunia inaisha kesho!
Hata Nyerere aliwahi kusema angekuwa na uwezo angevivuta visiwa hivi mbali kabisa na Tanganyika.
Kwamba tumeshawachoka na maneno maneno ni dhahir , taadhali jitangazieni uhuru tujue moja.

Nafikiri wa maneno ni nyie! Kwani si tumeshasema kuwa hatutaki mali asili zetu kuwemo ndani ya Muungano? Mbona hili sasa linakuja, hivyo nani mlalamishi na nani mdomo mtupu iwapo mmeshachoka nasi?
 
Mkuu unajichanganya kwa hili. Kosa la Prof. Tibaijuka lipo wapi? Mbona mnapenda kucomplicate mambo? Chuki haitakusaidia. Be realistic hizi njozi za mchana zitakuumiza bila sababu. Hakuna nchi inaitwa Zanzibar. Hata UN watawashangaa actually so far wanawashangaa. Acheni kuwapotosha wananchi kwa propaganda zenu kwa kujineemesha wenyewe kwa chuki zisizo na msingi wowote. Tanzania
ni ya watanzania wa bara na visiwani.[/QUOTE

WAZANZIBARI WENZETU WANAPIGANIA KULIRUDISHA JINA LA NCHI YAO NDANI YA UNITED NATION
]
images

Zanzibar ikiwasilishwa katika umoja wa mataifa 1963

KAMA WEWE NI MTANGANYIKA HALISI BASI IJUE HISTORIA YA NCHI YAKO KULIKO KUBERULIWA BERULIWA
TUU NA MAJACUC:focus:



 
Ph.D holder huyo. Sasa ukutane na mvuvi ndiyo utatoa machozi. Hivi hao akina Jussa kwanini wasipeleke kwenye baraza la wawakilishi hoja ya kuuvunja muungano badala ya kubaki kuchokonyoachokonyoa tu na kukuza vitu ili Zanzibar ionekane inaonewa kwenye huu muungano?

Alileta Jumbe yakamkuta ya kumkuta.

Waliileta G55 kudai Tanganyika ikasambaratishwa!

Wawakilshi walishasema maliasilizetu si za Muungano, sasa limekuja hili la Tibaijuka!

Hebu kwa akili yako twambie tufanye vipi ili mtuelewe?????
 
Huyo jamaa ni mnafiki kiasi kuwa hata shaitwani mwenyewe anaweza asimfikie kwa unafiki! Hapa ataitaja Chadema, atamtaja Slaa lkn hutaona anaitaja ccm wala kikwete!! Mtawatambua kwa matendo yao!! Na huyo huko kwao ni 'msomi' anaongelea madudu (kama kweli yapo) ya serikali ya ccm, lkn anailaumu Chadema!!! Jiulize utegemee nini kutoka kwa wavuvi wao masikini wasio na elimu waliozoea kukaririshwa tu mambo na 'wasomi' wao!!! Balaa duniani...



Hongereni kwa usomi wenu! Kina Dewji, Sabodo na wahindi wengine wanakutawaleni.
 
Katika msafara wa kwenda UN walikuwepo waziri Shamhuna na katibu mkuu wa wizara yake, kwahiyo ni dhahiri kwamba SUK Zanzibar ilishirikishwa. Sasa hizi propaganda za ccmB kuwaambia wapemba wawe tayari kufa wakati walikufa 2001 na wengine wamekuwa wakimbizi hadi leo bila msaada wowote, pamoja na cuf kuingia serikalini bado imeshindwa kuwasaidia waathirika wa mauaji ya jan.2001, sasa tena anataka kuwadanganya nini wapemba??

UN ikikubali na kuiongezea JMT eneo hilo kama lilivyoombwa, then SUK Znz kama watakuwa hawajaridhika na kipande walichogawiwa wanaweza kuendelea kuzungumza na wenzao wa JMT, lakini kushauri kwamba zoezi lisistishwe, ama kusema ccmB watakwenda UN kuitaka isituongezee hilo eneo lililoombwa huo utakuwa ni ufinyu wa mawazo.

