Huduma ya msaada wa Kisheria kuwa endelevu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mtandao wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria (TANLAP) na Menejimenti ya Legal Services Facility “LSF” jijini Dar es Salaam.

Mhe.Ndumbaro amekutana kujadili masuala ya msaada wa kisheria na ufahamu wa masuala ya sheria ili kuona namna ya kuwa huduma ya msaada wa kisheri inavyokua endelevu.

“Ni vyema mara baada ya kutekeleza Kampeni ya Mama Samia Legal Aid katika mikoa husika ni vyema zikawa endelevu ili wanachi waendelee kupata huduma. Ni vyema TANLAP na wadau wengine wakiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika kutumia Ofisi ambazo zipo katika maeneo husika na kuwezesha migogoro iliyoibuka iweze kushughulikiwa na si kutoitelekeza”

Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa TANLAP imewasilisha ombi kwa Serikali kuendelea kuangalia kwa jicho la ukaribu Sheria zinazuhusu ndoa na mirathi kwa kuwa zimekua zikiongezeka kwa kiwango kikubwa na ipo haja ya Serikali kuongeza rasilimali watu katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Temeke kinachoshughulikia migogoro ya Mirathi na Ndoa.

Katika hatua nyingine, Mhe.Dkt.Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Bi.Lulu Ng’wanakilala, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF.

WhatsApp Image 2023-08-03 at 19.18.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 19.18.33.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 19.18.47.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 19.18.48.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 19.18.49.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom