Kwa kuwa ni msomi tena wa ngazi zote tatu sidhani kama hauelewi kodi ni nini na zinalipwa kwa sababu gani. Wapo Watanzania wengi tu ambao wazazi wao walilipa kodi kama hao wazee wako lakini wewe ukachukua nafasi yao. Ukasoma wewe chuo kikuu huku ukijifanya Mtanzania!Kumbuka kuwa kwa biashara alizokuwa wanafanya wazee wangu basi kodi yake ingetosha kusomesha watoto zaidi ya wanane hadi Chuo kikuu lakin sie tumesoma watatu tu. Na watano wengine tumechangia kwa jamii nyingine kama wewe wenye dhana ya kuwa kuna cha bure duniyani.
Turejee kwenye Mada.
Je Znz itanufaikaje na hicho kilichooombwa na Prof Tibaijuka?
Kama hakuna namna kwanini BLW wasihusike katika kadhia hii nzima?
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Kunufaika ni lazima kama ambavyo imenufaika na mengine mengi tangu mwaka 1964 likiwemo la wewe kusoma chuo kikuu cha Dar bure!
BLW litaarifiwa tu muda ukifika. Mambo bado yako ngazi ya serikali. Mbona unasahau kuwa kuna WABUNGE wa Zanzibar kwenye Bunge la JMT? Au wenye akili na uchungu kwa "nchi" yao ni wajumbe wa BLW tu?