Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

kwani mafuta waliyokuwa wanayazungumzia zanzibar ndiyo hayo waliyotaka kuja kuyachukulia kwa mlango wa nyuma? kama ni hayo basi imekula kwao, eneo ndiyo linaombwa na litaongezwa na kuna mifuta bwelele.
 
naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la muungano na ndio maana znz kuna waziri wa wizara hiyo na bara yupo.

Kumbuka kuwa mamlaka ya tibaijuka mwisho wake ni chumbe akiwa znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. Hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya znz. Kwa msingi huo katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la znz kiufasaha kabisa. Sasa kwa ombi hilo la tibaijuka ni lazima katiba ya znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima blw litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika picha walopiga kule un wakti wanawakilisha alikuweo tibaijuka, balozi wa tz katika un, mbunge wa mafia na katibu wa wizara kutoka znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi prof tibaijuka alipata baraka zote za bunge la muungano dio maana akachukua muwakilishi wa bunge.

Sasa upande wa blw hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima blw litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la znz.

Sasa labda tujiulize.
Je znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? Hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa tz na znz zote zinaongozwa na rules of law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani serikali, bunge na mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji serikali ya znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa tz kujiunga na oic.


kumbe wewe ndio jussa?
 
Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.

Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.

Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.

sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.

Nadhani wewe unachotaka kuelezea ama kushawishi hapa ni upupu mtupu.Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika sasa waziri wa Tanzania anapokuwa hana mamlaka Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni nchi,hoja yako inakosa mwelekeo.

Huwa najiuliza hivi watu kama ninyi na hao kina Jusa mnasiri gani dhidi ya wananchi! .Mtazamo wangu wananchi wanahitaji huduma bora za jamii na usalama wa maisha yao .Ila wote mnaoleta hizi chokochoko ni waroho wa madaraka, badala ya kuishauri na kuikosoa serikali kuweka uwiano wa matumizi ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi,ninyi mpo majukwaani mkidai Zanzibar ni nchi.Mnachokitaka hakitakaa mkipate kwa sababu wengi wenu hamjui mnachohitaji.

Halafu ningewashauri wewe na hao wapiga debe wenzako kina Jusa kipindi hichi cha kubadili katiba ndio muafaka kuweza kuweka mambo sawa kwa yale yote mnayoona ni kikwazo.Ila kutokana na kuwa mna ajenda zenu za siri mnatanguliza matakwa yenu binafsi badala ya matakwa ya wananchi.

Hiyo ardhi /bahari inayoongezwa ni ya Tanganyika ama Tanzania! kwanza hiyo Tanganyika haipo sasa sijui kinachowapandisha majukwaani na kupaza sauti kama vile nyie sio watanzania.Wapemba wanaofanya biashara Kariakoo na kusaidia ndugu zao walioko Zanzibar isingekuwa huu muungano unafikiri mambo yangekuwaje! .Nadhani ni vyema kuleta hoja zenye/zilizofanyiwa utafiti na sio kutoa hoja kutokana na hulka za mrengo wa kivyama.
 
zanzibar ni wapi, na nchi ya muungano ndo ipi inayotaka kumega eneo la zanzibar? Mamlaka ya rais wa JMT ni yapi?
 
Hakika Jusa wewe ni shujaa sana kwa kuliona hili kwani kuna dhulma kubwa sana ilitaka kufanyika hapa. Ikiwemo ile ya kumega eneo la bahari kwa Znz na kuitumbukiza katika Muungano.

Lazima kieleweke na Prof lazima aondolewe hapo. Kwani ubabe hauna nafasi kwenye sheria. lazima sheria zifuatwe.

Nimelipenda hilo neno. Rarely huwa linatumika kuelezea hisia kali mtu alizonazo. Ila kwa kumwambia Prof ajiuzuru ni kumuonea. She did not go there as Prof Tibaijuka trust me
 
Hao ndio wajukuu wa Sultani wamewambukiza mpaka wamatumbi nao wameingia kwenye kukana bidii za kukombooa Nchi yao,iliyokombolewa kwa mkono wa Okello mmatumbi mwenzao.Wanzanzibar shida sana, najua tuliovijana sasa hivi kuna siku isiyo na jina uko mbele ya safari wakisha toka kwenye utwala hawa wazee wanaongangania Muuungano tutawapa Ultumatum kuchagua wawe watanzania Zanzibar iwe Mkoa au Tuwaache wakaishi wanavyotaka.Na wale watakaao amua kuwa Watanzania watabaki Tanzania wtakao amua kuwa Wanzanzibar kwaheri hivyo hivyo kwa Wamatumbi walio Zanzibar wakitaka kuwa Wanzaibar hay wachague wakiataka kuludi Tanzania karibu waachane na Uzanzibar.

