Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC

Ebana hata siju huyu mama kavaa vazi la kiarabu la kiisilam au la kidosi mie simjui ila naamini angekua muisilam mwenye kufata sheria sidhani kama angekubali aende kukaribiana na wanaume namna hiyo Ingekua mitaa sudan kama huyu mama ndo kenda kujichanganya na wanaume bac adhabu yake ni fimbo ashukuru TZ hakuna udini
 
Kwa hiyo unataka kumvua uanazuoni na uprofesa wake kwa ajili ya kimtandio cha yule DC m@l@y@ ? Nyie mbona mnashindwa kufikilia kwa umakini jama

we ndo haufikirii kwa umakini mkuu.DC Kawaje malaya tena?kuweni wastaarab bana huyu ni mama kama si bibi yenu.
 
Yeyote iwe hata huyu!

aisee wana makosa mengi sana; wapo walioanzisha vita visivyo na sababu, wapo waliofanya ufisadi wa kila aina na kuwahukumu watu pasipo haki. Kwenye historia ya Kanisa Katoliki ya miaka 2000 yenye mapapa zaidi ya 260 well utawapata wema humo, na wapo waovu ambao majina yao hata kutajwa hayatajwi tena.

- Papa Alexander wa Sita - alikuwa malaya na womaniser mkubwa katika historia. Alifanya orgy ya makahaba pale Vatican Usiku wa Halloween 1501, tena siyo hivyo alikuwa anapenda zinaa kiasi kwamba alikuwa anazini na binti yake na dada zake wawili!

- Papa John wa Kumi na Mbili - huyo naye alikuwa mwovu na wengine wanasema labda ni mwovu kupita mapapa wote wa historia. Alikuwa muuaji, malaya, na fisadi! Alitawala kuanzia 955-964. Aliwahi kutimuliwa na aliporudi aliwatia mbingu na kuwaua wapinzania wake. Kifo chake inasimulia kuwa alipata upoozaji akiwa juu ya kiuno cha mwanamke!

- Papa Leo wa Kumi - huyu ndiiye ambaye kutokana na ufisadi wake na kupenda starehe alijikuta kwenye reformation ya Luther. Analaumiwa katika historia kwa kutokuwa makini katika kufuatilia matatizo yaliyokuwa yanalikabili kanisa la wakati ule. Alikuwa anapenda mambo yake ya siasa na mahusiano ya nje na kujifurahisha. Mtu mmoja aliandika hivi kuhusu yeye "In the general opinion it was injurious to the Church that her Head should delight in plays, music, the chase and nonsense, instead of paying serious attention to the needs of his flock and mourning over their misfortunes"

So, kwa Mkatoliki yeyote hakuna hofu ya kumsema yeyote kuhusu uovu wake hata kama mtu huyo ni Papa, Padre au Askofu. Ndio maana hata leo hii utaona wale wenye kufanya matendo mbalimbali ya uovu wanafunuliwa na waumini wenyewe. Haijalishi kama ni maaskofu au mapadre.
 
Haya wandugu naomba tujibu maswali yafuatayo:-

1.Katika purukushani za kumkamata muhalifu wa kike na ikatokea shanga,zikakatika,hijabu ikadondoka na saa ikapotea,kitendo hicho ni;
(a)shambulio la aibu
(b)utovu wa adabu wa mkamataji
(c)halali kwasababu bila hivyo vielelezo havitapatikana
(d)si halali kwasababu muhalifu mwanamke inabidi akamatwe na mwanamke na hayupo basi aachiwe'asepe'tu.

2.Polisi wa Tanzania ni wabovu kwa sababu;
(a)hawatumii akili bali hutii amri yoyote kutoka juu.
(b)wanapendelea chama tawala waziwazi.
(c)hawawapendi wapinzani.
(d)(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

3.Kwa kuwahukumu chadema kuwa ni wahuni kabla ya kuwasikiliza Rajabu kiravu ni;
(a)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya uchaguzi.
(b)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya CCM.
(c)msimamizi mzuri wa maslahi ya chama tawala.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

4.DC asiye jua ratiba za kampeni zinazo fanyika wilayani kwake ni;

(a)mvivu anaye pokea mshahara asio ufanyia kazi.
(b)mbumbumbu tu wa kazi ya ukuu wa wilaya.
(c)mbabaishaji tu ambaye ni kielelezo cha ubaya wa kuteua watu kwasababu tu ya ukereketwa wao.
(d)mtu safi anaye fanikishwa matakwa ya chama tawala.

