Uelewa wa maswala ya kisheria ni mdogo sana Tanzania

Jukwaa lirudishwe upya

  • Ndio

    Votes: 2 100.0%
  • Hapana

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    2
  • Poll closed .
Jan 28, 2024
41
43
Binafsi nadhani kuna haja ya jambo kufanyika ili kuongeza uelewa wa maswala ya kisheria baina ya watanzania. Najua sheria ni noble professional lakini hii aimaanishi ni wale waliosoma sheria tu ndo wanapaswa kuijua sheria, NO kila raia anatakiwa awe japo na uelewa wa kawaida kuhusu sheria (legal besic understanding).

Tukizingatia sheria ipo katika maisha yetu ya kila siku, Mfano; Makazini (kunasheria za kazi), Mwaswala ya ndoa (kuna sheria za ndoa), migogoro mbalimbali kama vile ya aridhi (kuna sheria za aridhi), mirathi (kuna sheria za mirathi) na maswala ya mikataba (kuna sheria za mikataba) n.k, hivi vyote ni maisha yetu ya kila siku kwaio ni muhimu japo kuelewa sheria ya maswala muhimu katika maisha yetu.

Kuongeza uelewa wa sheria kutasaidia watanzania kujua wajibu na haki zao, lakini pia itasaidia kuwafanya watanzania kuelewa pale haki zao zitakapovunjwa na nini wafanye na wapi waende na ndani ya muda gani ili kuweza kupata haki zao.

Ni aibu kuona watanzania wanashindwa japo kujua mpangilio wa mahakma (court hierarchy system) za Tanzania kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufaa, wanashindwa hata kujua mamlaka tofautitofauti (Jurisdictions) za mahakama izo, isitoshe wengi hudhani Kisutu ndio mahaka kuu ya Tanzania (what a shame). Pia asilimia kubwa ya watanzania hudhani kuwa sheria ni katiba, watu hudhani katiba ndiyo iliyosema kuua ni kosa, hudhani katiba ndiyo iliyosema wizi ni kosa n.k. Na, wengine hushindwa hata kutofautisha kati ya kesi za madai na jinai (unakuta mtu anadai ila anapeleka kesi polisi badala ya mahakamani) ,pia hushindwa kutofautisha kati ya mwanasheria na wakili ama jaji na hakimu na haya yote yanaashiria jamii yenye uelewa mdogo wa maswala ya sheria.

Nadhani kuna haja kubwa ya hili jukwaa kurudi upya na kutoa wigo wa watu kudiscuss juu ya maswala mbalimbali ya kisheria kwani dunia ya sasa imehamia kwenye technology so sidhani kama kuna haja yakufanya mikutano ya kisheria ili kutoa elimu ya kisheria, nadhani majukwaa kama haya ndio yanatakiwa kutumika zaidi ili kufikisha meseji kwa watu wengi zaidi na kwa haraka.

Ni wazo tu lakini wadau​
 
Back
Top Bottom