Hakika Watu hawa hawatachukua muda watanyukana tu,sasa hivi wanataka hayo kwa sababu ya msukumo wa kuapata nafasi za utukufu wa madaraka na si vinginevyo.Nje ya tamaa hiyo hakuan la msingi mpemba ni mpemba na munguja ni munguja tena HAWAPENDANI KAMA NINI.

Sasa hivi hii ni tamaa za viongozi aina ya JUSSA wakisaidiwa na WAFITISHINAJI ambao hapo zamani walionekana ndio wanaitakia mema Tanzania kupitia CCM walipopata PESA NA POWER kwa njia haramu sasa wanawachezesha viongozi wetu SINDIMBA kwa mapigo ya KIPEMBA.Wanajua sasa kuwa tayari Bara kumeshanuka na wakati wowote chaweza kutokea cha kutokea sasa lililopo kwa sasa ni kuengineer mchezo mchafu wa Zanzibar kuwa Nchi kisha wakimbilie huko kujificha chini ya kivuli cha undungu wa kufanana rangi.
 
Mamlaka ya JMT ni kamili. Eneo la jamhuri ya Muungano ni eneo zima la bara na visiwani. Hakuna eneo lolote la 'nchi ya Zanzibar' ambalo si eneo la JMT. Kama lipo niambie. Katiba ya ZNZ inaweza kusema lolote lakini ikipingana na ile ya Muungano vipengele vyake ni batili. Zanzibar ni nchi kwa Wazanzibari tu; siyo nchi inayotambulika mahal popote duniani. Kuwa na jeshi, mahakama, na rais (mihimili mitatu ya dola) hakuifanyi ZNZ kuwa nchi vinginevyo miye ningetamba niko "nchi" ya Michigan! Kuongeza eneo la bahari kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar na kwa Tanzania nzima. Wananchi wa ZNZ yawapasa wafurahi na kuunga mkono uamuzi huu wa serikali ya JMT.

Naomba nikuweke sawa kidogo.

Nilipo RED ni sahihi kabisa. Lakini kumbuka Nchi hizi mbili huru yaani Znz na Tanganyika zimeungana kimkataba. Na kilichomo kwenye mkataba ndicho kitu cha muungano na kilicho nje ya hilo sio kitu cha muungano.

Nimebainisha Suala la Ardhi na makazi sio suala la muungano kwani hilo halimo kabisa kwenye mkataba wa muungano.

Lakin pia ukisoma Katiba ya JMTz imelikubali hilo na inazungumzia mambo ya makubaliano ya kimkataba tu na Znz na yaliyo nje ya makubaliano ya mkataba hayo yatakuwa chini ya SMZ kama suala la Ardhi na makazi. Na kwa mantiki hii Znz kuna waziri kamili wa Ardhi na makazi na Bara yupo pia.

Mamlaka ya Tibaijuka mwisho ni Chumbe. hana mamlaka yoyote Znz kwani hatambuliki huko Kikatiba si ya muungano wala ile ya Znz. Mipaka yake ni kwa eneo la Tanganyika (Tz Bara).

Kwa mantiki hiyo inapogusa eneo linalohusu jambo ambalo haliko kwenye muungano ni lazima ashirikishe upande mwingine wa muungano kwa kila hatua kama alivyoweza kulihusisha bunge na mwakilishi wa bunge umemuona hapo juu Mbunge wa mafia. Sasa upande wa Znz vipi.

Tuwe na subra kwani shamuhuna yupo kikaangoni saa hizi huko Barazani na hapo ndipo way forward itakapojulikana. Kwani kwa namna yoyote kuna dhulma hapo inataka kufanyika na kuihujumu Znz kiuchumi na eneo.

Tuvute subra. Lakin tumpongeze Jusa kwa kuangalia mbali na wawakilishi kutanguliza utaifa mbele katika kutetea maslahi ya Znz.

 
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi moja inayotambulika kimataifa halafu kuna kijisehemu kidogo ndani ya JMT inayojulikana kwa jina Zanzibar ukipenda unaweza kuita Wilaya,Mkoa au Nchi isiyotambulika kimataifa.
 
Nadhani wewe unachotaka kuelezea ama kushawishi hapa ni upupu mtupu.Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika sasa waziri wa Tanzania anapokuwa hana mamlaka Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni nchi,hoja yako inakosa mwelekeo.

.

Acha upofu wa kutosoma katiba yako vizuri.

Nitakujibu kwa kifupi na kwa kutumia mifano halisi labda utazinduka.

waziri wa Ardhi na makazi muungano ni Prof Anna Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi na makazi Znz ni Mh Ali Juma Shamuhuna.

Waziri wa Afya na Ust wa Jamii Muungano ni Dr Haji Mponda
Waziri wa Afya Znz ni Mh Juma Duni.

Je unalijua hilo? Na unajua mamlaka yao wote hapo juu.

tafakati kabla kukurupuka na kuleta hoja.

watakucheka wenzakoo wewe.

 
kama OIC ilizimwa na Muungano kwanini na hili lisizimwe.

Tibaijuka amechamke lazima ajiuzuru tu hakuna mjadala.