5.Waandishi na wachambuzi wanaoilaumu chadema kwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu;

(a)wanafanya kazi yao vizuri
(b)wanajipendekeza kwa ccm na watawala ili wapate safari na posho.
(c)hawajui walifanyaro kwasababu hawajasoma katiba ya nchi .
(d)mamluki wanao tumiwa na ccm kuvuruga upinzani.

6.Jukumu la kumkamata muhalifu ni la;
(a)polisi pekee.
(b)kila mwananchi.
(c)askari yoyote mwenye magwanda na silaha.
(d)vyama vya siasa.

7.Kama anaye paswa kumkamata muhalifu hataki yaani polisi wajibu wa mwananchi wa kawaida ni;

(a)kumwachia muhalifu aendelee kuvunja sheria.
(b)kumwachia muhalifu aende zake.
(c)kulalamika kwa polisi wale wale wasio taka kukamata.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

8.Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

(a)polisi wasio taka kutenda haki.
(b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
(c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
(d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.

Toa hoja sio vihoja.
Maswali ya chekechea? P'se go direct to your point.
 
Naomba niulize maswali haya:

a. Muislamu ili awe Muislamu safi ni lazima akubaliane na Waislamu wenzake wote katika mambo yote?
b. Muislamu akitofautiana na Muislamu mwingine katika masuala ya kisiasa ni lazima mmoja wao awe anatumikia tumbo au maslahi mengine binafsi?
c. Je Muislamu anaweza kutofautiana hata na viongozi wengine wa Kiislamu katika tafsiri ya misimamo mbalimbali ya kisiasa. Kwa mfano, kama viongozi wa dini wanasema "tufanye hivi" na Muislamu dhamira yake inamuambia "tufanye vile" je asipokubaliana na msimamo wa viongozi Uislamu wake una mashaka?
d. Je ili uwe Muislamu safi ni lazima ukubaliane na usioweza kukubaliana nao?

jibu ni hili hapa uislam umeelekeza jinsi ya kuchagua kiongozi kwasababu uislam ni dini iliyokamilika
 
A:Nichangie kidogo kwa kuweka sawa maana halisi ya tafsiri ya maneno yafuatayo.

1. Vazi la Burqa: Is an envolping outer garment worn by women in some Islamic traditions to cover their bodies in public palces.
(Vazi linakuwa kama joho)

2. Niqab = face veil (Hapa Tanzania wanatumia neno la mtaani ninja)

3. Hijab= Kiarabu ina maana curtain to cover however (Most Islamic legal systems define this type of modest dressing as covering everything except the face and hands in public). The words for a headscarf or veil used in the in Quran are khimār not Hijab.

Ingawa Hijab linatumika kuonyesha kitambaa cha kichwani, tafsiri halisi kama ilivyo hapo juu ni kitambaa kinachotenganisha wanaume na wanawake ili wape hifadhi(privacy) na wala halikutumika katika Quran kuonyesha kitambaa cha kichwani. Neno lliilotumika ni Khimar.

Hata hivyo matumizi yamekuwa yanabadilika kutokana na tafsiri ya jamii moja hadi nyingine na huenda jamii yetu imeamua hijabu iwe kitambaa cha kichwani kama kulivyo na tafsiri tofauti katika nchi nyingine za kiislam.
Imeelezwa kuwa mavazi kama Burqa yalikuwepo zama zaidi kabla ya Uislam.

Kwa mantiki hiyo tunaposema amevuliwa hijabu basi tuangalie maana halisi.

B: Si kweli kuwa hijab(kama tunaikubali kwa maana hiyo) kuwa ni vazi la utambulisho wa mwislam. Inaweza kuwa ni vazi linalosisitizwa kumhifadhi mama wa kiislam lakini si utambulisho kama watu wanavyodai.

Hawa wanaosema tukio lile ni kudhalilisha dini wanashindwa kuelewa kuwa kumshambulia mtu tu ni udhalilishaji bila mavazi yake. Hivyo hoja ingekuwa kumdhalilisha mwanamke ambaye ni kiongozi kwa kuchukua sheria mkononi. Sio kumdhalilisha kwasababu amevaa hijabu vazi la kiislam!!
Hata hivyo mbona kwenye mashitaka halionekani?