Mwisho, Barubaru wewe ni msaliti wa wazenjiberi wenzako, leo unajifanya kuwa na huruma nao, kama bado unaipenda zenji si urudishe uraia wa omani na kuomba kurudi nyumbani? kwanini kila siku kuongelea mambo ya Tanganyika wakati ulishaamua kujilipua na sasa wewe ni mwarabu wa omani?
Wakati unaposhauri Prof. Tibaijuka kwa kupigania maslahi ya JMT ungeutumia vizuri muda huo kumshauri mwanaccB mwenzako, waziri wa miundombinu wa zenji ajiuzulu kwa uzembe wa kuisimamia wizara yake hadi kuruhusu meli chakavu kubeba wapemba wenzako na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1300. Kama huna uchungu na wale wapemba wenzako zaidi ya 1300 basi wewe ni zaidi ya mnafiki.

Ama wewe kwa kuchupia chupia! Sasa inahusu nini kuleta yasiyojiri hapa! Hivyo nawe si mnafiki wewe? Toka lini ukasapoti Serikali yaCCM na Mawaziri wake? Wacha unafiki, sijakuona hata siku moja ukapongeza kilichofanywa na CCM leo imekuwaje?
 
nimeamini leo kwamba zanzibar si nchi.[/QUOTE

WAZANZIBARI WENZETU WANAPIGANIA KULIRUDISHA JINA LA NCHI YAO NDANI YA UNITED NATION

images

Zanzibar ikiwasilishwa katika umoja wa mataifa 1963

KAMA WEWE NI MTANGANYIKA HALISI BASI IJUE HISTORIA YA NCHI YAKO KULIKO KUBERULIWA BERULIWA
TUU NA MAJACUC:juggle:

 
Naomba niweke wazi mipaka na nchi yetu kama ilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977.

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:

1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

KGBNcMDacOJvbN49x3WKL

Kwa tafsiri ya kisheria ni kuwa eneo la Zanzibar ni kama lile lililokuwepo kabla ya kuungana (1964), yaani maili 12 za majini kutoka ufukweni mwake. Na kwamba haina haki ya bahari kuu na eneo la EEZ maili 200 kutoka ufukweni, kwani mataifa yanayopakana na bahari yameipata mwaka 1982 wakati Makubaliano ya Sheria za Bahari yalipofikiwa.

Ni vizuri watu kama wakina Jussa wafikirie vizuri kabla ya kuzungumza masuala kama hayo. Ni lazima ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa Zanzibar si nchi kwani nchi hiyo hii ndani ya JMT ambaye ni mwananchama wa Umoja wa Mataifa na mwenye haki ya kuomba haki na upendeleo wa Makubaliano ya Sheria za Bahari ya Mwaka 1982.


Zanzibar iwe ni nchi au la kwa tafsiri yako haimaanishi kuwa Jumuiya ya Kimataifa hawatambui kuwepo kwa sehemu inayoitwa Zanzibar.

Sijui kwa uielewa wako wa mambo ya kimataifa kama unaelewa suwala la haki za kibinaadamu ni suwala amalo kila mwanachama wa UN ametia sahihi na ndio maana ukaona kuwa UN inaingilia kati migogoro ya haki za minority, suikwambii kuwa UN inatambuwa kuwa Tanzania ni Muungano wa Sehemu mbili.


Sasa nduhu yangu ukizania kuwa Jumuiya ya Kimataifa itakaa kimya kwa kuvunjiwa haki ya Zanzibar eti kwa kuwa si mwanachama wa Unu nafikiri umekosea sana.


Ningeomba ukumbuke suwala la kisiasa la Zanzibar jinsi lilivyoingiliwakati na jumuiya za Kimataifa.

Halafu nyinyi ndugu zetu mnasahau mapema kuwa kulikuwa na nchi kama urusi, Chekoslovakia, Eritrea kwa hapa Afrika na Sudan ya Kusini, Jee hizi zilitokana na nini? Sikwambii Muungano wa hiari.
 