Watu wengine sijui wanafikiri kwa kutumia masuburi? umeambiwa mchakato huu ulianza mwaka 2007. Prof. Tibaijuka amekuwa waziri tangia 2010. Pili hili jambo liweze kwenda UN lazima liliridhiwe na baraza la mawaziri, ambalo mwenyekiti wake ni Rais JK na rais wa Zanzibar ni member kama waziri asiye na wizara maalumu.

Kwa mukhutada huo kwanini Tibaijuka ajiuzuru na siyo JK au Shein aliyeshindwa kuitetea ZNZ kwenye kikao cha baraza la mawaziri?!

Acha masaburi bana! OIC na EPZ wapi na wapi, I guess baada ya hapa utaifananisha EPZ na Vatican?
 
zanzibar ni wapi, na nchi ya muungano ndo ipi inayotaka kumega eneo la zanzibar? Mamlaka ya rais wa JMT ni yapi?


Je unajuwa mamlaka ya rasi wa Znz kwa mujibu wa katiba ya muungano?

Mamlaka ya rais wa JMTz ni kwa mambo yote yaliyomo ndani ya mkataba wa muungano na mambo yote yanayokhusu Tanganyika (kwenye katiba yenu wameita Tanganyika kama Tz Bara)
 
Wanapotokea waungwana fulani wakidai Serikali ya Tanganyika irudishwe wanaonekana wachochezi na wasioitakia mema Tanzania. Wazanzibar wanajukwaa la kusemea na kudai haki zao; iweje Watanganyika wasiwe na fursa ama mahali pa kusemea mambo yao?

Mbona Waunguja na Wapemba wamejaa Tanzania Bara na hakuna anayehoji uhalali wa wao kuwepo tena wakimiliki ardhi na rasilimali nyinginezo lakini hilo haliwezekani kwa mtu kutoka Tanzania Bara kwenda kumiliki japo kipande cha ardhi huko Zanzibar.

Tukisema Tanganyika imekuwa koloni la Wazanzibar itakuwa ni uchochezi? Nini uhalali na manufaa ya muungano unaong'ang'aniwa kati ya Zanzibar na Tanganyika kwa Wananchi wake?
 
Watu wengine sijui wanafikiri kwa kutumia masuburi? umeambiwa mchakato huu ulianza mwaka 2007. Prof. Tibaijuka amekuwa waziri tangia 2010. Pili hili jambo liweze kwenda UN lazima liliridhiwe na baraza la mawaziri, ambalo mwenyekiti wake ni Rais JK na rais wa Zanzibar ni member kama waziri asiye na wizara maalumu.

Kwa mukhutada huo kwanini Tibaijuka ajiuzuru na siyo JK au Shein aliyeshindwa kuitetea ZNZ kwenye kikao cha baraza la mawaziri?!

Acha masaburi bana! OIC na EPZ wapi na wapi, I guess baada ya hapa utaifananisha EPZ na Vatican?

Naomba upitie kwanza na kujua madaraka ya Serikali ya Muungano kwa mujibu wa sharia za JMTz. na madaraka ya SMZ kwa mujibu wa katiba ya muungano. Kisha leta hoja zako kabla kuanza kutoa shutuma na matusi.

 
Je unajuwa mamlaka ya rasi wa Znz kwa mujibu wa katiba ya muungano?

Mamlaka ya rais wa JMTz ni kwa mambo yote yaliyomo ndani ya mkataba wa muungano na mambo yote yanayokhusu Tanganyika (kwenye katiba yenu wameita Tanganyika kama Tz Bara)

Je zanzibar au tz bara inaweza kuomba kuomba kuongezewa eneo pasipo kutumia jina la JMT? Rais wa zanzibar ni mtawala ndani ya JMT, Bunge la JMT lina wakilishi kutoka sehem zote za JMT na Zanz ikiwemo
 
Wanapotokea waungwana fulani wakidai Serikali ya Tanganyika irudishwe wanaonekana wachochezi na wasioitakia mema Tanzania. Wazanzibar wanajukwaa la kusemea na kudai haki zao; iweje Watanganyika wasiwe na fursa ama mahali pa kusemea mambo yao?

Mbona Waunguja na Wapemba wamejaa Tanzania Bara na hakuna anayehoji uhalali wa wao kuwepo tena wakimiliki ardhi na rasilimali nyinginezo lakini hilo haliwezekani kwa mtu kutoka Tanzania Bara kwenda kumiliki japo kipande cha ardhi huko Zanzibar.

Tukisema Tanganyika imekuwa koloni la Wazanzibar itakuwa ni uchochezi? Nini uhalali na manufaa ya muungano unaong'ang'aniwa kati ya Zanzibar na Tanganyika kwa Wananchi wake?

Hilo ni wazo zuri lazima kila upande wa muungano kuwa huru kujadili muungano. Ni wazo zuri kuliweka kwenye katiba.

 
Back
Top Bottom