Kwa mara ya kwanza sasa waTanzania wanaweza kujifunza wao wenyewe kupitia mfumo wa kisheria wa kidijitali unaopatikana simu janja za kiganjani.
Hatua hii imefikiwa kupitia msaada mkubwa wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Haki yaani LSF About LSF – Legal Services Facility kupitia app inayojulikana kama HAKI YANGU na kupakua yaliyo mengi ili kuweza kupata faida ya kuelewa Haki zao zote za msingi, Haki za Binadamu na pia Msaada wa Kisheria Tanzania unafanyika vipi.
Waziri wa sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewataka sasa waTanzania kutumia simu zao janja kujifunza na pia kuweza kupata msaada wa kisheria popote walipo.
Palamagamba Kabudi amesema App hiyo inayojulikana kama HAKI YANGU ni ya kimapinduzi kabisa na kujua haki yake kupitia simu na kujua nani anaweza kumsaidia kisheria bila kusafiri mbali ili kupata taarifa muhimu za haki yake kisheria na wapi aweze kupata msaada wa kisheria.
CEO wa LSF Bi. Lulu Ng’wanakilala amebainisha kuwa wamehudumia jamii kuhusu haki kwa wote kwa miaka 10 sasa na Leo uzinduzi wa App - HAKI YANGU ni muendelezo wa kuwafikia wote kwa urahisi kila kona ya nchi hii kubwa ya Tanzania na kumshukuru waziri kukubali kuhudhuria uzinduzi kama mgeni rasmi katika siku hii muhimu kwa watanzania.
Prof. Palamagamba Kabudi amewashukuru LSF pamoja na wadau wote wa maendeleo wa nje na wengine waliowezesha sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 kufanikisha mfumo huu wa kisheria.