Mwakalinga na Wana JF,
siku zote mpambe ndio ana sauti kuliko hata ya Boss, ni watu wachache sana wanaopinga Muungano huu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ila kama wote wataamua kuukataa hata kama wanasema tuliungana ki-mkataba na sio ki-katiba sawa sisi Watanganyika hatutakuwa na la kupinga.
My take: Sisi wote ni Ndugu, Watanganyika, Wazanzibar, Wapemba wote wamoja, hivi hakuna mwenye Mkataba huo wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ??? atuwekeee tuuchambue
Nawakilisha

Nadhani wewe unachotaka kuelezea ama kushawishi hapa ni upupu mtupu.Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika sasa waziri wa Tanzania anapokuwa hana mamlaka Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni nchi,hoja yako inakosa mwelekeo.

Huwa najiuliza hivi watu kama ninyi na hao kina Jusa mnasiri gani dhidi ya wananchi! .Mtazamo wangu wananchi wanahitaji huduma bora za jamii na usalama wa maisha yao .Ila wote mnaoleta hizi chokochoko ni waroho wa madaraka, badala ya kuishauri na kuikosoa serikali kuweka uwiano wa matumizi ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi,ninyi mpo majukwaani mkidai Zanzibar ni nchi.Mnachokitaka hakitakaa mkipate kwa sababu wengi wenu hamjui mnachohitaji.

Halafu ningewashauri wewe na hao wapiga debe wenzako kina Jusa kipindi hichi cha kubadili katiba ndio muafaka kuweza kuweka mambo sawa kwa yale yote mnayoona ni kikwazo.Ila kutokana na kuwa mna ajenda zenu za siri mnatanguliza matakwa yenu binafsi badala ya matakwa ya wananchi.

Hiyo ardhi /bahari inayoongezwa ni ya Tanganyika ama Tanzania! kwanza hiyo Tanganyika haipo sasa sijui kinachowapandisha majukwaani na kupaza sauti kama vile nyie sio watanzania.Wapemba wanaofanya biashara Kariakoo na kusaidia ndugu zao walioko Zanzibar isingekuwa huu muungano unafikiri mambo yangekuwaje! .Nadhani ni vyema kuleta hoja zenye/zilizofanyiwa utafiti na sio kutoa hoja kutokana na hulka za mrengo wa kivyama.
 
Naomba niweke wazi mipaka na nchi yetu kama ilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977.

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:

1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

KGBNcMDacOJvbN49x3WKL

Kwa tafsiri ya kisheria ni kuwa eneo la Zanzibar ni kama lile lililokuwepo kabla ya kuungana (1964), yaani maili 12 za majini kutoka ufukweni mwake. Na kwamba haina haki ya bahari kuu na eneo la EEZ maili 200 kutoka ufukweni, kwani mataifa yanayopakana na bahari yameipata mwaka 1982 wakati Makubaliano ya Sheria za Bahari yalipofikiwa.

Ni vizuri watu kama wakina Jussa wafikirie vizuri kabla ya kuzungumza masuala kama hayo. Ni lazima ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa Zanzibar si nchi kwani nchi hiyo hii ndani ya JMT ambaye ni mwananchama wa Umoja wa Mataifa na mwenye haki ya kuomba haki na upendeleo wa Makubaliano ya Sheria za Bahari ya Mwaka 1982.


Sasa kwa hiyo Tanzania yako ufukwe unaanzia wapi? Kigamboni au Makunduchi au Kigomasha???? Kazi kwelikweli!!!!
 
Hivi kuongezewa eneo kwa ajiri ya uchumi wa nchi na kuimarisha ulinzi halikuwa swala kufanya mjadala wa kitaifa kwanza ndio tuchukue uamuzi, Mama Prof. Timaijuka kafanya kwa usahihi kabisa kufanya alivyo fanya. Au ulitaka pesa za walipa kodi zipotee tena kwa ajili ya kuratibu maoni ya raia juu ya kuomba kuongezewa eneo nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kama alivyo sahihi JK na kupoteza pesa kwa kuulizwa wannchi nani aunde Katiba!!
 
Barubaru,

..Makamu Mwenyekiti wa Tume iliyofanyia utafiti wa suala hili ni Mzanzibari.

..Ujumbe wa Tanzania uliowasilisha ombi letu UN yupo Afisa toka serikali ya mapinduzi Zanzibar, na Mama Zhakia Meghji ambao ni Wazanzibari.

