Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Kitila sasa amejulikana rangi Yake! Nakumbuka mh.Rais alipokuwa Zanzibar alisema hata diriki kuteua wapinzani kwenye serikali yake,kwahiyo alichokifanya Leo ametuonyesha watanzania wenye macho ya rohoni rangi ya chama cha ACT.

Nilikuwa naota tu
 
Mbona kuna yule jamaa aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akakataa?
Kuwa mkuu wa wilaya ni sawa na kiranja,unakimbizana na wananchi,malipo kidogo,huyo jamaa alikuwa na haki kukataa,alikokuwa malipo ni mara tatu ya malipo ya mkuu wa wilaya.
 
Nina bachelor ya Arts with Education tangu 2012GPA 3.96,naomba Rais aniteue japo niwe napanga majalada Ikulu chaki nimezichoka.
 
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
Nitashangaa nikimuona mhadhiri huyu mwandamizi akiapa. Ndio nitajua siasa ni kitu gani?
 
Huu utaratibu wa kuteua wasomi tu ambao ni waalimu na wataalamu kutoka vyuo vikuu hasa cha Dar es salaam si mzuri maana rais haonyeshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao,tuache wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaalamu.
Prof.Kitila Mkumbo
ITV- 17/4/2016
 
Nina bachelor ya Arts with Education tangu 2012GPA 3.96,naomba Rais aniteue japo niwe napanga majalada Ikulu chaki nimezichoka.
Yaani 2012 tu umeshachoka chaki??? Waliomaliza 1980s - 90s sijui waseme nini. Ningekushauri kama kweli umechoka chaki, umri wako bado mdogo, soma kozi zingine ambazo hazihusiani na chaki. Kuna Engineering, Medicine, Law nk. Kapige shule kijana, uachane na chaki.
 
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
yeye anataka tu kaUjumbe kule EALA.
 
Back
Top Bottom