Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

profesa huyo jaman!!.. ... maoni yangu mtu anpokua na level ya uprofesa bac asipewe mamlaka yoyote yale...,,
source. elimu , cuf, maliasil.....
 
Maghembe hovyo kabisa anamsimamisha Mhifadhi mkuu wakati alikua anatimiza wajibu, huwezi kuwaacha Waganda na Wanyarwanda waendelee kuchunga Ngo'mbe na kuua wanyama wetu kisa kuna zuio ka kukamata Mifugo.
Wabunge wa hiyo kamati nao Wajinga kabisa badala ya kumpongeza Mhifadhi mkuu wanaleta bla bla bla bla.
 
nasisitiza tena ma PRO na ma DR wa Tanzania elimu zao sijui zinawasidia nini ni wachumia tumbo tu, hawana tofauti na yule Pro maji mafupi na Dr mapaka paka
 
Magu hayuko makini katika uteuzi wake na haya ndio matokeo yake.

Historia ya Maghembe alikuwa haijui?Huyu si alikuwa mmoja wa mawaziri mizigo enzi za Kikwete?Haya alikuwa hayajui wakati anampa uwaziri?

Magu nae ni tatizo tena kubwa tu

Kama ingekuwa ni wewe ungefanyaje? Maana katika safu zake alikuwa amebaki yeye. Najua asingemteua mgezungumzia uteuzi wake umewatenga kanda ya kaskazini. Haya bora liende. Leo tena mnaanza kelele. Kwakuwa rais ni msikivu Anaweza kulichukua. Ila nimesikitika kuwasimamisha maafisa wanaosimamia sheria
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Nilishitushwa sana nilipoona kwenye tv Rais anampa pole Katibu mkuu mali asili kwamba kuna watu walijaribu kumzuia asitekeleze majukumu yake ya kuwakamata majangiri.

Nikawa najiuliza kwa ngazi ya katibu mkuu ni nani tena aliyeko juu yake mwenye uwezo wa kumzuia kama siyo waziri and above.

Dawa ya yote haya Rais arudishe Azimio la Arusha kama lilivyokuwa pamoja na katiba ya Warioba. Ni hivyo atakavyoweza kuinyoosha nchi vinginevyo kwa hali tuliyokuwa tumefikia hatua anazozichukua ni sawa ni kumpa mgonjwa wa malaria paracetamol ili kutuliza homa kumbe malaria iko pale pale.

Kwenye ujangiri hadi watu walibadili utambulisho wa majina yao na kuniita Malikia wa meno ya tembo.

Rais asiishie tu kwenye ujangiri aende hadi kwenye ugawaji wa vitalu vya uwindaji huko ndiyo balaa
 
profesa huyo jaman!!.. ... maoni yangu mtu anpokua na level ya uprofesa bac asipewe mamlaka yoyote yale...,,
source. elimu , cuf, maliasil.....
Sijui kwanini maprofesa wengi wanafanya mambo ya ajabu kuliko hata division five ona lipumba.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Kwa hiyo kama ulionyesha wasiwasi ktk uteuzi wa prof maghembe Mbona ulikuwa kimya ukawa unashabikia uteuzi wa mtukufu. Si maghembe tu kuna wengine kati ya wale waliitumbuliwa kwenye sakata la escrow, domo kaya, yule wa viwanda anayewaambia wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wajenge viwanda vidogovidogo
 
Kama waziri huyu anahusika kwenye hili naomba sana mtukufu amtumbue haraka kwani hii ni dharau kwa watanzania
 
Kama ingekuwa ni wewe ungefanyaje? Maana katika safu zake alikuwa amebaki yeye. Najua asingemteua mgezungumzia uteuzi wake umewatenga kanda ya kaskazini. Haya bora liende. Leo tena mnaanza kelele. Kwakuwa rais ni msikivu Anaweza kulichukua. Ila nimesikitika kuwasimamisha maafisa wanaosimamia sheria

Angetafuta mtu mzuri wa kasakazini akamteua kuwa mbunge na waziri
 
Sijawahi kumkubali Prof hata siku moja.
 
Huwa sielewi ni kwa nini huwa anateuliwa. Inefficient person.
 
Magufuli anathani mtu anaitwa prof au Dr basi wana akili za ziada. Waliotufikisha hapa ni madr na Prof
 
Hakika Mkuu. Kuna watu wanaendekeza maslahi yao binafsi. Wakitumbuliwa eti watu wanajitokeza kuwatetea
Hakuna,, tatizo siyo Maghembe bali ni mamlaka ya uteuzi ndo ina matatizo. Yeye mwenyewe si ndo alitamba kwamba yuko makini kwenye uteuzi? Mbona mambo yanazidi kuharibika tu!! Ila ngoja wamtumbue akalalamike tena huko nje na kuanza kumponda mteuzi wake kwamba hana uwezo!! Yetu macho wacha tushuhudie match kubwa hapa!!
 
Jamaa aliteuliwa ,ili kukAmilisha ile dhana ya kaskazin lazma kuwe na waziri na c utendaji wake
Nape ashawai kasema n mzigo enzi za jk.
 
Maghembe siyo kiongozi shupavu ni msanii flani tu hivi anaongoza kwa kuvizia tu.
 
Maghembe siyo kiongozi shupavu ni msanii flani tu hivi anaongoza kwa kuvizia tu.
 
Back
Top Bottom