Prof. Mbarawa: Msitupe TV zenu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Prof.Makame Mbarawa amewatoa hofu wananchi kwa kuwaambia kuwa hawapaswi kutupa TV zao hata kama 'Digital' itatumika Tanzania nzima.Akizungumza na Radio One leo asubuhi,Prof. Mbarawa amesema cha kuangalia ni kama TV husika ina tundu tatu nyuma yake :nyekundu,njano na nyeupe zinazoruhusu matumizi ya ving'amuzi vya 'digital' toka yale ya zamani ya Analojia.
 
Mi nilivyokurupa kuufungua uzi huu nilidhan labda huyo ndugu Makame anataka kutupatia ving'amuz vya chee, kumbe profesa mzima anazungumzia habar za 'matundu', upuuz mtupu.
 
Mi nilivyokurupa kuufungua uzi huu nilidhan labda huyo ndugu Makame anataka kutupatia ving'amuz vya chee, kumbe profesa mzima anazungumzia habar za 'matundu', upuuz mtupu.

anazungumzia AM na FM huyu prof ni mbu lu la kweli inamaana kwa kizaz iki ukanunue tv ambayo aina sehemu ya kuunganishia deki kwanza s
 
Wakuu vp kuhusu DSTV wataingiza local channels au ndo nijiandae kununua king'amuzi kingine
 
Wizara ya Sayansi na Technologia pamoja na Taasisi zake ni "Mzigo"...! Sina uhakika kama kuanzia Waziri mpaka Wakurugenzi kuna mtu ambaye ni "sahihi" kuwa pale...!

Ukienda pale Wizarani unaweza kudhani kuwa umeingia kwenye shule ya sekondari kantalamba...! hakuna anayefahamu nani anafanya nini na kwa nini...!

Kuanzia wataalamu wa "Mkonga wa Taifa"... hadi wataalamu wa "Anwani za Mitaa" - it looks like a "no-man lands"...!

Kikubwa wanachokifanya pale ni mashindano ya "kusafiri"... Leo Waziri yupo uswizi... kesho Naibu waziri yupo Bumbuli... keshokutwa Katibu Mkuu yopo Mbeya... and the trips goes on and on.... SoB...!
 
Haya mambo ya kipya kinyemi yatatugharimu sana watanzania,mimi nadhani analog signal bado ni muhimu sana,Kama watu wenye ving'amuzi startimes na zuku hawafiki laki nne na watu wenye uwezo wa kununua sattellite receiver kwa Tanzania wako wangapi,Sidhani kama kuna wataalam wanaofikiria vizuri na tabia hii ya kufuata maagizo ya wazungu kwamba no analog ni upuuzi,Jaribu kufikiria nchi ambayo ni 18% wanaopata umeme halafu leo unasema no analog signal.Iacheni technologia mpya iiondoe ile ya zamani,kuliko kuondoa ya zamani wakati hiyo mpya watu wengi wataikoso.Je hiyo universal receiver itayokamata local channel zote free itaanza lini.THINK TWICE AND ACT ACCORDINGLY
 
[Ukienda pale Wizarani unaweza kudhani kuwa umeingia kwenye shule ya sekondari kantalamba...!]

Mkuu, tuombe msamaha waliosomea Kantalamba. Huwezi kufananisha mazao ya shule ile na uharibifu unaofanywa na hao wasioweza kutoa dira.
 
Na kama hayana tundu tatu tuna gereji pale sinza kijiweni tunatoboa na kuweka matundu hayo kwa beio chee kabisa
 
aiseeeeeeee babaangu tv yangu ya mbao huku kijijini inatundu moja 2 sasa sijui itakuaje
 
Back
Top Bottom