Kama Hijabu ni vazi la kiislam basi baibui (abaya) , baragashia, kanzu, kikoi n.k navyo pia.
Je mtu akivaa suti yake ya hariri atakuwa ameasi au amekiuka misingi ya uislam? Je, akina mama wanaovaa mitandio hasa kwenye matukio ya misiba ambao wengine si waislam wakishambuliwa na vibaka ni dini gani itakuwa imeshambuliwa?
Je, wale wazee wa kihaya wanapokwenda kwenye harusi na kanzu na baragashia tunaweza kusema ni waislam?

Hivi ikitokea mzee wa kihaya akashambuliwa kwasababu amefanya uhalifu hapo shambulio litahusu haiba na wasifu wake au litakuwa ni shambulio la dini. Hivi tukimuona mwanamama amevaa baibui na kafumaniwa tutasema amefumaniwa mwajuma au mwislam?
Kule kwetu Tanga mwanamama wa dini yoyote ile hujuzu kuvaa baibui kama tradition.Akishambuliwa tutajuaje kuwa ni mwislamu, mkristo au pagani? Wazee huvaa kanzu na kofia kama ilivyo Lushoto na Upareni, wakikamatwa uzinzi ni dini gani imekamatwa uzinzi hapo.

Sisi ni watu wa ajabu sana tumeagiza majina toka Ulaya na uarabuni, tukafuata taratibu za mavazi yao sasa tumeingiza katika imani zetu na tunaacha kusema juu ya kuchukua sheria mkonini na kulinda utu wa mtu tunaangalia mtu kavaaje.

Ninachosema hapa ni kuwa vazi linatumika tu kama kisingizio cha kuonyesha chuki kama tulivyoona maandamano ya kupinga bei ya sukari yalivyopewa sura ya kuvuruga amani.

Viongozi wa dini ni watu wenye heshima katika jamii yetu,kwahiyo kauli wanazotoa lazima waziweke katika uzani na ulinganifu. Wawe tayari kuzitetea vinginevyo wanadhalilika na hata kudhalilisha umma unaowafuata.

Lau kama wangelaani kitendo cha kumshambulia kiongozi au mwanamke japo kidogo ningewawelewa lakini kutanguliza hijabu ambalo ni vazi lenye stara kwa imani flani ni upungufu wa hali ya juu.
Lakini pia wasiachie hapo wajiulize tatizo lilianzaje?

Kama Hijabu ya mkuu wa wilaya imekuwa ni muhimu sana kuisimamia, vipi machangudoa(ambao wapo waislam na dini zingine) kwanini viongozi hao hawaonyeshi hasira zao dhidi ya uovu huo? Je Hijabu ya mtu mmoja ni muhimu zaidi kuliko mamia ya mabinti wanaonajisiwa chini ya umri na kupata mimba! Kwanini kukatiza mtoto shule aende kuolewa isiwe ajenda ya viongozi hao.
Kwanini iwe hijab ya mtu mmoja na sio mamia ya watu walioko segerea na ukonga wanaoteseka kimwili na kiroho!

Unapokuwa na kundi la watu wamenunuliwa kisiasa ili kucheza karata ya dini ni hatari sana. Waumini wenye imani zao wakemee kuburuzwa na kundi la walafi wachache na wala hakuna mahali imeandikwa uumini uwe na chama gani cha siasa. Hakuna mahali unapopingana na mtu kisiasa ummeasi dini. Kwamba unatakiwa useme uongo na upupu ili uwe muumini safi, utetee hata ujinga ili uwe muumini safi.
Kwamba, atokee mtu awafundishe wafuasi wake chama gani cha kisiasa waegemee. Ukismikiliza mtu wa namna hiyo wewe ni moron!
 
Nafikiri wengi wenu mumejawa na jazba kiasi cha kuwa na chongo katika kuangalia shitaka lilipo.

Ndani ya shitaka hakuna neno dini hapo bali ni kuwa kumdhalilisha kwa kumvua kivazi chake ( Hichi kivazi kinaweza kuwa kanga, Kitambaa cha kichwani, gauni au hata nguo za ndani) Hizi hazihusiani na dini yoyote so long as mwenyewe kwa ridhaa yake alikivaa basi inakuwa kosa kubwa sana mtu mwingine kumvua pasi na ridhaa yake.

