figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ameoneshwa kusikitishwa na baadhi ya masuala yaliyowasilishwa na Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Nchini kinachoongozwa na Mwenyekiti Prof. Rwekaza Mukandala kwa kueleza kuwa baadhi ya masuala hayo yaliyowasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kupitia kwake kwa Umma si miongoni mwa yale waliyokubaliana kwenye mkutano wa Baraza la vyama vya siasa uliofanyika Jijini Dodoma
Akizungumza na Wanahabari kwenye makao makuu ya Ofisi za Chama hicho Jijini Dar Es Salaam Prof.Lipumba amefafanua kuwa kwenye Mkutano huo ambao ndio uliopelekea kuundwa kwa Kikosi Kazi hicho hakutokea Mjumbe yeyote aliyependekeza kuwa mchakato wa Katiba mpya ufanyike baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, hivyo ameeleza kuwa ameshangazwa kusikia Prof.Mukandala na Kikosi cahe wanawasilisha jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya Wajumbe wa Mkutano huo
Mwenyekiti huyo wa CUF amewataka Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho kufanya kazi wanayopaswa kufanywa badala ya kuanza kugeuka na kufikiri wanamtumikia Rais au Serikali