VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Prof.Makame Mbarawa amewatoa hofu wananchi kwa kuwaambia kuwa hawapaswi kutupa TV zao hata kama 'Digital' itatumika Tanzania nzima.Akizungumza na Radio One leo asubuhi,Prof. Mbarawa amesema cha kuangalia ni kama TV husika ina tundu tatu nyuma yake :nyekundu,njano na nyeupe zinazoruhusu matumizi ya ving'amuzi vya 'digital' toka yale ya zamani ya Analojia.