Elewa kuwa ni kosa kubwa sana kumvua Sister wa RC kile kilemba chake pasi na ridhaa yake . na vile kumvua singasinga kilemba chake.

nawashauri msichukulie kosa kisiasa bali litazameni kisheria.

lakini pia kwa kuwa shauri lipo mahakamani ni vizuri tukiachie chombo hichi cha mahakama kufanya kazi yake kiadilifu pasi na kuingiliwa na maneno yetu.

Kila la kheir
 
hivi kwanini viongozi wa dini wote kwa pamoja wasikemee mbinu hizi chafu za ccm? au waikatae kabisa ccm bana
 
Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.

Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.

Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.

"Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.

Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.

Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM

Helkopta kukata anga

Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.

SOURCE:MAJIRA

Watu kama wewe Prof. ndiyo aina ya wasomi tunaowahitaji Tz. Tatizo kubwa la uelewa kwa Watanzania walio wengi ndiyo linalowapa CCM urahisi wa kutumia dini kuharibu mapambano dhidi ya uovu ulio katika sura ya ufisadi na ukandamizaji wa haki za Watanzania
 
Sijui kwa nini bakwata hawajajua siku zote wanatumiwa kama dalaja na ccm mambo yanapokuwa magumu na wakisha fanikiwa wanawamwaga.itachukua ndio maana kuana jamaa alishawahi andika makala katika gazeti la mwanahalisi akisema bakwata itakufa siku ccm ikifa alikuwa sahihi kabisa ulingo wa siasa wanazuoni wa dini wanaingiaje hawaoni wanatumika?
 
aisee wana makosa mengi sana; wapo walioanzisha vita visivyo na sababu, wapo waliofanya ufisadi wa kila aina na kuwahukumu watu pasipo haki. Kwenye historia ya Kanisa Katoliki ya miaka 2000 yenye mapapa zaidi ya 260 well utawapata wema humo, na wapo waovu ambao majina yao hata kutajwa hayatajwi tena.

- Papa Alexander wa Sita - alikuwa malaya na womaniser mkubwa katika historia. Alifanya orgy ya makahaba pale Vatican Usiku wa Halloween 1501, tena siyo hivyo alikuwa anapenda zinaa kiasi kwamba alikuwa anazini na binti yake na dada zake wawili!

- Papa John wa Kumi na Mbili - huyo naye alikuwa mwovu na wengine wanasema labda ni mwovu kupita mapapa wote wa historia. Alikuwa muuaji, malaya, na fisadi! Alitawala kuanzia 955-964. Aliwahi kutimuliwa na aliporudi aliwatia mbingu na kuwaua wapinzania wake. Kifo chake inasimulia kuwa alipata upoozaji akiwa juu ya kiuno cha mwanamke!

- Papa Leo wa Kumi - huyu ndiiye ambaye kutokana na ufisadi wake na kupenda starehe alijikuta kwenye reformation ya Luther. Analaumiwa katika historia kwa kutokuwa makini katika kufuatilia matatizo yaliyokuwa yanalikabili kanisa la wakati ule. Alikuwa anapenda mambo yake ya siasa na mahusiano ya nje na kujifurahisha. Mtu mmoja aliandika hivi kuhusu yeye "In the general opinion it was injurious to the Church that her Head should delight in plays, music, the chase and nonsense, instead of paying serious attention to the needs of his flock and mourning over their misfortunes"

So, kwa Mkatoliki yeyote hakuna hofu ya kumsema yeyote kuhusu uovu wake hata kama mtu huyo ni Papa, Padre au Askofu. Ndio maana hata leo hii utaona wale wenye kufanya matendo mbalimbali ya uovu wanafunuliwa na waumini wenyewe. Haijalishi kama ni maaskofu au mapadre.

Mkuu MMMJ,

Papa huyu ndio kiboko

Pope Joan is a legendary female Pope who, it is purported, reigned for a few years some time in the Middle Ages. The story first appeared in the writings of 13th-century chroniclers, and subsequently spread through Europe. It was widely believed for centuries, though modern historians and religious scholars consider it fictitious, perhaps deriving from historicized folklore regarding Roman monuments or from anti-papal satire.

The first mention of the female pope appears in the chronicle of Jean Pierier de Mailly, but the most popular and influential version was that interpolated into Martin of Troppau's Chronicon Pontificum et Imperatorum somewhat later in the 13th century. Most versions say that she was a talented and learned woman who disguised herself as a man, often at the behest of a lover. Due to her abilities, she rises through the church hierarchy, eventually being chosen as pope. However, while riding on horseback one day, she gives birth to a child, thus revealing her sex. In most versions, she dies shortly after, either by being killed by an angry mob or from natural causes, and her memory is shunned by her successors.
 
Majibu kwa Mwanakijiji question!

a. Muislamu ili awe Muislamu safi ni lazima akubaliane na Waislamu wenzake wote katika mambo yote?

Jibu: Lazima akubaliane na mafundisho ya Quran na Sunna za mtume Muhammad.

b. Muislamu akitofautiana na Muislamu mwingine katika masuala ya kisiasa ni lazima mmoja wao awe anatumikia tumbo au maslahi mengine binafsi?

Hapana: ndiyo maana kuna waislamu walioko CUF, CCM na Chadema. Wanaotumikia matumbo ni wale walio tayari kupindisha mafundisho ya Quran na Sunna ili kupata political popularity NJAA mfano Prof. Safari

c. Je Muislamu anaweza kutofautiana hata na viongozi wengine wa Kiislamu katika tafsiri ya misimamo mbalimbali ya kisiasa. Kwa mfano, kama viongozi wa dini wanasema "tufanye hivi" na Muislamu dhamira yake inamuambia "tufanye vile" je asipokubaliana na msimamo wa viongozi Uislamu wake una mashaka?

Jibu: Hakuna tatizo kutofautiana kisiasa ndio maana kuna wana CUF, CDM na CCM waislamu..

d. Je ili uwe Muislamu safi ni lazima ukubaliane na usioweza kukubaliana nao?

Jibu: Muislamu safi ni yule anayekubaliana na Quran na Sunna na ana-practice. waislamu wengi hawakubaliani kwenye mambo mengi ya dunia lakini siyo kwenye mambo ya msingi ya dini.. (fundamentals)

NB: jielimishe zaid acha ushabiki wa kikristo hapa
 
Mzee Wakristu wanapingana na maaskofu wao kila kukicha. Si kweli kwamba wakristu hawawezi kubishana na Maaskofu wao. Kwani Uprotestanti ulianzaje? Wakristu wanaweza kupingana tena hata kwenye mambo ya msingi kabisa ya imani na ya ibada. Hili ni gumu katika Uislamu utaona. Kwamba kuna mambo ambayo yanahusu imani ambayo Waislamu hawawezi kuyabishania na wakabakia kuwa Waislamu.

Lakini la msingi ambalo nilikuwa nahofia ni hilo la Prof. Safari kuonekana anapingana na viongozi wa Kiislamu na tayari watu wengine wameshaanza kumshuku kuwa labda kanunuliwa na wengine hata kuashiria kuhoji elimu yake na siwezi kushangaa kuwa hata imani yake kama Muislamu itaonekana na mashaka. Ndio maana nimeuliza hayo.
Prof. Hapingani na viongozi wa kiislamu ila "Fundamentals of Islam"
Kukubali wahuni kumvua mama wa kiislamu Hijabu yake ni kukubali kuwa wakipata madaraka wataweka sheria ya kuondoa uvaaji wa aina hiyo kama walivyofanya Ufaransa sasa

Kuvua hijabu ni agizo la Allah katika kitabu kitakatifu aache kuganga njaa period

Besides..namhakikishia hapati cheo chadema hata akitaka kujipendekeza vipi...

Tunaendelea kuangali hiyo move itakuwaje..
 
Hajasoma dini, hajagombea, anatafuta cheo cdm kwa sasa...

Nafikiri anafaa sana kuwa "Mwenyekiti wa Chadema" ok

ulivyo muhenga prof safari! ndio maana umejitahidi kumjb mkuu mwana kijj
ila kutokana umetangulza chuki bnafs kwa PROF umeteleza kidogo ungeneutraizi kidogo chuk bnafs ungekuwa umemjibu vzur sana mkuu m/kjj
lakin safi umeza maana mwingine angekuja na jazba mpaka povu lingemtoka mdon.
 
Back
Top Bottom