..Hata sasa hivi tunavyozungumza Naibu Balozi wa Tanzania UN ni Mzanzibari.

..Zanzibar kama "nchi" isingeweza kuwasilisha ombi hilo kwasababu haitambuliki UN. kinachotakiwa kufanyika ktk mazingira haya ni kusubiri kwanza ombi hilo la kuongezewa mipaka ya bahari lipite. Baada ya hapo SMZ na SMT zinaweza kukaa na kuchanganua mgawanyo wa eneo lililoongezeka kwa kuzingatia mipaka ya Zanzibar na Tanganyika.



Jee hili la kutakiwa Shamuhuna ajiuzulu nalo unalijuwa? Viongozi wa Zanzibar walishirikiana na mafisadi kwa tamaa zao na wananchi sasa wanachachamaa kuwa hawataki ufisadi. Na aliyekwambia Zakia Meghji ni Mzanzibari nani? Hivyo kuzaliwa pahala ndipo kunakokufanya raia iwapo hutaki kuwa Raia. Kina Zakia ni hao hao Mafisadi basi na walitumiwa ili kama unavyofanya wewe ionekane kwa Wazanzibari walikuwamo basi!
 
Mkuu unajichanganya kwa hili. Kosa la Prof. Tibaijuka lipo wapi? Mbona mnapenda kucomplicate mambo? Chuki haitakusaidia. Be realistic hizi njozi za mchana zitakuumiza bila sababu. Hakuna nchi inaitwa Zanzibar. Hata UN watawashangaa actually so far wanawashangaa. Acheni kuwapotosha wananchi kwa propaganda zenu kwa kujineemesha wenyewe kwa chuki zisizo na msingi wowote. Tanzania ni ya watanzania wa bara na visiwani.

Naam leo hawaijuwi lakini pale walipomshinikiza JK na Serikali yake juu ya Zanzibar ulikuwa wapi? Sawa UN hawaitambui Zanzibar jee wewe kimwana pia huitambuwi? Hebu niambie Desemba 9 ulisherehekea nini, Januari 12 Kikwete alikaribishwa kwenye nini na April 26 utalala nyumbani kwa sababu gani? Sasa hapo jiulize nani anajichanganya au labda werwe unachanganywa?
 
CUF na siasa zao za msimu,lol! Siku hizi hawana cha kuongea. Wamevamia meli inayoutwa muungano, ili tujue nao bado wapo.

Kumbe CCM ina mazuri yake!!!! Au ndio ile ndowa ya juzi kule Ikulu?
 
Sera ya CUF ni kuvunja muungano tangu zamani. Lakini ni ukweli kabisa kuwa Jusa ni msemaji wao mkuu ambaye mara nyingi nashindwa kutafakari na kupima anayoyaropoka. Maalim Sefu kwa sasa hatamani sana kujiweka mbele kwenye hili. Hata hivyo wazanzibari wasiopenda muungano asilimia kubwa ni wapemba matajiri, wenye uhusiano na uarabuni wakisaidiana na na wale matajiri na wenye madaraka serikalini wa Unguja. Lengo kubwa ni manufaa yao ya binafsi ambayo kwa kiukweli ni kuona karibu na pua zao tu, mafanikio yao kiuchumi yanategemea sana bara.

Tanzania inatakiwa iwe nchi moja na wala siyo tatu
Sera ya Chama Chako inasemaje???
 
si na wao waende wakaombe kama ni nchi? kwanini wapige kelele?waende UN wakaombe wapewe kama nchi sio kama sehemu ya muungano. full stop. braza Barobaro mi nafurahi mnatusaidia kuipata Tanganyika yetu. Hapa wala hatutatumia nguvu na bado mtalalamika kuwa mmefanya tanganyika imerudi pasipo watanganyika kuidai


Tatizo ni kuwa Tanganyika haina masafa makubwa ya bahari muelekeo wa Zanzibar hivyo huo wanaotaka kufanya ni wizi. Eti kuomba kwa kuwa kitu ni cha mdogo wako basi si umshauri kwanza?
 
Back
Top Bottom